SIDO ifumuliwe awamu hii ya Viwanda

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,553
32,177
Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) lifumuliwe ili liweze kuundwa upyaikiwezekana lipate Boss msomi wa ngazi ya juuu kabisa, maana ni kama halipo halisiskiki kwa vitu vya maana zaidi ya kuoka mikate ya kumimina na batiki. Na wafanyakazi wanalipwa mishahara. Hakuna ubunifu kabisa.
Jifunzeni Rwanda
 
Naunga mkono. Lazima tuwaze mbali Haiwezekani Ubunifu uwe ni wa viwango vya kutengeneza mashine za tofari, incubators, na vitu vidogo vidogo. Atafutwe mtu mwenye maono ya MegaIndustries through SIDO.
Inawezekana
UKIFIKA ofisi za SIDO mkoa wa DAR-ES_SALAAM utapatwa na butwaa kabla hujaanguka chini puu, maana ni kama jengo la makumbusho KILWA KIVINJE au makaburi ya KAOLE Ila magari mapya kabisa full AC. Iweje wahindi na wachina hata wale waarabu wa SYRIA wanafanikiwa kuajiri vijana wenzetu na kutengeneza fenicha hapa hapa nchini na kuuza bei ya kutupa ila sisi tunawatumia wafungwa na JKT kwani SIDO wanafanya nini? hawa wasanii wakina Stiv Nyenyerer wapelekwe huko SIDO wakajifunze jinsi kupamba, kusuka ukili na mambo dizaini hiyo kwa ajii ya kuongeza kipato kuliko kupiga domo tu.............
 
UKIFIKA ofisi za SIDO mkoa wa DAR-ES_SALAAM utapatwa na butwaa kabla hujaanguka chini puu, maana ni kama jengo la makumbusho KILWA KIVINJE au makaburi ya KAOLE Ila magari mapya kabisa full AC. Iweje wahindi na wachina hata wale waarabu wa SYRIA wanafanikiwa kuajiri vijana wenzetu na kutengeneza fenicha hapa hapa nchini na kuuza bei ya kutupa ila sisi tunawaukumia wafungwa na JKT kwani SIDO wanafanya nini? hawa wasanii wakina Stiv Nyenyerer wapelekwe huko SIDO wakajifunze jinsi kupamba, kusuka ukili na mambo dizaini hiyo kwa ajii ya kuongeza kipato kuliko kupiga domo tu.............
Pale niliwahi kumkuta jamaa mmoja Multiskilled anajua vitu vingi kuliko yaani kiasi kwamba nikajiuliza kama angekuwa MIT au Silicon Valley angekuwa billionea. Nilimkuta anatest gari aliyoiunda mwenyewe na anadesign chochote unachotaka au ukimpa wazo. Bongo kuna vichwa aisee. Sido, Veta zifanyiwe mapinduzi ili wawe na maono makubwa na wawe kivutio cha wengi wenye Ideas
 
Tusijikite tu katika kuokota faini za NEMC &Trafiki. Nchi hii itaokolewa na viwanda vidogo vidogo (kupitia SIDO).
 
Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) lifumuliwe ili liweze kuundwa upyaikiwezekana lipate Boss msomi wa ngazi ya juuu kabisa, maana ni kama halipo halisiskiki kwa vitu vya maana zaidi ya kuoga mikate ya kumimina. Na wafanyakazi wanalipwa mishahara. Hakuna ubunifu kabisa.
kuna kipindi nilikaa Africa ya kusini yaani jamaa wana kitu wanakiita (PROUDLY SOUTH AFRICAN)..Yaani humu kazi yao kubwa ni kusapoti viwanda na biashara za kisauzi. karibia body nzima imejaa watu walio na elimu tofauti tofauti na watu wanaofikiria mbali zaidi. Tanzania tuna vipaji vingi sana sana na kuna watu wanajua sana ufundi ila ndio vile tena serikali yetu haijaweka msisitizo katika maswala kama haya...wakina Mwaijage maneno mengi lakini hata kutafuta njia tofauti za kuweza kufanikisha watu kuanzisha viwanda au kuwasaidia wenye viwanda vidogo kukua zaidi hata kuanzisha semina ambayo itawasaidia hawa wafanya biashara na wenye viwanda vidogo.
kuna jamaa ni mtanzania alitengeneza mashine ambayo inaweza kuvuta moshi wa angani na kuubadilisha na kutengeneza mbolea gani sijui...yaani sijamsikia tena
hatuna plan, strategy wala idea ya vitu tunavyotaka kufanya..serikali kama serikali ikiamua kufungua branch ndogo ya benki ya serikali yenye kutoa mikopo nafuu i mean NAFUU SANA SANA. na hawa watu wenye viwanda vidogo esp ambao wana operate kwa sasa wataweza kukopa kwa riba nafuu basi Tanzania ya viwanda itawezekana
 
SIDO pekee achilia vyuo vikuu, VETA n.k ingeweza kuleta mapinduzi ya viwanda. Sasa sisi tumekalia siasa na kuwania za kula posho na kutembea VX/V8, full kiyoyozi
 
Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) lifumuliwe ili liweze kuundwa upyaikiwezekana lipate Boss msomi wa ngazi ya juuu kabisa, maana ni kama halipo halisiskiki kwa vitu vya maana zaidi ya kuoga mikate ya kumimina. Na wafanyakazi wanalipwa mishahara. Hakuna ubunifu kabisa.
Naunga mkono hoja! SIDO ina clusters tofauti za wajasiriamali Ila ukiangalia kwa undani mchango wake ni mdogo sana.
Kwanza: SIDO hawana wataalamu waliobobea ktk fani ambazo wanajinasibu kuwa ndio maeneo wanayotoa huduma kwa wajasiriamali wadogo.
Pili: Ushirikiano wa SIDO na taasisi nyingine mfano vyuo vikuu, taasisi za utafiti na viwanda ni mdogo sana.....

Hivyo ni vigumu SIDO kuleta mabadiliko kwa wajasiriamali ikiwa imefunga milango ya ushirikiano na sekta nyingine. Kutoa ushauri tu hakutoshi waende mbele zaidi na kuanzisha viatamizi kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.., na wawe tayari kushirikiana na sekta ambazo zitasaidia kutoa mchango chanya.
 
Nilikopaga pale senti kidogo mkopo wa pili wakaniambia niende akiba bank awataki usumbufu niliondoka kinyonge kweli wakati walinihaidi makiza mkopo tukukopeshe nikalipa fasta kumbe walikuwa wanaitaji pesa yao kwa haraka
 
Ni aibu wafanyakazi wa SIDO kuendelea kulipwa mshahara na kupewa mgao wa Magari ya kifahari (Land Cruiser VX / V8 na NISSAN PATROL.
 
Naunga mkono. Lazima tuwaze mbali Haiwezekani Ubunifu uwe ni wa viwango vya kutengeneza mashine za tofari, incubators, na vitu vidogo vidogo. Atafutwe mtu mwenye maono ya MegaIndustries through SIDO.
Inawezekana
tatizo ukiweza kutengeneza bunduki utaozea jela
 
Back
Top Bottom