nchi hii ngumu sana kila eneo lina vikwazo kibao pia kwa wahasibu ndo kabisa kuipata hiyo CPA (T) ujue si chini ya miaka 7 hata wanaosomea udaktari ni cha mtoto.wenzetu ulaya na marekani vitu kama hiyo ni rahisi sana kuvipata na wanafunzi wakifeli huyo mwalimu anajisikia vibaya sana kwani kufeli kwake ni sawa na kufeli kwa huyo mwalimu.Mada yako kuihusianisha na siasa nakubaliana nawe, namfahamu mwalimu mmoja hapo Law School aliwahi kupewa shavu na JPM enzi zile, akawa wakili wa serikali, hivyo tabia za kisiasa kuwepo kwenye utendaji wa hicho chuo sishangai.
Hii elimu ya Law School huwa naona kama imelazimishwa kuwa ngumu kwa manufaa ya wachache, siku hizi imegeuzwa kufaulu mitihani yao kuwa kama kushinda bahati nasibu.
Huo mfano uliotoa wa idadi ya wanafunzi wanaofaulu huku wengi wa wanaofeli wakiwa wametoka vyuo vile vile vinavyofundishwa na walimu walewale, ni jambo la kushangaza zaidi, nieleweke; sio kwamba nalazimisha wafaulishe wengi ili kuturidhisha, lakini kwa trend ilivyo ya ufaulu kila mwaka hairidhishi.
Wale jamaa zangu ni kama wamejigeuza "miungu watu" wanajua wao ndio wameshika funguo zenu kuwa mawakili, hivyo lazima wafanye namna ya kuwapunguza kwa kila njia ilimradi siku ya mwisho viwango vya wafaulu viwe chini.
Lakini hawajui kwa kufanya kwao hivyo, wanaitia jamii mashaka juu ya uwezo wao wa kiufundishaji, kwanini wanafunzi wengi wanafeli kila mwaka zaidi ya wanaofaulu? sasa "Law School" imegeuka kuwa "School of Failures"?!
Huwa nahisi kama wana mpango maalumu wa kuhakikisha wana "regulate" idadi ya mawakili Tanzania, kwamba isiwe kubwa na kupunguza soko lao, hasa ukizingatia "unyeti" wa fani yao [wakili msomi].
Huo mfano wa kuingia kwenye chumba cha mtihani na kitabu OG uliotoa, huku wenye photocopy wakibanwa, nao ni kielelezo cha ujanja ujanja wanaofanya hao walimu, lakini niwape angalizo tu...
Hata hao wanaoingia kwenye chumba cha mtihani na kitabu OG, bado wasijiamini, wajiandae kwa lolote, hapo kinachoangaliwa na muuza kitabu ni biashara yake pekee, ufaulu wako haumuhusu, matokeo ya hilo somo yakitoka mtu akafeli licha ya kuwa na kitabu kwenye chumba cha mtihani msishangae, maisha yenu sio mepesi hivyo.