sihitaji kuolewa je ni tatizo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sihitaji kuolewa je ni tatizo?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Latifaa, May 31, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Latifaa

  Latifaa JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 474
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  nimetimiza miaka 30 sasa, huko nyuma nilitamani sana kuolewa nanilikuwa namlilia mungu sana anijalie nipate mume bora hiyo ndio ilikua
  dua yangu kubwa kwa mungu, imekua bahati mbaya sijaolewa wala kuchumbiwa na mwanaume yeyote nimeishia kurubuniwa na kutapekliwa, nilitamani sana niwe na mume wangjt nimthani na kumjali ila baha ti ni mbaya sijabahatika.
  Any way 4 sasa nimekua mtu mzima nimepata akili nimepitia mengi na nimejifunza mengi nanimetafakas4ri kwa kina n.ifmegundua sio kila unalolipanga kwenye maisha yako lazima ulipate hata ukimwomba mungu mengine inabidi usacrifise, japo utavumilia masengenyo kutoka kwenye jamii na mitazamo hasi kwa ndugu hata wazazi.
  Leo hii nimekua mtu mzima sitamani kuolewa tena wala sivutiwi na ndoa yoyote hata mwanaume wa kuishi em3.
  Napenda kuwa na watoto wawili nakupambana na däisha bila kujali baba yao atakua nani..
  Nayafurahia maisha yangu na maamuzi yangu kuliko zamani nilivyokua nahitaji kuolewa najiona nimeshakua
  mama nanina familia isiyokua na baba ninafuraha sana naninamshukuru mungu kila kukicha.
  Sipendi kuolewa na sivutiwi na kuolewa wala ndoa sihitag!
   
 2. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 837
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  Tatizo kubwa, kwa nini usiolewe kama uko sawa?
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  Mh!Sijui nikupe pole au vp,lakini ungejua kama wewe mwenyewe ndo msababishi wa yote yaliyotokea maishani mwako usingelaumu!
   
 4. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mhm haya dada yetu naona poa tuu kama hutaki kuolewa.
  ila kama hutaki kuolewa basi ukubaliane na fact kuwa uamuzi huo unakuja na kukubali kukosa chance ya kuwa mama.
  najua wengi wanasemq watalea wenyewe lakini hiyo ni selfishness. so usiolewe na pia usipate mtoto kuwa alone alone
   
 5. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mpe MUNGU heshima anayostahili! Umendika neno 'mungu' mara nne; yawezekana maombi yako yote ulilenga kwa mungu (semi-god), ambaye hatakusaidia kamwe! Funguka, ni MUNGU siyo mungu!
   
 6. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Unaitaji maombi dear. Uko na majiraha ambayo dawa yake ni maombi. It is just a matter of time factor.
   
 7. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Ni maamuzi mazuri kama utasimamia mtazamo huo. Shida tu ni kwa wale wanaotamani tena kuolewa bahada ya kujiapiza kama wewe na wakati umeshapita.

  Mimi niliolewa na miaka 29 na sikuwahi kujiapiza kuwa sitakuja kuolwa na sikuwahi fikiri wala kusumbuliwa na mtu kuwa kwa nini siolewi kwani nilikuwa kwenye serious relationship for 4 years na ndiye mume wangu kwa sasa.

  Sasa usijesema hutaki kuolewa kwa kuwa umekata tamaa; kwani maneno uumba. Miaka 30 ni umri muafaka wa kuolewa na wala hujachelewa kihivyo ila unafall kwa wrong men ungekuwa na wanaume husband material ungekuwa na mtazamo tofauti na huu.
   
 8. Bufa

  Bufa JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 4,168
  Likes Received: 3,376
  Trophy Points: 280
  Enjoy your life.
   
 9. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  miaka 30 mbona bado unamuda kwa miaka ya siku hizi?
   
 10. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Umesema umeshaamua halafu unauliza kama ni tatizo?!

  Swali lako ni dalili kuwa hujiamini na hujui unachofanya. Nachoona hapa ni kuwa unaamini kuwa umri umekuacha na umekata tamaa sasa unataka maoni ambayo yatakufariji. Si jambo jema kujidanganya, kama kuolewa utaolewa hata ukiwa na miaka 50, cha msingi ni kuwa usikae ukaacha kufanya mambo mengine ukisubiri ndoa au kufanya uwindaji uwe ndio shughuli yako ya msingi.

  Ningejua maisha yako angalau kwa kifupi ningeweza kubaini ni kwa nini uliishia kudanganywa na kwa vipi utaliepuka hilo.
   
