shikwashikwa
Senior Member
- Jun 5, 2015
- 188
- 46
Habari zenu,
Poleni na majukumu ya kitaifa, hapana shaka weakend yenu inaendelea vizuri.
Nina mahusiano na binti mmoja yapata mwaka na nusu sasa nikawa nimejiridhisha kuwa anafaa kuwa mke wangu halali (nataka kumuoa) Jana usiku nilikuwa na kikao na familia yangu na kuwaeleza hili,nashukuru hawakuwa na pingamizi.Baada ya kumaliza kikao ilibidi nirudishe viti kwenye baadhi ya vyumba vingine.
Maana kikao kilikuwa na watu wengi kidogo nilifanikiwa kurudisha lakini nilipofika kwenye chumba cha bwana mdogo (baba mmoja mama mmoja) nilivutika na Albamu ya picha iliyokuwa juu ya meza nikaanza kutizama picha moja baada ya nyingine. Hamadi nikaona picha inayofanana na binti ninaetaka kumuoa (mchumba) tofauti ni kuwa ilipigwa kama miaka 3 nyuma lakini sura haijabadilika sana, nikashawishika kuigeuza nyuma nilichoka iliandikwa "my love forever" kazi ya viti ikawa imekomea hapo. Dogo yupo chuo nikampigia simu na kumueleza hili na kumtajia jina la muhusika pamoja na picha kuikuta kwake hakunificha. Ni mpenzi wake siku nyingi na yeye ndio mtu aliekata utepe.
Nikataka kubalansi story nikampigia mchumba mtarajiwa na kumpa ukweli wote,alikubali pia baada ya mabishano makali yaliyoambatana na ushahidi wa picha yake mwenyewe niliyoituma kwa Whatsapp, lakini akaomba msamaha na akajitetea kuwa hakufahamu kama huyo mtu ni mdogo wangu wa damu, kumbukwe mimi na familia yangu tumeishi miji tofauti kwa muda wa miaka mingi shule pia baba yetu hakupenda tutumie majina ya ukoo.
Sasa sijui niendelee na taratibu za kuoa au niitishe kikao tena na niwape sababu za kusitisha mpango wangu. Ushaidi ninao niliwarekodi wakinithibitishia japo kila mmoja alikiri hana mpango na mwenzie. Msaada wa kiushauri ndugu zangu maana sijapata hata lepe la usingizi hii leo kwa kuliwaza hili, maana hata nikioa hawa si wataendelea kubanjuana vipi nikisafiri na siwezi kumpiga stop dogo asije kwangu kinachoniuma dogo ndio kavunja kikombe.
Alafu Jana kwenye simu kabla sijamtamkia kuwa lengo la safari yangu ni kuhusu huyo binti kwenye picha yake alikuwa akijibu kwa njonjo na dharau kuwa nanukuu: "huyo demu bro kwangu hapindui hata iweje si unajua mimi ndio mtengeneza njia.Niko kama naumwa hii leo hapa ushauri wenu labda utanipa auheni.
Asante