Siasa za Upinzani: Kilimanjaro vs Tabora

Siasa za Upinzani: Kilimanjaro vs Tabora

Wengi wetu tunafahamu namna ambavyo mikoa hii miwili ya Tabora na Kilimanjaro ilivyo na umuhimu katika siasa nchi hii.

Tangu wakati wa kutafuta uhuru hadi wakati wa siasa za mageuzi mkoa wa Tabora umekuwa chimbuko la wanasiasa wapinzani kama James Mapalala aliyeanzisha CUF, Chief Abdallah Fundikira aliyeanzisha TADEA, Prof. Lipumba aliyejipatia umaarufu ndani ya CUF kwa kuiongoza kwa miaka kadhaa.

Hata hivyo, pamoja na umaarufu wa wanasiasa hao, bado mkoa wa Tabora haukufanikiwa kuwa ngome ya wapinzani. Ni miezi michache tu iliyopita ndipo CUF ilipofanikiwa kupata mwakilishi kwenye Bunge la Tanzania, ambaye hata hivyo mgogoro uliopo umetishia nafasi yake ya uwakilishi.

Kwa upande wa Mkoa wa Kilimanjaro, kuna wanasiasa maarufu wengi, kuanzia kwenye vyama vyao hadi majimboni. Augustine Mrema (NCCR Mageuzi & TLP), Edwin Mtei (Chadema), James Mbatia (NCCR Mageuzi), Freeman Mbowe (Chadema).

Swali, imekuwaje wenyeviti wa vyama vya upinzani kutokea mkoa wa Tabora washindwe kuimarisha upinzani mkoani Tabora, ilihali wenzao wa Kilimanjaro wamefanikiwa kukitoa jasho chama tawala?

Doesn't charity begin at home?
Lipumba ni Raia wa Congo huko Tabora alizamia tu , hivyo ni vigumu kuaminika
 
Kama kuna udini na ukanda umeanza sana ni awamu hii ya tano. Mola atuepushe sana!
 
Very simple try to review different leaders of Public and private sectors in Tanzania as well as view different names of student who join different University and colleges, the same applied modern and good school. I'm not from Kilimanjaro but Inspire them

If it is simple why don't you present those figures here? Do you consider the difference in regional population size as well? Have you factored in nepotism and favoritism too?
 
Makamanda kwenu exposure ni kuchagua upinzani? Ndio maana lazima mnyooshwe safari hii.
kwani uongo?angalia mikoa yote iliyo juu kielimu imechaguwa chama kipi?na mikoa ambayo iko nyuma imechagua chama gani...halafu urudi hapa ulete mrejesho!
 
Wanyamwezi ni watu kutoka mbele yaani mbele hawana makuu wanajenga kokote sio lazima kwao
 
kwani uongo?angalia mikoa yote iliyo juu kielimu imechaguwa chama kipi?na mikoa ambayo iko nyuma imechagua chama gani...halafu urudi hapa ulete mrejesho!

Kwani hii mikoa ya Tanzania haina makabila tofauti tofauti ingawaje sio kwa asilimia kubwa? Hivi Dar wote ni wazaramo?
 
Mikoa Ipo Mingi Tanzania! Angalau Huko Tabora Wametoa Wanasiasa Walioshindwa Kuendelea Kisiasa!! Je Mikoa Mengine Haihusiki na Siasa?? Au Hukuliona Hilo Bali Umeona Tabora Na Kilimanjaro tu??
Hii Mikoa Mengine si Tanzania au Haistahiki Kuwa Na Wanasiasa??

Lakini Swali La Msingi Hasa Hujalizungumza Ngoja Nikusaidie Pakuanzia!!

1) Mapalala Aliongoza CUF kama Mwenye Kiti! Lakini Baada Alisaliti Katikati Ya Safari! Kwahiyo ni TRAITOR..

2) Lipumba Kaiongoza CUF kama Mwenyekiti! Lakini Baada Ya Upinzani Kuunganisha Nguvu (Yaani Kuunda UKAWA)! Yeye Kasaliti Katikati ya Safari! Kwahiyo ni TRAITOR.

3) Chief Abdalla Fundikira Sina Kumbukumbu nae.

Sasa Swala La Hapa Si Kuwatukana Wenyeji Wa Tabora! Bali Ni Kujiuliza Ni Kwanini Viongozi Wa Upinzani Wanaotoka Tabora Huishia Kuwa Wasaliti???
 
Kuna baadhi ya makabila ni wagumu wa kufanya mabadiliko ili kujikwumua ki maisha, ni waoga hawana uthubutu, sasa ukiongezea na mwamko mdogo wa elimu basi ni matatizo matupu. Kijana wa kinyamwezi ni mara chache sana kumwona akitoka nje ya mkoa kusaka maisha, wengi hubakia karibu na familia (ukoo) wakiendelea kuugawana umaskini. Hii ni nature yetu yaani vina saba vyetu havina chembe chembe ya uthubutu. Pia kuwa makini sana kufanya deal na sisi maana muda wowote ule tunaweza kubadilika bila kujali madhara.
 
kwani uongo?angalia mikoa yote iliyo juu kielimu imechaguwa chama kipi?na mikoa ambayo iko nyuma imechagua chama gani...halafu urudi hapa ulete mrejesho!

Poleni sana Makamanda. Msichanganye demokrasia, uhuru wa kuchagua na matamanioyenu. Ni kama vile kamanda Lema alivyochagua kutokula wakati Lowassa anafyonza mvinyo baridi na washkaji zake wa ccm.
 
If it is simple why don't you present those figures here? Do you consider the difference in regional population size as well? Have you factored in nepotism and favoritism too?
Its very Open simple google or just review leaders of different company, association etc e.g Cleopa Msuya,Reginald Mengi,Johnson Minya, Peter Kibatala, John Malya, Eliach Mrema, Augustino Lyatonga Mrema, James Mbatia, Freeman Mbowe others find yourself, I can not take much time to find for you otherwise you will pay for me. Be educated!!!!!!
 
Makamanda kwenu exposure ni kuchagua upinzani? Ndio maana lazima mnyooshwe safari hii.
Kuna correlation kubwa kati ya kuchagua upinzani na elimu au exposure ya mtu, mikoa mingi iliyochagua upinzani ukiangalia ina kitu kimoja in common, ni wafuatiliaji wa kinachoendele a serikalini na wana elimu, nadhani unabisha hili kwa kuwa wewe ni kada wa CCM, so it's understandable ukibisha ili uendelee kukipa credit chama chako
 
tumeanza kuelekea huko...ndiyo matokeo ya multi party system na globalization
Eti multiparty hata aibu huna.Mbona sasa hivi kama wewe sio mkatoliki Na haujatokea kanda ya ziwa hauna nafasi kwenye utawala wa sasa.Usifukie kichwa chini Kama mbuni ukadhani hauonekani.
 
Kwa hiyo unamaansha hao wa CCM wanaogombea wanakuwa waisilamu au wanakuwa sio wachaga ndio maana wananshindwa?
Basil Mramba hakuwa mchaga na akashindwa mwaka 2010 Rombo? Salakana hakuwa mchaga na kushindwa mwaka 2010 Moshi mjini? Davis Mosha nae hakuwa mchaga? Agrey Mwanry nae hakuwa mchaga akashindwa Siha? Hao walioshindwa mwaka huu walikuwa waisilamu au sio wachaga?

Ukabila wa mkoa wa Kilimanjaro hauko katika mchaga na kabila jingine, upo katika unatokea sehemu gani na unaongea lugha gani, kimachame, kiseri, kishumundu, kikibosho, kimarangu, kisanyajuu nk, pia udini hauko katika muislamu wala mkiristo bali upo katika mlutheri na mkatoliki. Mashirikiano ya kijamii yapo hivyo. Waislamu wa machame wachache wa kutoka katika ethnic zingine za wanaoitwa wachaga wanakuwa kama watoto yatima Kilimanjaro isipokuwa kwa wale waislamu walio matajiri. Matumizi ya hizo jamii katika siasa sizifahamu kwani sijawahi kushiriki siasa za uchaguzi nikiwa Kilimanjaro. Ubaguzi wa kikabila na kidini upo hata bila siasa kama siasa hapa tunamaanisha nani achaguliwe, lakini kama tunamaanisha maisha ya kila siku ya wakazi basi ubaguzi wa kidini na kikabila upo
 
SUKUMA + NYAMWEZI LAND zamani Bomani aliita MWASHITA( Mwanza,Shinyanga & Tabora) The Three Sleeping Giants Kule Usingizi wa Maarifa upo na ndio Chanzo cha Upinzani Dhaifu na Umaskini
 
Eti multiparty hata aibu huna.Mbona sasa hivi kama wewe sio mkatoliki Na haujatokea kanda ya ziwa hauna nafasi kwenye utawala wa sasa.Usifukie kichwa chini Kama mbuni ukadhani hauonekani.

Heeeeeeeeeeeeh!!!!!!!
 
Ukabila wa mkoa wa Kilimanjaro hauko katika mchaga na kabila jingine, upo katika unatokea sehemu gani na unaongea lugha gani, kimachame, kiseri, kishumundu, kikibosho, kimarangu, kisanyajuu nk, pia udini hauko katika muislamu wala mkiristo bali upo katika mlutheri na mkatoliki. Mashirikiano ya kijamii yapo hivyo. Waislamu wa machame wachache wa kutoka katika ethnic zingine za wanaoitwa wachaga wanakuwa kama watoto yatima Kilimanjaro isipokuwa kwa wale waislamu walio matajiri. Matumizi ya hizo jamii katika siasa sizifahamu kwani sijawahi kushiriki siasa za uchaguzi nikiwa Kilimanjaro. Ubaguzi wa kikabila na kidini upo hata bila siasa kama siasa hapa tunamaanisha nani achaguliwe, lakini kama tunamaanisha maisha ya kila siku ya wakazi basi ubaguzi wa kidini na kikabila upo
Hapa tunazungumzia upinzani kuchaguliwa Kilimanjaro ni kwa sababu ya ukabila na udini? kama ni ndio leta ushahidi wako straight, hivyo vingine vyote unavyosema ni upuuzi na hearsay za watu,huu ubaguzi amabo unasemwa sana hapa JF sijawahi kuuona wala ku experince labda Moshi ya miaka ya 70'S
 
Back
Top Bottom