 11. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Labda kama ana mpango wa kulea watoto yatima. Lakini kama ana mpango wa kuzaa na waume zetu that is more than selfishness. Kwanza anawapa watotowake label mbaya katika jamii pili anaharibu nyumba za watu ambao wana imani na ndoa.

   
 12. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Yale mambo yetu unashiriki? If yes basi fikiri mara mbili kuhusu msimamo wako! Isije kufika mwaka 2014 ukamdondokea jibaba!
   
 13. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Maisha ni uamuzi..na huo ni uamuzi ukiacha yote uliyopitia!!
   
 14. Latifaa

  Latifaa JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 474
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  nimelelewa maisha ya dini na
  nina mheshimu mungu nina maadili na heshima ila ninachokiamini sio lazima
  kila unachoomba upate, dmndio maana maisha yametofautiana matajiri na
  maskini sio kwamba maskini hawaombi nao pia wanaomba ila ndio hivyo, sio lazima kila bidada aolewe
   
 15. Latifaa

  Latifaa JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 474
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  kwahiyo kama sina ndoa na kizazi pia sina? Kuzaa dumuhimu
   
 16. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unajuwa kwanini Mola aliweka ndowa? Ni kwasababu binaadamu awe tofauti na mnyama.
  1.Hamu yake isiwe kama ya mnyama ya kuchupia alie karibu nae tu au kupanga foleni kutimiza hamu ya mwili
  2. Kuwe na mpangilio mzuri wa kizazi chenye kuelewana na siyo kuzaa bila ya kujuwa damu ya nani.
  3. Tuwe na vigezo vya kukubaliana kufanya uhusiano wa Kibinaadamu (kumbuka kuwa tumeppangiwa ndowa ili iwe njia ya kibinaadamu)
  Mwisho, ni kuwa si lazima kuowa au kuolewa lakini ulazima wa kuheshimu mpango uliowekwa na mola. Hutaki kuolewa basi ipige maji ya moto tu wala huna makosa.
   
 17. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  wanaume tumejaa tele ni ww tu labda hujui kutanua mabawa kama ndege tausi ili kutuvutia
  jitahidi mama kuzaa na kulea bila baba sio kazi rahisi kama unavodhani
  toa dhana yako potofu na omba sana pepo la kukataliwa likutoke
   
 18. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Inategemea kama unaamini kuwa kuna kitu kinaitwa dini.

  Nasema hivyo kwa kuwa nilikuwa na class mates watano wanatokea Malaysia walikuwa wanasomeshwa masters an nchi yao. Wote ni mabosi huko kwao, ila walikuwa wote ni single. Walikuwa wanaonekana wadogo ila walikuwa na more than 30 mmoja alinambia ana 35. Walikuwa hawajaolewa. Katika kundi lao ambalo walikuwa kama 15 wanasomeshwa na serikali yao kulikuwa na wanaume; wote wameoa na walikuwa wamekuja na wake zao huko masomoni. Walikuwa rafiki zangu sana nilikuwa nawauliza sasa nyinyi hamjaolewa hamtaki watoto; wakanambia si kuwa hatupendi kuolewa ila kwetu ukiwa msomi na chance ya kuolewa inapungua. Ni kweli wale wanaume wa Ki Malaysia wake zao walikuwa hawajenda shule kihivyo; ni housewives.


  Walichonifurahisha wale wadada ni kuwa walinambia NK wote tuna mpango wa kulea watoto yatima kwa sababu sheria ya Kiislamu hairuhusu kuzaa nje ya ndoa.

  Ndio maana nikasema inategemea kama una dini na unaishika kweli.
  Maana siku hizi naona hata Obama karuhusu ndoa za jinsia moja. Dunia inaelekea kusiko.

   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280

  Bi Latifaa kama roho yako imeridhika na mfumo wa maisha uliokuwa nao wa kuishi bila mume na siku za usoni hutakuja kujutia uamuzi wako huo basi hakuna tatizo lolote lile. Kupanga ni kuchagua hivyo furahia maisha yako....Kila la heri
   
 20. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Sasa utazaa na nani? Manake vijana wanataka kuoa. Kama ni mume wa mtu hakikisha unabaka mwenye possibility ya kukuoa japo mke wa 7 manake siku hizi wamama wakali hawasusi ndoa wala nini! Ndio nyie unazaa na mume wa mtu afu unamsaka mkewe unamuelezea!
  Una tatizo wewe aisee, ongea na wakubwa wako...
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...