Siasa zaiondoa BP Tanzania

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,317
Wana jamii.

Nimesoma katika economic forum na kuona BP imeamua kuuza hisa zake zote ilizokuwa inamiliki katika BP Tanzania kwa mwekezaji mwingine na hivyo kujitoa rasmi katika umiliki wa kampuni hiyo ndani ya Tanzania.

Na sababu walizobainisha ni kwa kuwa biashara ya mafuta inaendeshwa kisiasa zaidi na mamlaka za Tanzania na kwa kuwa wao hawakuwa tayari kugombana na mamlaka hizo ndani ya TZ wameamua kujitoa rasmi kwa kuuza hisa zao zote 50% kwa kampuni nyingine.

My Take: Je ni wapi waTZ watapata mafuta kwa ajili ya magari yao yasiyochakachuliwa? na vipi mafuta ya ndege itakuwaje?

Nawapa Pole wa Tz na kuwapongeza BP kwa kujali ubora wa bidhaa zenu.
 
mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
554
Mafuta yasiyochakachuliwa na usimamizi mbovu tu wa serikali ya ccm, unajua kule depot hakuna mafuta yanachakachuliwa,deal hizo zinapigwa mitaani/vituoni so wakisimamia yatapatikana tu. Lkn pia kujitoa kwao ni pigo kwa ajira za wabongo waliokuwemo nk
 
CR wa PROB

Senior Member
Sep 21, 2011
170
29
hiyo ndiyo bongo land, waja leo waondoka leo!!!! sasa 2ombe na wale wa makapuni ya MADINI nayo yachakachuliwe ili yaondoke!!!
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,942
Wana jamii.

Nimesoma katika economic forum na kuona BP imeamua kuuza hisa zake zote ilizokuwa inamiliki katika BP Tanzania kwa mwekezaji mwingine na hivyo kujitoa rasmi katika umiliki wa kampuni hiyo ndani ya Tanzania.

Na sababu walizobainisha ni kwa kuwa biashara ya mafuta inaendeshwa kisiasa zaidi na mamlaka za Tanzania na kwa kuwa wao hawakuwa tayari kugombana na mamlaka hizo ndani ya TZ wameamua kujitoa rasmi kwa kuuza hisa zao zote 50% kwa kampuni nyingine.

My Take: Je ni wapi waTZ watapata mafuta kwa ajili ya magari yao yasiyochakachuliwa? na vipi mafuta ya ndege itakuwaje?

Nawapa Pole wa Tz na kuwapongeza BP kwa kujali ubora wa bidhaa zenu.

Kuna taarifa kwamba ccm wameingia mkataba na kampuni ya camel oil, huenda ndiyo itapewa jukumu la kuhakikisha mafuta yanapatikana kwa wingi wa kutosha!!

Vile vile tumeambiwa TPDC wameshafungua tender kwa ajili ya kupata kampuni itakayofanya biashara ya mafuta na COPEC kwahiyo hilo gap la BP linaweza kuzibwa na COPEC!!

Suala la kuchakachua mafuta halihusu depots, uchakachuaji unafanyika mahali pengine kabisa na vijiwe vya kuchakachua vinafahamika.

We pita tu barabara ya morogoro kati ya kibaha na chalinze uone utitiri wa vituo vya mafuta na maukuta marefu yaliyojengwa nyuma ya vituo ama kuzunguka vituo, uone misururu ya malori ya mafuta, then ujiulize ni biashara gani inafanyika humo?

Kwa hatua hii ya BP kuna uwezekano wa nchi kukumbwa na matatizo ya upatikanaji na ubora wa mafuta.
 
twahil

JF-Expert Member
May 31, 2011
4,100
2,791
Bora BP waondoke.Kwakweli wametutesa sana kipindi kile walipogoma kuuza mafuta.Mimi kama mzalendo siumii kuondoka kwao wanaf.ki tu.Kwa wale waliokuwa wakifanyakazi BP waende vijijin kusupport kilimo kwanza.
 
Cynic

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
5,146
1,642
Biashara ni kuchagua. BP wameamua baada ya kuona ubabe unazidi hekima. Dunia kubwa, kuna pengi na namna nyingi ya kuwekeza.
 
