Kimbweka
JF-Expert Member
- Jul 16, 2009
- 8,597
- 1,683
KATIKA zama hizi kuliko zama zingine zozote pesa imepewa kipaumbele kikubwa katika suala zima la uhusiano wa kimapenzi. Mwanamke asiyempenda mtu bali pesa si rahisi kujenga uhusiano wowote wa maana na mwanamume maskini, au yule ambaye hatakuwa na uwezo wa kutimiza mahitaji yake makubwa.
Hata kama una pesa, ni gharama sana kumfanya mwanamke mpenda pesa kuwa na furaha. Naam, yupo mwanamke ambaye hataki mapenzi wala chochote kwa mwanamume bali faida ya fedha au mali. Huyu hawezi kufurahishwa kwa chochote kile pungufu ya matakwa yake ya
fedha na mali.
Katika pitapita zako unaweza kuukwaa mkenge na kujikuta umeingia katika uhusiano na mwanamke wa aina hii, au ukajikuta ukimfukuzia mwanamke huyu ambaye hampendi mtu bali pesa. Unapaswa kuwa mjanja na kumbaini mwanamke huyu kabla hajakupotezea muda na kukuingiza hasara.
Yafuatayo ni mambo 10 ambayo yatakuonesha kuwa mwanamke uliye naye au unayemfuatilia hakupendi bali anapenda waleti yako: -
1. ANAPENDA ZAWADI ZA BEI MBAYA
2. MARAFIKI ZAKE NI WAPENDA PESA
3. ATATAKA SANA KUJUA MAISHA YAKO
4. HATAGHARIMIA CHOCHOTE, POPOTE
5. ANAWACHUKIA WANAWAKE WENZAKE
6. HUTUMIA UREMBO WAKE KAMA TANZI
7. HUPENDA SANA KUONEKANA WA HADHI YA JUU
8. HUWATUMIA WANAUME KAMA NGAZI
9. MWONEKANO WAKE SI SAIZI YAKO
10. HUJIONA MWENYE KUSTAHILI KILA JEMA
JIEPUSHE NAYE
Hakuna mwanamume ambaye kwa makusudi kabisa atataka kuingia katika uhusiano na mwanamke ambaye malengo yake ni kuchuna buzi tu na kuondoka zake. Ni kweli kuwa wapo wanaume wanaolipia mapenzi, mathalani kwa makahaba, lakini angalau mtu anayefanya hivi anajua uhusiano huu ni wa dakika chache na hakuna mapenzi yoyote bali ngono.
Ukiisha kuzifahamu ishara hizi muhimu za mwanamke mpenda pesa na mali, unaweza
kujiepusha naye, usije ukaishia kujuta maisha yako yote huku ukiwa umeshapoteza muda wako na mali nyingi, nyumba umeshamjengea na magari umemnunulia. Kumbuka majuto ni
mjukuu.
Kama kuna mengine leteni tuongezee ili kuzidi kujilinda zaidi na wanawake wapenda pesa