Sii kwa kujua bali kwa imani tunammwendea Mungu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sii kwa kujua bali kwa imani tunammwendea Mungu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiby, Jan 27, 2010.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Ama ndani ya biblia katika kitabu cha methali 3:5 kuna onyo hili. 'mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitumainie akili zako mwenyewe.
  Kwa wale wanaozitumainia akili zao wanapaswa kukumbuka kuwa, elimu ya dunia hii itakusaidia katika fedha, riziki lakini kumbuka jambo moja huna budi kufa. Sasa hiyo haidhuru una elimu kiasi gani. Mkristo hawi mkristo kwa kujiunga na dhehebu fulani au elimu fulani ya kundi fulani, mkristo ni mkristo kwa kuzaliwa upya katika ufalme wa Mungu. Maana isipokuwa umeteulowa kuzaliwa upya hauwezi, kwani Bwana Yesu alisema hakuna awezae kuja kwangu asipokuwa amevutwa na baba, na wote aliyonipa baba watakuja.
  Hakuna mahali hata pamoja katika biblia, panapotaka watu kulielewa neno la Mungu zaidi ya kutakiwa kuliamini. Kwani kama unalifahamu(elewa basi unabatilisha imani. Kama ningelikuwa namfahamu Mungu isingenibidi kumwamini. Vivyo hivyo silifahamu neno la Mungu ila naliamini kwa kulikubali.
  Katika ayub 38:2-4 kuna maneno haya 'Ni nani huyu atiae mashauri giza kwa maneno yasiyo maarifa? Basi jifunge viuno kama mwanamume, maana nitakuuliza neno nawe niambie. Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema kama ukiwa na ufahamu.
  BWANA MUNGU WA MANABII WATAKATIFU NA ATUJALIE KULITAFAKARI NENO LAKE KWA KULIAMINI.
   
 2. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ameeeni pia katika mithali hiiyo hiyo 1 :7 imeandikwa, 'kumcha Bwana Mungu ni chanzo maarifa' hivyo kwa kukosa kumcha Mungu utakosa maarifa, je utajuaje kuwa kuzini ni dhambi pasi na kumcha yeye au kumtii yeye aliyeagi usizini ? hii ni amri ya sita katika amri zake Mungu. Maana pia katika kitabu cha Yohana imeandikwa ' aliyekwisha oga hahitaji kuoga tena bali kunawa,......pia anayemcha Mungu anahitaji kutekeleza yale aliyo amuliwa na Mungu, wapo watu wanao dhani kuwa anatambua utakatifu kwa mahudhurio ya kwenye nyumba za ibada au kuvaa kanzu na hijabu, hapana bali ni kwa matendo mema mbele zake. Maana kama ilivyonenwa ya kuwa Mungu hamhukumu mtu kwa mavazi, vivyo hatamhukumu mtu kwa chakula, unaweza usile nguruwe kwa madai ya kuwa ni haramu lakini ukawa mshenzi wa wake za watu,
  lipi sasa lililo jepesi kula nguruwe lakini usitembee na wake za watu? ama kuhudhuria kanisani huku wazini na wake za watu? Hivyo kumbe ni rahisi tu ukaupeleka mwili kanisani lakini moyo wako ukawa kwednye uasherati.....Mungu na atusaidie
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Jan 27, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Dear Kiby, asante kwa ujumbe mzuri but I beg to differ with you in some issues, especially to understand the word of God.

  Ephesians 5:15-20


  15 Be careful then how you live, not as unwise people but as wise, 16making the most of the time, because the days are evil. 17So do not be foolish, but understand what the will of the Lord is

  The bible is clear that we do need to understand the will of God, we can only understand the will of God through studying the bible.


  First stage

  To understand the bible you need first to believe that is the word of God, breathed and inspired by HIS spirit. Make sure you have Holy spirit to understand it. "all Scripture is God-breathed and is useful for teaching, rebuking, correcting and training in righteousness, so that the man of God may be thoroughly equipped for every good work"


  Second stage

  Once you believe that is the word of God can help you,then you need to search, we have so many questions that answers are in the bible! look examples of Bereans!Paul said that the Bereans(WABEROYA) were of more noble character than even the Thessalonians because of the eagerness to search the Scriptures that they exhibited.

  angalia uumbaji wa binadamu, anguko la Adamu, kuja kwa Yesu kufa na kufufuka, You need to understand the theory behind, the mechanisma behind, you can not just believe something blindly! kuelewa kuja na mission ya Yesu ndio kuna kuza imani! Bible tell us that "So then faith comes by hearing and hearing by the Word of God". Understanding the word of God is the key in the life of believer

  Kumbuka sio kila kitu unaweza kuelewa,uivyoelewa ni kumuomba Roho Mtakatifu akueleweshe.


