Mimi maoni yangu ni haya:
Kwenye hiyo picha naona mwanamke ametimiza jukumu lake
Ninavyofahamu mwanaume ni kichwa cha familia, mlinzi wa familia yake, na katika yote familia lazima iwekwe mbele kabla ya vitu vyote kwa sababu hawa ndio watakaokujali wakati unaumwa, watakaokufariji wakati wa shida mfano kifedha na kukumotivate, na ni kazi ya mwanaume kuprovide kwa ajili ya familia yake wala sio jambo ambalo anatakiwa ajisifie (kwa mfano hatusifii t.v ikiwa inaonesha picha kwa sababu ndicho inachotakiwa ifanye) wala nini ni kazi ya mwanaume kufanya kazi kutoka jasho kuilisha familia yake,
Mwanamke ni msaidizi wake wa karibu zaidi
Mwanaume anatakiwa ailinde familia yake na physical attacks na spiritual attacks, na anatakiwa aongoze familia yake katika kumjua na kumtumikia Mungu kama kichwa cha familia anatakiwa awe mfano wa kuigwa