Sielewi kabisa, naomba kuwauliza wanawake swali

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,265
21,441
Katika ulimwengu wa leo, kuna kitu ambacho nimeshindwa kabisa kuelewa kinafanywaje, japo kukiri huku kunaweza sababisha wanaume wengi wasinielewe. Mie sijui kabisa kutongoza mwanamke tuliyekutana punde tu au hata yule tunaefahamiana kwa muda kwa ajili tu ya kufanya nae ngono na kila mtu aishie zake baada ya hapo - au labda ije itokee tena siku nyingine. Inaweza kunitokea kutokana na mazingira fulani tukiwa pamoja, lakini haitakuwa kwa namna ya kumbembeleza na kumwaga sera ili akubali tufanye ngono!

Sasa kwenu wanawake, hebu niambieni, hivi katika dunia ya leo bado kuna mwanaume kumtongoza mwanamke kwa ajili tu ya kufanya ngono na mwanamke akakubali?

Naelewa kwamba mahusiano ya kimapenzi yanaanza taratibu, urafiki wa kawaida ambao utakua hadi inafikia mwanaume (au hata mwanamke) kuweka wazi hisia zake na uhusiano wa mapenzi kuanza. Yaani ngono inakuwa matokeo ya uhusiano uliokuwapo au hisia zilizokuwapo tayari, sio agenda ya kuanzia uhusiano. Lakini hivi bado kweli mwanaume leo hii anaweza akakufuata na kuanza kukutongoza kwa ajili ya siku hiyo au kesho yake au hata wiki ijayo mkutane ili tu mfanye ngono tu, na wewe ukakubali? Hivi huwa hao wanaume wanawaambia nini hadi mnakubali?

Kumbuka hapa siongelei wale wanaume wanaokuambia ukiwakubalia watakupa gari, au kazi nk. Hao sio watongozaji, ni wanunuzi wa ngono, na kama unawakubalia wewe ni changudoa tu, utake usitake.
 
swali refu sana nimepotea njiani

Ngoja nikufupishie;

Hivi katika dunia ya leo bado kuna mwanaume kumtongoza mwanamke kwa ajili tu ya kufanya ngono na mwanamke akakubali? Hivi huwa hao wanaume wanawaambia nini hadi mnakubali?
 
Ngoja nikufupishie;

Hivi katika dunia ya leo bado kuna mwanaume kumtongoza mwanamke kwa ajili tu ya kufanya ngono na mwanamke akakubali? Hivi huwa hao wanaume wanawaambia nini hadi mnakubali?

ndio ipo kwani dada poa si wanakuwa na mwanaume kwa sababu ya ngono tu
wanachoambiwa sina nacho uhakika, labda nikafanye utafiti....lol
 
73501.jpg
 
Ya hivyo yana maslahi haiwagi kazi ya kanisa.

Makubaliano mezani game inapigwa kawaida tu.
 
Ya hivyo yana maslahi haiwagi kazi ya kanisa.

Makubaliano mezani game inapigwa kawaida tu.

Umetoa definition ya changudoa hapa. Hao sio tatizo, nawaelewa. Tatizo ni hili kundi jingine ambalo ni jepesi kuitikia bila malipo wala uhusiano wowote uliositawishwa, au hisia zilizojengwa pande zote mbili kwa muda fulani. Tulikutana jana, tukavua jana, tukaagana jana.
 
Back
Top Bottom