  Third stage

  Interpretation the word of God is probably the biggest failure that church is encoutering today! People do interpret bible so that they can compromise with the situation or for their own benefits.

  There are many christian practise that denounce bible today! there are many things that are unexplainable all by the name that ''BELIEVE''

  Kuna watu wanasema Yesu anakuja April, wengine wanaweza kwenda Europe kwa ndege kuhubiri injili-bure, kuna wachungaji wanawaunganisha vijana waoelewe makanisani na mengine mengi ambayo nikiandika hapa, utaona KABISA YOUR CONCEPT kuwa uamini tu hata bila kuelewa is wrong.Kumbuka pia waumini wengi hawasomi biblia,na wanawaheshimu sana wachungaji kiasi cha kusema NDIYO.The very same bible tells us to test spirit, chunguzeni , jaribuni....

  Your argument could be right kwa mtu ambaye ni mkristo tayari na ambaye anajua Roho Mtakatifu na ambaye kwa muda huo hajaelewa neo la Mungu ila ataelewa baadae au akiuliza , ila sio kumeza tu kila kitu! thats why Holy Spirit is present now! NENO LA MUNGU NI ZURI NA PANA na maskini kuna watu wanaangamia kwa kukosa maarifa.MUNGU ANASEMA TUWE NA MAARIFA!


  Kuelewa biblia kuna kupa urahisi wa kuedefend imani yako;

  Unachofanya hapa ni kuthibitisha watu hawana ROHO MTAKATIFU, hawawezi kuelewa neno, so waamini tu!!! hata kama mchungaji kabadili maana ya neno waamini tu!! kuna wahuni wamejifanya wachungaji wakatransalte neno la Mungu na kulala na wake za watu!!

  Lastly; please do not compromise with God's word by anyhow, some churches dont follow the bible!!! hao ndio wanasema aminini kila kitu!

  kwingine uko sawa ila point ya kuamini kama sina akili NO-BIG NO!

  Nisipoelewa najua tatizo ni mimi; I will ask father to make me understand!
   
 4. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante kwa somo kiby.
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Waberoya. Ninafahamu kwa hakika kwamba kila kitu lazima kijaribiwe, na ukiri lazima ewe wa kweli, na fundisho sharti liwe sahihi. Sasa vitu hivyo havitangulii imani. Kwani imani ndio msingi na ufunguo kwa Mungu. Maana imeandikwa haimpendezi Mungu bila imani. Na vipi basi waweza je kujifunza kwa kusoma kitu usichokiamini? Kufafanya hivyo kumepelekea kuwe na watu wanaomfahamu Mungu bali hata hivyo hawamwamini. Na hii ni sawa na ebrania 6:4-6 na ebrania 10:26 inayozungumzia watu waliokwisha pata ujuzi wa kweli, kisha wakaanguka haifai kuwarejesha tena. Hapa hazungumzii watu walioamina na kuzaliwa katika ufalme kisha wakaanguka, la hasha! Watu wa namna hiyo hawapo. Isingeliwezekana kamwe leo Yesu asema wote walio katika mikono yangu hakuna awezaye kuninyang'anya halafu kesho aseme na kama nikinyanganywa haiwezekani kuwarejesha. Kuamini unaamini kama kipofu au kama mtoto mdogo na ndivyo Bwana Yesu alivyosema: aaminie na kubatizwa ndie atakaeokoka, na wala kamwe haiwi ajifunzae na kufahamu ndie atakaeokoka. Au na ishara hizi zitaambatana na hao waaminio, na wala sii ishara hizi zitaambatana na hao wajifunzao. Kupima roho ni kwa neno la Mungu lililoaminiwa na wala sii kwa tafsiri za watu kumhusu Mungu, maana hatuzaliwi upya kwa tafsiri na mafafanuzi ya watu kumhusu Mungu bali kwa imani ya kweli ya Mungu kama ilivyoletwa na hao watumishi chini ya uvuvio wa Roho mtakatifu wake. Unapozungumzia kuhusu Mungu kuwataka watu wawe na maarifa, ni maarifa gani hayo? Maana neno la Mungu linasema hekima ya dunia hii ni upuuzi mbele za Mungu. Pia usisahau kwamba Adamu alikatazwa kula katika mti wa ujuzi wa mema na mabaya MWANZO 2:17. Yaani hapa Adamu alitakiwa kwa kukiamini kile Mungu alichomwambia na wala sii kwa kutafuta maarifa na kuhoji.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Amen.
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Jan 28, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  You see! kwa hiyo unataka kusema neno la Mungu linajicontradict? ona ulivyochanganya neno maarifa na hekima! Mungu anasema watu wangu wanahangamia kwa kukosa maarifa, wewe unataka kunegate this statement kwa 'Hekima ya wanadamu ni upuuzi mbele ya Mungu! unasema kitu tofauti kabisa.

