Sifa ya wilaya ya Mpanda

Lady G

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
515
130
hello wanajamii wa tzee.
Naomba mnisaidie walau kujua wilaya ya mpanda na sifa zake. Nimepata kazi huko thoo sijaripot bado.

Thanx
 
Maisha ni popote, nenda karipoti mengine utayaona mwenyewe. Mambo ya kuambiwa unaweza acha kwenda bure na maisha yenyewe magumu haya.
 
Chakula cha kumwaga usiwe na shaka, nenda kaone mwenyewe kisha amua uendelee au la
 
Tukuambie ili iweje sasa?...unataka usiende....watu mnapenda miji mizuri_sijui mnafikiri hiyo mingine nani atakaye iendeleza....wewe nenda bana,...acha habari za kutenga sehemu,..cha muhimu ni kuangalia kazi yako inakulipa ama la.
 
Kwanza umekosea jukwaa mkuu..mahusiano na wilaya ya mpanda wapi na wapi..nwy..kama ni ajira wewe nenda kapige mzigo..usingoje ya kuambiwa..kwa mwenzio inaweza kuonekana ni tatizo kwako ikawa ni neema..kiujumla wilaya nyingi za Tanzania zinafanana..
 
Siunajua kule kwa mzee Pinda so tegemea mazuri mana kunazidi kuboreshwa
 
Pazuri sana niliwai kufika miaka ya 1999; ila sijui sasa hivi pakoje ila kwa mtu anayeanza maisha panafaa sana ukifika huko husisahau kutafuta shamba lako ukome kuja kupote muda hapa nenda shamba kalime
 
Pazuri sana niliwai kufika miaka ya 1999; ila sijui sasa hivi pakoje ila kwa mtu anayeanza maisha panafaa sana ukifika huko husisahau kutafuta shamba lako ukome kuja kupote muda hapa nenda shamba kalime
duh!..................
 
Mbona mpanda kwa kawaida tu. Kuzuri. Ghalama za maisha at least zipo chini. Na hata miundo mbinu ni ya kawaida
 
nI pazuri sana na utapapenda. Mimi nilifika hapo kwa mara ya mwisho mwaka 1978. wenyeji ni wakrimu na halafu ni wakulima wengi sana na sokoni chakula bei nzuri sana . Ni mahala pazuri sana kuanzia maisha. Ila kitu cha mwisho ni uwe muadilifu na mtu usiye majivuno ya intelectual arogance. Yaani ukiongea sentence lazima utie kiingereza ili kuonekana wa maana!
 
Kama una malengo ni sehemu nzuri kwa investments, ardhi ipo ya rutuba, imepakana na mbuga ya katavi national park, reli ipo, kuna migodi ya dhahabu na shaba kwa ssa, wanalima pia tumbaku.
Hali ya hewa huwa ni ya joto kama dar kwa kipindi kirefu.
Wageni wengi huwa wanaingia na kutoka huko kutokana na vitu nilivyotaja hapo juu.
Ukifika usisahau kutafuta ardhi ujenge, kwani ni wilaya inayoibukia kiuchumi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom