Sifa ya mwanamke wa kuowa


mahirtwahir

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Messages
511
Likes
83
Points
45
Age
34
mahirtwahir

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2013
511 83 45
Salaamu zangu natuma, zifike kila mahali,
Tunaziomba rehema, za Mungu zituwasili, -
Hapo siku ya Qiyaama, tuwe chini ya kivuli,
Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.
-
Oa mke Muumini, funga ndoa tawakali,
Mke aloshika dini, na kila siku kuswali,
Hijaab iwe kichwani, afunike yote mwili,
Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.

Usitafute uzuri, au yule mwenye mali,
Chagua tabia nzuri, alotulia akili,
Aloleleka vizuri, kidini na kiasili,
Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.
-
Fadhila zake ni nyingi, uliza kila pahali,
Huo ndio ni msingi, wa maisha ya halali,
Ni kinga kwa mambo mengi, kwa madhambi mbalimbali,
Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.
-
Kuoa ni utulivu, tumeshaona dalili,
Huyaondoa maovu, na mambo huwa sahali,
Hukufanya mtulivu, shida ikikukabili,
Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.
-
Wajibu wako timiza, nyumbani mpo wawili,
Mkikaa kuzungumza, na mambo kuyajadili,
Mjaribu kueleza, muelezane ukweli,
Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.
-
Mume ni msimamizi, kwa mali na kila hali,
Ayaonyeshe mapenzi, maneno kama asali,
Katika masimulizi, asiseme kwa ukali,
Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.
-
Mungu awape watoto, hao ni rasilmali,
Mke ni mama watoto, awe mwema na mkali,
Awatazame watoto, wasikuwe kijahili,
Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.
-
Mke ni nguzo nyumbani, kama vile matofali,
Na mume ndio rubani, huona yaliyo mbali,
Kamba ya Mungu shikeni, ibada iwe awali,
Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.
-
Mungu Watunze vigoli, pamoja na wanawali,
Wawe kama wa awali, kama zama za Rasuli,
Nimemaliza kauli, hapa nafunga kufuli,
Funga ndoa tawakali, oa mke Muumini.
 
K

Kijivi/mdumange

Member
Joined
Jun 9, 2013
Messages
7
Likes
0
Points
3
K

Kijivi/mdumange

Member
Joined Jun 9, 2013
7 0 3
Aaaaaa! Toa point acha kuimba shairi. Kuna kurasa za mashairi bhana.
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
32,933
Likes
15,568
Points
280
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
32,933 15,568 280
Huu uzi utakuja kutiwa lock tu mbeleni.
 
Mwali

Mwali

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Messages
7,024
Likes
36
Points
0
Mwali

Mwali

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2011
7,024 36 0
Hii ipelekwe jukwaa la lugha maana thamani yake kubwa ni kule ku-rhyme tu!
 
stevoh

stevoh

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2011
Messages
2,924
Likes
9
Points
135
stevoh

stevoh

JF-Expert Member
Joined Dec 5, 2011
2,924 9 135
Kuna ujumbe lakini tatizo njia ya kufikisha ujumbe
 

Forum statistics

Threads 1,275,230
Members 490,947
Posts 30,536,270