  kwa maana nyingine kuifuta sentensi ya biblia kwa neno lingine la biblia ni alama ya kuwa inabidi kuelewa neno la Mungu kiundani.

  Kila ulichosema kiko sahihi ndugu,rudia stage ya kwanza.UKISHAAMINI BIBLIA ni neno la Mungu basi ndio msingi wa kuanzia hapo. Ila siyo kila unachokisoma au kuhuburiwa ukichukue kama kilivyo kwa kisingizio cha Imani! you need to understand it!

  Yesu(ambaye ni neno ata kuwezesha kuelewa andiko) mfano unaweza ukasoma agano la kale na kuyachukua baadhi ya mambo kama yalivyo, usipojua kutofautisha maana ya agano la sasa na la kale unaingia porini na kuleta confusion nyingi sana! haya yapo kila leo; Nadhani unachosema wewe ni kuuliza maswali yale ya kijinga ili hali unamwamini Mungu; LAKINI SIO KUELEWA NENO KWA LENGO LA KUUKULIA WOKOVU, mimi nasema inabidi kila mkristo aelewe neno la Mungu, neno ni Yesu mwenyewe unaposoma unaongea naye-tafsiri nyingi tulizonazo leo inaonyesha kuna tatizo sehemu ndugu! HALAFU kila siku inabidi ukue kiimani, na kukua huku ni kujua neno la Mungu!

  Nasisitiza kuwa na Roho, kumtegemea Mungu akusaidia ndio uelewe andiko.
  1.Sauli alienda vitani, akaua wanyama akatoa sadaka mbele ya Mungu, ilikuwa makosa
  2. Daudi alihesabu watu;makosa
  3. Ibrahim hakumuelewa Mungu, akazaa na mjakazi!
  4. Petro hakuelewa mission ya Yesu mpaka akafundishwa na Paul kuwa asiwatenge wamataifa
  5. Kuna watu wengi waliozaliwa mara ya pili wanawatenga watu wasiomjua Mungu! kuna andiko linasema jitengeni nao, na kuna andiko linasema shirikiana nao! lipi la kuamini? lazima mtu aelewe neno la Mungu hapa
  6. Kuna wakristo fulani ninawafahamu baada ya kujua Mungu anajaibu maombi, hawafanyi kazi! lakini the same bible inasema asiyefanya kazi na asile!
  7. Kuna andiko linasema unywe pombe kama dawa ya tumbo, mtu asipoelewa ni kitu gani hasa anaingia chaka
  8. Msingi wa makanisa yetu mengi kuna taratibu zinazoendelea humo ambazo ziko kinyume kabisa na biblia! yet watu wanaabudu tu , kama vile Mungu mjomba wao kuwa wakijiamulia tu kufanya kitu fulani Mungu anasema Ok!! LAKINI si kuna andiko linawasupport wao, lakini biblia inasema usiongeze wala kupunguza neno!

  Kutokuelewa neno la Mungu kunaendana sana na watu kufanya dhambi!

  Leo hii watu wanatambika, wanatembelea makaburi ya ndugu zao, wanakunywa damu za wanyama, yote haya ni makosa, yet they are in the churches!!

  Nazungumza hili kwa mtu ambaye tayari ameshamjua Mungu na kumpokea Yesu.

