Sifa hizi zikufanye ukajitegemee

Hayo mahitaji kayatoe ukiwa unaishi pahala pengine. Ukiishi na wazazi mkeo na watoto wako hawana uhuru wala furaha
Waarabu na wahindi wanaishi hivyo na wanafanikiwa .

Shida kubwa ya waswahili Akili ndogo kwahiyo kila jambo unalitazama Kama tatizo au Mzigo.

Unaweza ukakaa na Mama na Baba Mke wako na watoto na mkaishi Vizuri Sana na wahindi wanaishi hivi na ukiangalia familia zao zimestawi Sana .

Kukaa kwenu sio tatizo Ila muhimu in life make sure unakuwa Provider tu haijalishi unakaa wapi.
 
Iwe wazazi ni wazee kabisa na hawajiwezi ila jitahidi uwe na mjengo wako mbali na hapo kwa wazee utailetea familia yako heshima
 
Miaka 25 mbona umeanzia mbali Sana mkuu?
Mwanaume akishafikisha umri wa miaka 20 Tu huyo tayari kashakuwa mtu mzima na anapaswa kujitegemea
 
Mzazi akishakuzaa hiyo ni fursa mengine kajipambanie mbele kwa mbele
Ndio maana wabongo wanazaa watoto ambao hawawezi kuwalea. Sio sawa watu wazima kurundikana kwenye nyumba ya mzazi lakini hiyo ni dalili kuwa kuna sehemu wazazi walilegea kimalezi. Kingine si kila kuzaliwa ni fursa ila laana za mahangaiko tu
 
Hizo ndizo fikra za kiafrika tena za kimasikini. Mbona wahindi, waarabu, wazungu na wachina hawafanyi hivyo? Hebu iangalie familia tajiri ya Bakhresa wanavyoishi pamoja. Na wanashiriki pamoja kuuendeleza na kurithishana utajiri wa familia
 
Doh! Kweli dunia kubwa hii.. njoo Unguja hapa kuna dogo haeleweki hela anapata hatujui anapeleka wapi na kujitegemea hataki
 
😅 Kwahiyo kilicho kukimbiza kwenu..ulihc mshua wako angemshika kalio wife? Kama anahizo tabia atakuja kumshikia huko huko kwako mzee
Nimeongea lugha ya picha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…