Kama nitakuwa nimesema uwongo ninaomba radhi kabla. Kinachojengwa sasa hivi Ubungo ni tofauti na kile cha awali. Mwanzoni ilikuwa ni interchange halafu na barabara ilikuwa itoke Ubungo hadi Kibaha. Financing ilikuwa ni partly ya WB na partly fedha za ndani.
Kutokana na sera za Jiwe kukataa kuwafidia waliobomolewa nyumba zao ikiwa ni pamoja na kudharau mazuio ya Mahakama juu ya kuwabomolea wamiliki wa nyumba hizo, WB walijitoa kufadhili kwa kuwa taratibu zinawakataza. Taratibu za WB zinakataza kujuhusisha na mradi wowote unao kandamiza haki za binadamu.
Baada ya hapo Serikali ikaamua kuwa kwa vile "unga hautoshi basi tukoroge uji badala ya kupika ugali" kwa kuwa ingredients ni hizo hizo na sufuria liko jikoni. Ndiyo maana mradi wa barabara unaishia Kibamba, na interchange imekuwa daraja juu ya daraja.
Kama nimekosea naomba radhi