Sifa za mwanamke mpenda pesa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifa za mwanamke mpenda pesa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kimbweka, Dec 16, 2010.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  KATIKA zama hizi – kuliko zama zingine zozote – pesa imepewa kipaumbele kikubwa katika suala zima la uhusiano wa kimapenzi. Mwanamke asiyempenda mtu bali pesa si rahisi kujenga uhusiano wowote wa maana na mwanamume maskini, au yule ambaye hatakuwa na uwezo wa kutimiza mahitaji yake makubwa.

  Hata kama una pesa, ni gharama sana kumfanya mwanamke mpenda pesa kuwa na furaha. Naam, yupo mwanamke ambaye hataki mapenzi wala chochote kwa mwanamume bali faida ya fedha au mali. Huyu hawezi kufurahishwa kwa chochote kile pungufu ya matakwa yake ya
  fedha na mali.

  Katika pitapita zako unaweza kuukwaa mkenge na kujikuta umeingia katika uhusiano na mwanamke wa aina hii, au ukajikuta ukimfukuzia mwanamke huyu ambaye hampendi mtu bali pesa. Unapaswa kuwa mjanja na kumbaini mwanamke huyu kabla hajakupotezea muda na kukuingiza hasara.

  Yafuatayo ni mambo 10 ambayo yatakuonesha kuwa mwanamke uliye naye au unayemfuatilia hakupendi bali anapenda waleti yako: -

  1. ANAPENDA ZAWADI ZA BEI MBAYA
  2. MARAFIKI ZAKE NI WAPENDA PESA


  3. ATATAKA SANA KUJUA MAISHA YAKO  4. HATAGHARIMIA CHOCHOTE, POPOTE


  5. ANAWACHUKIA WANAWAKE WENZAKE  6. HUTUMIA UREMBO WAKE KAMA TANZI


  7. HUPENDA SANA KUONEKANA WA HADHI YA JUU


  8. HUWATUMIA WANAUME KAMA NGAZI  9. MWONEKANO WAKE SI SAIZI YAKO  10. HUJIONA MWENYE KUSTAHILI KILA JEMA


  JIEPUSHE NAYE

  Hakuna mwanamume ambaye kwa makusudi kabisa atataka kuingia katika uhusiano na mwanamke ambaye malengo yake ni kuchuna buzi tu na kuondoka zake. Ni kweli kuwa wapo wanaume wanaolipia mapenzi, mathalani kwa makahaba, lakini angalau mtu anayefanya hivi anajua uhusiano huu ni wa dakika chache na hakuna mapenzi yoyote bali ngono.

  Ukiisha kuzifahamu ishara hizi muhimu za mwanamke mpenda pesa na mali, unaweza
  kujiepusha naye, usije ukaishia kujuta maisha yako yote huku ukiwa umeshapoteza muda wako na mali nyingi, nyumba umeshamjengea na magari umemnunulia. Kumbuka majuto ni
  mjukuu.

  Kama kuna mengine leteni tuongezee ili kuzidi kujilinda zaidi na wanawake wapenda pesa
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Hiyo 1,5,6 10 mmmmmhhhh kiboko
   
 3. M

  Mnyalu wa Kweli JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  It is true!
   
 4. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ni kweliiiiiiiiiiiiii
   
 5. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe ....niliwahi kuwa na mwanamke wa dizaini hiyo , thanks God nilimshtukia mapema
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Na tatizo na hawa watu, huwa ukimpa kiasi anachotaka, say 50K, next time atataka higher amount, harudi chini!....Wengine huweza hata kuazima vitu vya gharama kwa mwenzake ili aonekane wa juu, na hivyo umkatie mafao ya juu zaidi...

  Kuna mtu alinambia kuwa kuna wanawake wanaishi mbavu za mbwa, lakini ukimkuta ametegesha mahali utadhani anamiliki hekalu...complications kibao..hahahaaa!
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Pole sana afadhali ulizinduka:A S-alert1:
   
 8. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  tehe teh usipokaa chonjo unaingia mkenge mmmh:A S-alert1:
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nadhani hizo zote ni sifa wa dada wa kawaida.
   
 10. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna asiyependa pesa...si mwanamke,si mwanaume.:eek:
   
 11. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45

  Je, ni zipi sifa za mwanamume mpenda pesa???? Ziweke hapa ili akina preta, maria roza, first lady, lady n, nyamayao na wengineo wazifahamu na kuchukua tahadhari wasije kuingia mkenge!!!
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  No :nono:
   
 13. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mpenda pesa kupitia mapenzi ya uongo:A S-alert1:
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Dah!Kazi mnayo!Ila wengine sio rahisi kuwagundua!
   
 15. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ngoja watuletee wao maana sisi hili tumeng'amua wenyewe:A S-alert1:
   
 16. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jamani wanawake wa aina hii ndio nawataka. Hata jana niliomba wajitokeze. Mwanamme tafuta pesa, mwanamke atumie. Nimekoleza kwa wino wekundu 1,4,7-9 kuonyesha kuwa wanawake wenye sifa hizo ndio niwatakao mimi.
   
Loading...