Mkapa hata siasa za urais hatakiwi kujihusisha. Tunakosea sana tunapowaacha marais wastaafu kufanya siasa za vyama. Kimsingi, hata kama ili mtu awe sharti atokee chama fulani, lakini sanctity ya urais inabeba dhamana zaidi ya chama. Kwa hiyo, ni bora anapostaafu asijihusishe na masuala ya vyama ili kulinda heshima ya urais.
CCM wanapingana na dhana hii, lakini wakumbuke kuwa kuna wakati rais mstaafu wa chama chao anaweza kujihusisha na siasa za kupingana na rais aliye ikulu, kama Kambarage alivyoonekana kufanya akazua tafrani. Utamu wa kumtumia Mkapa unalingana na uchungu wa Mkapa kuamua kupingana na chama chake. Ili kuokoa heshima ya wote, chama na Mkapa mwenyewe ni bora akae pembeni.