Sifa za mwendazake na hali halisi..

Sifa za mwendazake na hali halisi..

ndiyo maana Jiwe alitamani atawale milele akifahamu haya madudu yake yasingefahamika
 
Tumeambiwa Mwendazake alifanikiwa kufuta ufisadi serikalini na nidham ya kazi akarudisha..Leo mmoja wa wateuliwa wake DG wa TPA katimuliwa Kwa upotevu wa bilioni zaidi ya 3...

Halafu tukaambiwa alifufua shirika la ndege

Leo tunaambiwa shirika la ndege linaleta hasara ya bilioni 60 kila mwaka
Kwa ufupi halijawahi kuleta faida...

Mimi kama sielewi ...
Au zile sifa zote na kilichopo vinaendana?
Yeye alikuwa anaanzisha tu bila kujali faida!
 
Watanzania tukiwekewa kichwa cha habari tunajazia content..kakonko hajafukzwa kasimamishwa kupisha uchunguzi...yeye km mkurugenzi ana kua responsible ya kila kinachoendelea chini...na uchunguzi ulianza tangu marehem yupo hai uliopelekea mkurugenzi fedha wa TPA kusimamishwa na waziri mkuu...
 
Jinsi vijana wa jiwe walivyokua wakikosoa awamu zilizopita kwa zile kauli kama:

"Haijawahi tokea tangu tupate uhuru" mara "imevunja rekodi " na nyingine nyingi sasa ni muda wa payback watulie nasi tupate kujua awamu hii yaliyotokea wao wakiwa kwenye usukani muda ni hakimu mzuri
 
Imagine Magu angefanikiwa kuibadili Katiba ili atawale milele yaani Raisi wa Maisha? upigaji ungefikia viwango cha kutisha
 
Tatizo lake lilikuwa si kufuta uffisadi bali lilikuwa ni anaye fanya ufisadi ni wa upande upi? Je upande unao muhusu au usio muhusu?

Kwani unataka kuniambia hakujua kwamba shirikal la ndege linaLiingizia taifa hasara? Alijua vyema sana lakini hakutaka hilo lisemwe hadharani kwa sababu yeye ndiye muhusika mkuu wa hilo.
Shirika la Ndege kutopata faida sio ufisadi. Kama unamtuhumu kwa kufufua shirika la ndege lisilozaa faida ieleweke hivyo, lakini huwezi kusema alilea ufisadi katika shirika. Hayati alilichukulia swala la kufufua mashirika ya umma kama kipaumbele cha awamu yake ya uongozi, hakufanya hivyo kwa shirika la ndege tu. Siwezi kufahamu kilichokuwa kikimsukuma kufanya hivyo ukizingatia kwamba inaonekana nchi hii ubinafsi ni mwingi sana, na kuna watu wapo tayari kuua mashirika ya umma kwa ajenda zao binafsi. Vyovyote vile, the man alikuwa very proud na nchi yake na alitamani aone kila kitu kinachobeba alama na taswira ya Tanzania kinasimama na kuimarika. Mzuka na hamasa yake katika kufufua Air Tanzania unaakisi hilo.
 
Mbona hawa wote wanapigiwa chapuo la mmoja wao kuwa VP! [emoji848]
Hakuna atakaye pewa hapo walikuwa wanataka kufanya huo mpango ndio maana walikwapua Yale mabillion pale BOT baada ya kifo cha Meko lakini tayari wamesha shtukiwa report ijayo ya CAG haito waacha salama stay tune [emoji16][emoji16]
 
Tumeambiwa Mwendazake alifanikiwa kufuta ufisadi serikalini na nidham ya kazi akarudisha..Leo mmoja wa wateuliwa wake DG wa TPA katimuliwa Kwa upotevu wa bilioni zaidi ya 3...

Halafu tukaambiwa alifufua shirika la ndege

Leo tunaambiwa shirika la ndege linaleta hasara ya bilioni 60 kila mwaka
Kwa ufupi halijawahi kuleta faida...

Mimi kama sielewi ...
Au zile sifa zote na kilichopo vinaendana?
Kwenye "Shirika la ndege", labda madudu yatafutwe kwenye ununuzi wa madege hayo!

Uendeshaji wa kuleta faida?... Sidhani. Tena wakati mgumu kama huu?

Pengine lengo lilikuwa ni hizo sifa tu la kuwa na shirika letu la ndege, kama taifa. Kutegemea faida ipatikane katika muda mfupi huu, sidhani.

Inaanza kuonekana sasa hata huko mikoani na wakurugenzi wake hali haikuwa nzuri sana!

Kama ni 'legacy', bila shaka itaanza kuwa nyembamba, kuliko tulivyoaminishwa.
 
Mkuu JPM ni binadam kama tulivyo mimi na ww. Ikiwa binadam tulioumbwa na Mungu tunafanya machafu na kukwamisha yale yote anayoyataka Mungu tuyafanye, vipi tutashindwa kukwamisha yale aliyoyataka binadam mwenzetu hayati JPM. Kumbuka kwamba hata malaika walimuasi Mungu wakawa mashetan sasa sijui unashangaa nini baadhi ya watu kuiasi serikali na kukwamisha juhudi za JPM
Ondoeni utetezi wakipuuzi huu ....ushawahi kumsikia mwenyewe akikiri yeye sialikuwa anapenda kuabudiwa tu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Hv yule nguchiro yehodaya cjui kafia wapi???mana co kwa mapambio yake yaliyotamalaki kwa mwenda zake
Jinsi vijana wa jiwe walivyokua wakikosoa awamu zilizopita kwa zile kauli kama:

"Haijawahi tokea tangu tupate uhuru" mara "imevunja rekodi " na nyingine nyingi sasa ni muda wa payback watulie nasi tupate kujua awamu hii yaliyotokea wao wakiwa kwenye usukani muda ni hakimu mzuri
 
Back
Top Bottom