  Hatari ya unachokisema ni kuwa utakuwa na wakristo dormant, wanaoamini chochote kile; wakati kusoma na kuelewa neno la Mungu ni mission ya kila siku ili ukue kiimani , unaposoma neno la Mungu unaongea na Yesu !
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Huwezi kujua kitu kisichojulika. Ndiyo maana namuunga mkono huyu anayesema si kwa kujua bali kwa imani tunamwendea mungu.

  Ameonyesha uelewa kwamba ujuzi na imani ni vitu viwili tofauti, tofauti na watu wengi hapa ambao wanakazania kwamba imani ni ujuzi.
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Jan 28, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Nilishatoa angalizo swala la kupost thread ambayo unajua kila mtu atachangia kutokana na mtazamo wake! alitakiwa a clarify the issue from the beginning. Anaongea kwa asiyemjua Mungu kabisa, anayeamini Mungu lakini kwa mtazamo mwingine au mtu kama yeye. nilishasema hapa atakayeelewa ni yule anayemjua Yesu tayari.


  Here we go again! tunarudi pale pale, umekubaliana naye na kuchukua alichosema for your advantage, ambayo yeye anajiweka kwenye wakati mgumu sasa

  Kiranga, Mungu tunayemwabudu siyo 'kitu kisichojulikana' Ni Mungu halisi, hakuanza kujidhihirisha kipindi cha Yesu tu,

  1. Ndiye aliyempa Musa mbao za amri kumi
  2. Ndiye aliyewaonyesha waisrael nguvu zake kwa kuwavusha bahari ya shamu
  3. Ndiye aliyemfanya Shadrack, meshack na abednego kutokuunguzwa na mto wa tanuru
  4. Ndiye aliyemwezesha Joshua kusimamisha jua kwa siku!
  5. Ndiye...


  Mungu akajifunua kwetu kupitia Yesu Kristo, Yesu ametufunulia yaliyopita, yaliyopo na hata yajayo.

  Mungu tunayemsema is real sio kuwa hajulikani anajulikana HE is real. If you can feel him in your heart,if he can purge and wash your sin, if you can experience some miracle like healing, if you can feel joy if you can feel the touch of Holy spirit! IF you can say hello! look! I was sinner, today I am no longer walking on those evil ways THEN this God is real!!

  What I am emphasing here is that God is not the author of confusion we have every answer from the bible! some issue need to grease our faith so that we may grow stronger and are understandable and straight foward.

  Kuna neno linasema ombeni bila kukoma! so we can stay praying day and night because the word says so? that what I am trying to say here

  Ujuzi au maarifa ninayoyasema hapa ni yale ya kuishi kama Mungu atakavyo, maarifa ya kujua neno lake, maarifa ya kutambua kipi ndicho na kipi sicho, maarifa ya kuweza kutambua hili si la Mungu na hili la Mungu!

  By the way welcome to our faith brother I can see your are real interested to know God. Surely, you will know him

  Remember HE loves you, even if you will deny!

  .
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,168
  Trophy Points: 280
  Amen.. ubarikiwe sana Mpendwa.
   
 11. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Waberoya, Mimi nilchokuwa najaribu kuonyesa hapa ni kitu IMANI kama ufunguo wa kumwendea Mungu. Kwani najaribu kuzingatia tafsiri ya Paulo katika waebrania kwamba imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyo onekana. Sasa ni kwa nini yasiyoonekana? Kwa sababu Mungu ni Roho nao wamwabuduo yafaa wamwabudu katika roho na kweli. Sasa mambo ya rohoni hayathibitishwi kimwili, ila jambo uliloliamini na kulichukua kuwa lako ktk ulimwengu wa kiroho, Mungu anapoithibitisha imani yako kwa mathihirisho ktk ulimwengu wa kimwili haibaki tena kuwa imani bali halisi (proofs) kwa mfano jiulize ni nini kilichowazuia wakuu wa kidini kukataa ujio wa Yesu ilhali walikuwa wakiyasoma maandiko daima na hata kulala wakijifunza hekaluni na ktk masinagogi yao? Hata yesu kulazimika kutoa maneno haya: 'mnayachunguza maandiko mkidhania mna uzima ndani yake, na hata hivyo hayo ndiyo yanayonishughudia. Hayakufanya kazi kwa sababu walizitumainia akili zao wenyewe za kiuchunguzi na kujiridhia kabla hawajaamini. Lakini kina petro ambao hata hawajasoma waliamina na hivyo wakapokea nguvu na ewezo mkuu hata watu wakaanzo kusoma kutoka kwao nakujipachika degree za kiungu (DD). Mimi naamini kwamba uwepo wa roho mtktf kwa dakika tano tu ndani ya mwamini unaweza kumpa ufahamu ambao huo utafundishwa na waalimu hata kwa zaidi ya miaka mia. Ndio maana kamwe huwezi kumpata nabii wa mungu aliyekuwa mwanachama wa muungano au kundi lolote lile la elimu fulani. Hivyo nasisitiza Mungu ni kwa imani na sii kwa kujua.
   