The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
14,328
11,181
Nijuavyo mimi BP wameuza share zao kwa PUMA kwenye usambazaji wa mafuta katika nchi nyingi Africa including Tanzania, Zambia, Botswana na Namibia. Inawezekana TZ process imechukua muda lakini ukienda Namibia sasa utakuta nembo ya BP imebadilishwa na kuwekwa ya Puma. Huo ulikuwa ni mkakati wao wa biashara Africa na si TZ pekee. Hili swala la kesi na politics inawezekana kabisa ikawa ni coincidence!!
 
share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
5,986
10,336
Sioni tatizo. Waondoke tu. Hakuna pigo lolote kwa mtu anayefikiri na kujua biashara. Wapo wengine watakaofanya biashara hiyo tena kwa ufanisi mkubwa. Kwanza BP ilikuwa mwanahisa tu akishirikiana na serikali katika umiliki. Wapo wengine walikwishalimezea macho dili hilo kwa siku nyingi na sasa watalidaka haraka. Acheni kuwapa bichwa hao makaburi. Kwanza lazima ujue kuwa wakati wamefungiwa kwa miezi mitatu cargo yao ya mafuta ilikuwa inauzwa kama kawaida kupitia kampuni ya Engen ambao ni makaburi wenzao. Kama Engen tu waliweza kuinunua cargo yote ya BP na kuiuza kila kukicha sembuse umiliki!!
 
joseeY

Senior Member
Nov 4, 2010
108
17
Naomba kueleweshwa inamaana nembo ya bp sitoiona tena katka vituo vya wese!

Serikali ya Tanzania ina hisa ya asilimia 50, na zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na kampuni ya BP Afrika, lakini kwa sasa kampuni hiyo ya BP imeuza hisa zake kwa kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited. Kutokana na hali hiyo kampuni hiyo itabadilishwa jina wakati wowote kuanzia sasa kutokana na kumilikiwa na kampuni nyingine.
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,434
Kuna taarifa kwamba ccm wameingia mkataba na kampuni ya camel oil, huenda ndiyo itapewa jukumu la kuhakikisha mafuta yanapatikana kwa wingi wa kutosha!!

Vile vile tumeambiwa TPDC wameshafungua tender kwa ajili ya kupata kampuni itakayofanya biashara ya mafuta na COPEC kwahiyo hilo gap la BP linaweza kuzibwa na COPEC!!

Suala la kuchakachua mafuta halihusu depots, uchakachuaji unafanyika mahali pengine kabisa na vijiwe vya kuchakachua vinafahamika.

We pita tu barabara ya morogoro kati ya kibaha na chalinze uone utitiri wa vituo vya mafuta na maukuta marefu yaliyojengwa nyuma ya vituo ama kuzunguka vituo, uone misururu ya malori ya mafuta, then ujiulize ni biashara gani inafanyika humo?

Kwa hatua hii ya BP kuna uwezekano wa nchi kukumbwa na matatizo ya upatikanaji na ubora wa mafuta.
Inabidi wawekezaji wa ndani wajitahidi, tusipate impact yeyote negative kutokana na maamuzi hayo. Hata hivyo Tanzania sasa hivi inawawekezaji wengi sana wakubwa katika sector ya mafuta tuna waarabu wengi tu na wazawa wengi wameibuka katika miaka ya hivi karibuni kama akina Ridhwani Kikwette
 
Edmond

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
359
54
Mafuta yasiyochakachuliwa na usimamizi mbovu tu wa serikali ya ccm, unajua kule depot hakuna mafuta yanachakachuliwa,deal hizo zinapigwa mitaani/vituoni so wakisimamia yatapatikana tu. Lkn pia kujitoa kwao ni pigo kwa ajira za wabongo waliokuwemo nk

Ajira za wabongo zitaendelea kuwepo,kwa maana hawajafunga ofisi,walichofanya ni change ownership pekee
 
MAJANI YA KUNDE

JF-Expert Member
Aug 25, 2008
213
37
HATA JET tayari tulisha ona OILCOM wamenza kulaza tank pale Airport tayari kusammbaza mafuta ya ndege nakubaliana na Zero BP waache zengwe walisha fikia ukomo kwa AFRICA hii imekuwa kama kisingizio tu.
 
alberaps

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,569
994
Few Serious Investor can Work in this Nonsense country! Unless they are in for a big fraudulent deal! PERIOD!
 
mwaJ

JF-Expert Member
Sep 27, 2007
4,074
2,942
BP walikuwa ktk mchakato wa kuuza hisa zao muda mrefu tu hata kabla ya EWURA haijaingilia upangaji wa bei na kuwaadhibu kwa kugoma kuuza mafuta!
Wasilete visingizio muda huu baada ya mchakato kukamilika.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom