Sifa za husband material hizi hapa

Sifa za husband material hizi hapa




1. Anakupigia simu mara kwa mara kukujulia hali: Anakupigia simu asubuhi kukujulia hali kama umeamkaje, mchanaatakupigia simu kujua umeshindaje na kama umeshakula chakula cha mchana, midamida ya kati kati ataku check kwa SMS kujua kama uko sawa na usiku atakupigiasimu na kupeana stori mbili tatu kisha atakutakia usimu mwema….

2. Hataki mkutane kimwili kabla ya ndoa nahuenda akawa hajawahi kuwa na uhusiano na mwanamke tangu azaliwe:Mwanaume mwenye sifa hii mara nyingi hutawaliwana aibu, swala la kukutana kimwili halipo katika mawazo yake hata kama muwewawili tu mmejifungia chumbani wala hanamihemko ya ngono, kwake yeye ni kupiga soga na kisha anaondoka zake kurudikwake. Ndoto yake ni kusubiri hadi mfunge ndoa.

3.
Ana mazoea ya kukununulia zawadi au kukupa fedha za matumizi mara kwa mara: Hivi ndivyo wasichana wengi wanavyopendawatendewe na wapenzi wao, kununuliwa zawadi, kupewa fedha za matumizi nakununuliwa muda wa maongezi kwenye simu, yaani kila akikutana na mpenzi wakeanamwaga pesa, yaani ni pesa pesa pesa hata huwazi kuhusu chochote maana mwanaume yupo kuhakikisha unapata kilakitu. Huyu ndiye husband material haswa

4
Hanywi pombe wala havuti sigara:Mwanaume wa aina hii huwavutia wasichana wengi, yaani hajui ladha ya pombe walasigara. Jamani tuacheni utani mwanaume anayekunywa pombe na kuvuta sigara hanamvuto maana hata kiss unajishauri kwa jinsi harufu ya kinywa isivyo rafiki wakupigana kiss, unaweza hata kutapika.

5.
Siyo mtu wa kwenda Klabu wala kujirusha kwenye matamasha ya usiku (Party): Mwanaume hatulii kila siku analala usikuwa manane kwa sababu ya kupenda kujirusha, inawezekana hanywi pombe wala havutisigara, lakini kwa kujirusha ndiyo hobby yake, huyu hafai. Ukimpata mwanaumeambaye kila akitoka kazini ni nyumbani na hata kama ni kutoka anakuwa anakwendakutembelea marafiki zake waliooa au ndugu zake na kurudi nyumbani mapema, yaanikampani yake ni watu wazima wenye kuwajibika sawa sawa kwa familia. Huyu nimwanaume wa kufaa kuolewa naye

6.
Awe anakumbuka Birthday yako: Yaani mtu wa kwanza kukuamsha alfajiri na kukuambia Happy Birthday anakuwa niyeye na baadaye anakushangaza na zawadi na sherehe ndogo inayowajumuishamarafiki zako. Yaani hasahau siku yako ya kuzaliwa, na kila mwaka anabadilishanamna ya kukushangaza tarehe ya siku yako ya kuzaliwa ikifika. Jambo hilihuwapa raha sana wasichana wa siku hizi….

7.
Ni mtu mwenye hofu ya Mungu:kama ni Mkristo yaani yeye na kanisa kanisa na yeye na anashiriki kwenye kamatimbalimbali za kanisa na anakuwa na majukumu makubwa katika kanisa na kama niMuislamu hivyo hivyo, anakuwa mtu wa hamsa swallati na mshiriki mkubwa katikashughuli za msikitini kwa kujitolea

8.
Unaweza kukisia wakati wowote kwamba yuko wapi na anafanya nini na ukawa hujakosea: Anaweza akawanyumbani, kazini, kanisani akihudhuria masomo ya biblia au msikitini akijisomeaQuran au yuko kwa rafiki yake au ndugu yake waliyeshibana na ukawa hujakosea.

9.
Anapenda sana kusoma:Mwanaume mwenye kupenda kujisomea vitabu mbalimbali vya maarifa na kufuatiliahabari mbalimbali kuhusu kinachoendelea duniani kuanzia mtandaoni hadi kwenye TV, yaaniukifika kwake unakutana na Big flat screen na bookshelf kubwa limeshehenivitabu vya maarifa ya kila aina. Mwanaume wa aina hii atakuwa na uelewa mpanasana na utambuzi wa hali ya juu, huyu atakuwa ni mtu wa kuyachukulia mambo kwaumakini wa hali ya juu na hadhari kubwa, ni mtu wa kufanya maamuzi bila kukurupuka,huyu naye ni husband material

10.Mpole na mnyenyekevu: Yaani unakutana na mwanaume mpole namnyenyekevu hadi raha, akiongea anakuwa kama vile hataki, lakini kuna wakatianakuwa na masihara na utani unaokufanya ujisikie furaha kuwa naye wakati wote.Masihara na utani wake unakuwa umebeba ujumbe wenye hekima na busara kiasikwamba kila unapokuwa naye unajikuta umejifunza kitu kipya.

11.Mpenda watoto: Hii sifa ilitakiwa iwe ni namba moja sema tu nimeghafilika, kwakweli mwanaume hawezi kuwa na sifa za kuitwa husbanda material kama amekosa hiisifa ya kupenda watoto na familia yake. Mwanaume husband materiala anatakiwaawe anajua kubadilisha mtoto nepi, kumlisha mtoto, kubembeleza mtoto akiliausiku wakati mama akiwa amelala kwa uchovu na pia awe anajua kuchagua zawadimbalimbali wanazopenda watoto, au awe na ratiba ya kuwatoa watoto kwenye mitokoyenye kuwavutia watoto kutokana na uwepowa michezo mbalimbali inayowafurahisha watoto.

12. Mwanaume anayeweza kumuua nyoka akafa: hapa simaanishi nyoka wa mdimu,namaanisha mwanaume asiyeweka visasi, mkitofautiana mnazungumza na kuyamaliza na kusahau. Huyu ni mwanaume mwenye sifa za kuitwa husband material.

Kama ikitokea mwanaume ana sifa zote hizo nilizozitaja hapo juu au angalau nusuyake basi huyo anastahili kuitwa husband material.

Hebu wanaume mjipime wenyewe kama mnazo sifa hizo.
Amini usiamini, nilichofeli ni namba 6 tu. kwenye namba 2 mke wangu nilimkuta bikra na ndio mama watoto wangu.
 
Muungwana umenigusa kiukweli,... Kuna mtu mmoja alikuwa na karibia sifa zoote ulizotaja hapo...! lakini sasa alipooa ikatokea ndani ya ndoa akawa amepatwa na tatizo la kiuchumi. Basi mkewake alimburuza kama kuku na kumuacha akamuacha.

Ivi nnavyoongea mke kafa kwa ukimwi mume yupo na afya njema tuu.., japokuwa bado hali yake kiuchumi haijawa nzuri kiviile,..jinsi alivyokuwa anampenda mkewe na familia yake hata kuoa tena hataki yuko barchelor tu.

Hizo sifa bila kuwa na hali kidogo nzuri ya kiuchumi kwa wanawake wa sasa Is nothing.
 
wanaume dizaini hiyo hawapati wachumba these days

wanawake wanataka sex kwanza ili ajue yaliyomo yamo au la

wengi wanakunywa pombe....na wengine wanavuta hadi bangi these days

wanawake wengi nyumba ya ibada ni siku ya kuolewa au kufa kuna msiba
Kumbe ndo maana mie sipati mchumba manake sifa alizotaja Zinduna zooooooote ninazo hadi nakera yaani!
 
Last edited by a moderator:
Hizi sifa za husband material kwa mwanamke mwente sifa zipi? Kwa wanawake wote au kwa wanawake wanaoendana sifa hizi?
 
Kuna baadhi ya points zina overlap ..sasa point namba 7awe na majukum kibao kanisan ..alafu bado awe msoma vitabu mbaaaaya alafu anafatilia mavitu yanayoendelea dunian.. alafu awe anafanya kaz za kumwingizia kipato.......apo apo akumbuke kukupigia simu mara kwa mara ....alafu awe mpoleeeee alafu asipende sex ...jamaaan huyu mtu labda robot ............si atakufa mapema...... ..nakubaliana na ww suala na kutokuvuta sigara na kutokunywa pombe na kwenda club kwel sio mazur...
 
kuna jamaa alijaribu ku pretend kuwa na sifa hizo ili ampate binti.. kumbe ni boooonge la mchepukaji, dah miezi mi3 ilikwa mingi aliumbuka. wanaume bana..!

hahaaaa....kweli kabisa
 
Sifa nyingi ulizoandika, ni za kufikirika na yawezekana ni sifa ambazo umeziandika kutokana na vile uonavyo wewe. Na kumbuka kuna wanawake wengine wengi tu hawapendi sifa nyingi tu kati ya hizo ulizotaja. Ninachokijua mimi, KILA MWANAMKE AU MWANAUME NI HUSBAND AU WIFE MATERIAL, ILA INATEGEMEA NA MATERIAL GANI UNATAKA.


Sent from my iPad using JamiiForums app
 
mimi nina sifa no 2 3 na 4 cc Honey Faith MAHAndow hizo zingine ni za kibwege mwanaume akiwa zoba namna hiyo hua munamuoneaga nyie mademu
 
Last edited by a moderator:
Namba mbili toa, zingine ninazo zote muulize Winifrida wangu anajua.
 
hhhh hizo no 2, 4, na 5, zitanifanya nisiwe kwenye list ya husband material, du aya asante.
 
wanaume dizaini hiyo hawapati wachumba these days

wanawake wanataka sex kwanza ili ajue yaliyomo yamo au la

wengi wanakunywa pombe....na wengine wanavuta hadi bangi these days

wanawake wengi nyumba ya ibada ni siku ya kuolewa au kufa kuna msiba
Duuh aisee!!jamaa nadhani ameandika bila kuangalia ulimwengu wa sasa tulionao wa ndoa zinafungwa kimazoea na uchumba wa miaka 6 mnagegedana huku mnachunguzana
 
Back
Top Bottom