 12. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  asante kwa somo zuri sana , Mungu akubariki
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Vyote vinaenda sambamba...vinatgemeana..ni muhimu kumtumaini Bwana lakini vile vile ni muhimu kutumaini akili...Biblia hiyo hiyo inasema..watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa...Maarifa yanayotajwa hapa ni yote ya MUNGU na ya dunia.....Mistari hii ya kumtumaini Bwana peke yake ilileta utata wakati ulokole unaingia hapa Tanzania..watu walipokuwa wakiumwa walikuwa hawaendi hospitali kwa kigezo kuwa mtumaini Bwana kwa kila jambo...watu wengi walizika wapendwa wao kwa ujinga huu.
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  1) when did man started leaving in this earth?
  2) when did the bible started? or rather when did those who wrote the bible came into existance?
  3) there were men on earth before the bible?
  4) if the bible is made of stories/events of the past of the believers and non believers, why did the writings of those events ceased at some point?
  5) If apostles wrote what they were preaching, (and that is supposedly made into the word of God) why is it that todays preachers dont write what they are preaching? and even if they do so, it will never made into the word of God - bible?
  5) Who is ths Holy Spirit - the spirit that inspire men differently, the spirit that lead different "men of God" into interpreting the "bible" differently - the claim that there will be fake pastors is off limit here! who determine the end of the world? events? surely, there have been events since time ememorial - and the end has never materialised.
  6) If God instracted his people those days (surely, He love every one of us) why is he not instracting his chosen brothens in christ on what to do to solve the problems that his people whom he loves very much, saffer from.

  Just Curious!!
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  asanteni sana wapendwa kwa kutupa mistari ya maneno matakatifu mbarikiwe sana na bwana pia muenende kwa hekima siku zote
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Can you prove the 5?

  Mbona amri kumi zina inconsistency katika sehemu tofauti katika biblia?

  Kama alisimamisha jua, na dunia iliendelea kulizunguka jua, mbona duniani siku ilisimama? Hii si inconsinstency iliyotokana na ignorance ya watu wa zamani waliofikiri jua linazunguka dunia na si dunia inazunguka jua.I mean if any part of the bible can show you the bible was written by ancient men and not god it is this. Kwa nini mungu hakusema alisimamisha dunia halafu tuje kuelewa baadaye?

  Mungu ni hogwash.
   
 17. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Amina Baba!
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Jan 28, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  I knew it!

  kuwa utakuja tu na theory zako, please I am not able to discuss this right now, ila haukutakiwa kuingia kwenye mjadala huu, wewe hauamini existence ya Mungu. Kuna kitu kinakuchoma eh!

  Please anzisha thread yake huku tunaajenda zetu tunaomwamini Mungu!
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Jan 28, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  I will be back
   
 20. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Kutokuzitumainia akili zako tunakokuzungumzia hapa ni pala mtu anapofanya jambo lolote na kufikiri moyoni mwake kwamba kwa uwezo wake na elimu yake na nguvu zake zimemwezesha kufanya hivyo. Na wala asitake kusikia kwamba kuna nguvu nyingine yeyote iliyoshiriki katika kumwezesha. Akili aliyo nayo anafikiri kwamba huo mfumo mzima wa ufahamu ni stahiki yake iliyojengeka kwa uwezo wake mwenyewe. Hata kama ni matumizi ya dawa kitu ambacho hakijakatazwa na Mungu yeye atafikiri kile kinachotokana na hizi dawa kwa mfano wa miti majani mizizi, matunda nk havingeweza kuwepo ila kwa utaalamu wake wa kiuchunguzi. Sasa mawazo ya watu wa namna hii ndio tunaosema wamezitumainia akili zao wenyewe na jawabu la miyoyo yao ni kwamba, hakuna Mungu.
   
Loading...