Sifa ipi wataiangalia hawa watu

Sifa ipi wataiangalia hawa watu

nyamva

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
249
Reaction score
163
Walimu zaidi ya elfu hamsini (50,000) Tanzania nzima wanatarajiwa kupanda madaraja mawili mfululizo yanayotambulika kama madaraja ya mserereko.

Hatua hii inakuja baada ya mwaka 2016/2017 Watumishi wa umma kupandishwa madaraja lakini kukatokea zoezi la uhakiki hivyo waliokua wamepewa barua hizo kusitishiwa upandaji wa madaraja kwa Waalimu.

Katibu Mkuu wa CWT Deus Seif akiwa mkoani Iringa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuwapandisha madaraja mawili Walimu hao waliyoyaita madaraja ya mserereko. #MillardAyoUPDATES
 
Hawa walimu ni intake ipi? Hiv intake ya 2015 haina mserereko kweli?
 
Back
Top Bottom