Sidhani kama bado naipenda nchi yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sidhani kama bado naipenda nchi yangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by zezeta, Dec 31, 2011.

 1. z

  zezeta Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAKUMBUKA nilipokua shule ya msingi na sekondari nili imba sana tena kwa shangwe na hamsa kubwa . nili imba TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE, NA NILALAPO NAKUWAZA WEWE PIA NIAMKKAPO NI HERI MAMA WEE......................... LAKINI kwa hali hii iliyonikuta sidhani kama kweli nitakuimbia wimbo huu eeeeweeh TANZANIA kwa moyo wangu. Ntakua mnafiki na mzandiki kuimba nakupenda wakati moyo wangu umejawa na simanzi kubwa, maswali mengi yasiyo na majibu. umebeba visasi na risasi umebeba ujumbe wa dhiki na shida. sina furaha tena na wewe TANZANIA. NAINGIA MWAKA 2012 NIKIWA NA FUNDO KUBWA MOYONI NIKIKUMBUKA YALIYO NIKUTA TAREHE ZA ISHIRINI. SIJUI KAMA NTASAHAU TUKIO LA MAJI KUINGIA NDANI MPAKA KUBOMOA UKUTA WANGU. SITA SAHAU JINSI NLIVYO JITAHIDI KUOKOA MAISHA YANGU NA MAISHA YA JAMAA ZANGU, SITASAHAU KUMPOTEZA MTOTO WANGU NA KUJIKUTA MIMI NA MAMA WA MTOTO TUKIWA TUMESHIKILIA MTI AMBAO UMEBAKI KIDOGO TU KUFUNIKWA NA MAJI. SITASAHAU NYOKA NA KENGE TULIOKUA NAO KARIBU WAKIJITAHIDI NA WAO KUOKOA MAISHA YAO. SITA SAHUA SAUTI YA SPIKA ZA POLISI INYOTAMKA TULIENI NA MUWE WAVUMILIVU TUNAJITAHIDI KUTAFUTA LIFE JACKETS ZA KUWAKOA.SITA SAHAU KUONA VIONGOZI WETU WAKITABASAMU NA KULA KRISMASS KWA BASHASHA WAKATI TULIOWACHAGUA TUKI TAABIKA KWA DHIKI ISIYO MFANO.. SITA SAHAU NAINGIA MWAKA WA 2011 NIKIWA NA KAPTULA 1 NA TISHET NA YEBOYEBO CHINI, HUKU MKE WANGU AKISHINDIA DERA MOJA. SITASAHAU.... HAKIKA..... SITASAHAU UPWEKE NILIONAO NA KUKOSA TUMAINI...SIDHANI KAMA BADO NAIPENDA NCHI YANGU
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Zezeta, pole mkuu kwa kuathirika na mafuriko, pole kwa kufiwa na mwanao. Mungu akupe moyo madhubuti kuukabili msongo wa fikra. mungu aipe pumziko la amani roho ya mwanetu, amen
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu pole kwa maswaibu, nakushauri uwe strong ili uweze kuishinda misukosuko ambayo hata nchi yetu Tanzania inapitia kwa sababu ya Serikali legelege isiyojali vipaumbele vya nchi wala wananchi wake.. Heb badilisha na jina labda hii itakusaidia pia..!
   
 4. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wimbo TANZANIA hauna shida,tatizo niletu wenyewe kwa kukosea na kumuweka msanii madarakani.pole sana ndg kwa yote yaliyokukuta
   
 5. M

  Maengo JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana mkuu! Tuko pamoja!
   
 6. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,078
  Trophy Points: 280
  Pole sana kaka, kama vp pigania uraia wa nchi mbili then ule kona
   
 7. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  SITA SAHAU NAINGIA MWAKA WA 2011 NIKIWA NA KAPTULA 1 NA TISHET NA YEBOYEBO CHINI, HUKU MKE WANGU AKISHINDIA DERA MOJA.


  pole sana hata mwaka umesahau!
   
 8. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Pole xana bro kwa yote yaliyokusibu na mola akupe ujasiri wa kuyakabili yote!
   
 9. z

  zezeta Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AHSANTENI SANA WAKUU WOTE MLIONIPA POLE.... hilo nafahamu ni dogo kuna wengine wamepata mkubwa kuliko yangu ila IPO SIKU viziwi watakaposikia na mabubu watakapo ongea ndipo kitakapo eleweka.......
   
Loading...