Sidhani kama kunaubaya, wakikumbishia je?

Sidhani kama kunaubaya, wakikumbishia je?

Lol huko kujiamin kama vile kumezidi japo yeye ndio kawahi - Mwekee mipaka lol kama kaka lazima uwe na say kwa dogo lako - Wadada wako wengi hapo hamna wakulaumiwa lol - Ni sehem ya maisha - matetere kibao kushare kataa
 
Lol huko kujiamin kama vile kumezidi japo yeye ndio kawahi - Mwekee mipaka lol kama kaka lazima uwe na say kwa dogo lako - Wadada wako wengi hapo hamna wakulaumiwa lol - Ni sehem ya maisha - matetere kibao kushare kataa

Sio siri naumia sana huyu binti anajitambua,mpole,mpambanaji hajui kunung'unika mara nyingi ukimkosea/mkishindwa kuelewana hata hapayuki ataomba myamalize siku nyingine mkiwa hamna jazba...hata kama namuacha lakini nakili itakuwa ngumu kumpata kama huyu tena
 
lol kama swala ni hilo basi na vile wakir usimwache coz hata ukija kupata mwingine utateseka tu bas mwite dogo ongea nae amheshim shemej yake - Mpaka hapo hakuna mwenyekosa any way fanya kile moyo wako wakitaka - Sio njia panda kivile maamuzi tu kikubwa mwanamke tu ajitambue na aheshim mahusiano yenu - wewe mpaka dogo lako akuambie mdada hapindui lol acha uzungu huo
 
KWANZA : ndoa ni kiapo/ahadi kuwa mtakuwa waaminifu kila mtu kwa mwenzie. Kutokana na Integrity degradation kati yetu wanadamu, hakuna guarantee kwamba viapo hivyo vitatunzwa. Hata kama ukikata wewe utepe, itakufaa nini kama atakusaliti mbeleni? Starting a race is not an issue , finnishing is. Halafu wala huhitaji ushauri wetu kwa sababu kama kweli unampenda , u will always find it in your heart to live with that.

PILI : Waswahili wanasema kitu chema kula na nduguyo (Dont take me serious here 🙂 ! ). Trust me when it comes to Issues you hold dear. Nduguyo wa damu yako ndie atakuonea huruma. At least nafsi ikishindwa kumuheshimu mke wa mtu itamuheshimu kaka yake. Jitu baki ambalo halikujui litakamua hadi usahaulike!

Nimekuelewa sana tu mjomba
 
Saa zingine inabidi ufanye hata kile usichopenda fanya.
 
Bila kujari maumivu,hasara..."maamuzi magumu"
Ndio kitu kinazunguka kwenye akili yangu saa hii

Saa zingine inabidi tu uvumilie na ufate kile moyo unapenda, sababu hawakuwahi kutambulishana kwenu au wewe ulikuwa hujui basi huna sababu ya kuacha endeela
 
Habari zenu,

Poleni na majukumu ya kitaifa, hapana shaka weakend yenu inaendelea vizuri.

Nina mahusiano na binti mmoja yapata mwaka na nusu sasa nikawa nimejiridhisha kuwa anafaa kuwa mke wangu halali (nataka kumuoa) Jana usiku nilikuwa na kikao na familia yangu na kuwaeleza hili,nashukuru hawakuwa na pingamizi.Baada ya kumaliza kikao ilibidi nirudishe viti kwenye baadhi ya vyumba vingine.

Maana kikao kilikuwa na watu wengi kidogo nilifanikiwa kurudisha lakini nilipofika kwenye chumba cha bwana mdogo (baba mmoja mama mmoja) nilivutika na Albamu ya picha iliyokuwa juu ya meza nikaanza kutizama picha moja baada ya nyingine. Hamadi nikaona picha inayofanana na binti ninaetaka kumuoa (mchumba) tofauti ni kuwa ilipigwa kama miaka 3 nyuma lakini sura haijabadilika sana, nikashawishika kuigeuza nyuma nilichoka iliandikwa "my love forever" kazi ya viti ikawa imekomea hapo. Dogo yupo chuo nikampigia simu na kumueleza hili na kumtajia jina la muhusika pamoja na picha kuikuta kwake hakunificha. Ni mpenzi wake siku nyingi na yeye ndio mtu aliekata utepe.

Nikataka kubalansi story nikampigia mchumba mtarajiwa na kumpa ukweli wote,alikubali pia baada ya mabishano makali yaliyoambatana na ushahidi wa picha yake mwenyewe niliyoituma kwa Whatsapp, lakini akaomba msamaha na akajitetea kuwa hakufahamu kama huyo mtu ni mdogo wangu wa damu, kumbukwe mimi na familia yangu tumeishi miji tofauti kwa muda wa miaka mingi shule pia baba yetu hakupenda tutumie majina ya ukoo.

Sasa sijui niendelee na taratibu za kuoa au niitishe kikao tena na niwape sababu za kusitisha mpango wangu. Ushaidi ninao niliwarekodi wakinithibitishia japo kila mmoja alikiri hana mpango na mwenzie. Msaada wa kiushauri ndugu zangu maana sijapata hata lepe la usingizi hii leo kwa kuliwaza hili, maana hata nikioa hawa si wataendelea kubanjuana vipi nikisafiri na siwezi kumpiga stop dogo asije kwangu kinachoniuma dogo ndio kavunja kikombe.

Alafu Jana kwenye simu kabla sijamtamkia kuwa lengo la safari yangu ni kuhusu huyo binti kwenye picha yake alikuwa akijibu kwa njonjo na dharau kuwa nanukuu: "huyo demu bro kwangu hapindui hata iweje si unajua mimi ndio mtengeneza njia.Niko kama naumwa hii leo hapa ushauri wenu labda utanipa auheni.

Asante

Automatic huyo hawezi kuwa tena mke wako amekosa sifa hawa viumbe wako wengi sana piga chini huyo topic closed
 
Pole mkuu,afadhari wewe mimi muhusika nilikuwa nameza panaldo tu kila baada ya dk 20

Asante mkuu ila daah sijui bwana ila fanya maamuzi sahihi kwa mda huu mbeleni usipokuw na aman ya ndoa na familia kwa ujumla ni zaid ya maumivu pia kukosa iman na ndugu yako. MKE ANAUMA BWANA SIO MCHEZO usilee maumivu mzee chukua hatua .
 
dah polee!! waite wt wawil uongee nao uwaulize km wataheshimiana km inlaws..thn apo ukiwa unawauliza waangalie machoni..koz olwayz eyez talk...koz dem anaweza sema ntamuheshm km shemej hk macho yana shy inabid ujiongezee sasa...mana maj yakizd unga itabid usonge ugali
 
Ahsanteni wakuu...kwa ushauri wenu hakika nimepata faraja sana sana saaana! Naomba niwaAhidi nitarudi na mrejesho.
 
Mkuu Shikwashikwa hapo umeshikwa pabaya.
 
Sio siri naumia sana huyu binti anajitambua,mpole,mpambanaji hajui kunung'unika mara nyingi ukimkosea/mkishindwa kuelewana hata hapayuki ataomba myamalize siku nyingine mkiwa hamna jazba...hata kama namuacha lakini nakili itakuwa ngumu kumpata kama huyu tena

kwa comment hii upo kwenye wakati mgumu

ukifikia maamuzi ya kumwacha utawaelezaje wazazi ambao tayari ulishawaeleza kuhusu mchumba na wakakubaliana nawe
 
Back
Top Bottom