Siasa za sasa za Tanzania, tujifunze kuheshimu mawazo na Maoni ya watu Wengine kudumisha Amani

Nikukumbushe tu, Ndugai alisifiwa kama malaika na watu hawa hawa wakati wanamtukana na kumkejeli Naibu Spika, Tulia. Ni kama wanamtukuza Kikwete saivi wakati kila aina ya tusi, kejeli na dharua alipewa. Nia yao ni kumchafua yoyote aliye kikwazo kwao, hata Lowasa alipewa dosi yake haswaaa.

Ndugai anaonekana mbaya kwao kwa kuwa tu amekataa ujinga wao, vingenevyo angekuwa anamwagiwa sifa tu kama wanavyomwagia sifa Nape saivi. Nami namuunga mkono Ndugai, hatuwezi kuendelea kuendekeza tabia ya matusi na lugha isiyo ya staha bungeni. Wewe unaweza kutukana "fala" mbele ya hadhira namna ile kama si bangi, unataka tuendekeza wabunge wa namna hii kwa maslahi gani ?
Unachosema kinaweza kuwa Kweli lakini ni vema tuangalie tulipojikwaa na sio tulipoangukia nafikiri tatizo Lipo Kwa spika Ivi Kwa mfano spika angesimamia wabunge wakajielekeza kwenye hoja iliyo mezani kusingekuwepo matusi lakini spika anampa mbunge dakika kumi za kuchangia hoja katika hizo kumi tisa zote ni mipasho taarabu zarau matusi kebehi mwisho naunga mkono hoja sasa Basi ni Kwa nini mtu akianza mipasho asitolewe nje Kwa sababu haya mambo yameanzia humohumo bungeni na kulelewa na hao spika yakija uraiani tunaanza kulaumiana huu ujinga imefikia hatua baadhi ya wabunge wakipewa nafasi ya kuchangia wabunge wengine wanajiandaa kucheka Kwa matusi mpaka spika anakenua meno Kwa furaha sasa yamemrudia yeye mnaanza kulaumiana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Synthesizer angalia huu ni mfano hai wa ambao wanafurahia mauaji ya Kibiti, kwao hii ni movement nzuri na ina justification. Watu wa namna hii hawatakiwi si tu kuisogelea Ikulu bali hata kuwa chama cha siasa.
Mkuu, wakati wa ukombozi wa South Afrika, wapigania uhuru wa ANC kuna wakati walivamia mashamba ya Makaburu na kuua hadi watoto. Mandela alikuwa ndani ya chama hicho. Unadhani alifurahia matendo hayo? Hapana. Lakini je, alifurahia ujumbe uliokuwa unaifikia serikali ya Makaburu kutokana na mauaji hayo? Ndiyo.

Humu ndani hata watu wamesema kuna watu wanafurahia polisi wakiuwawa, si kweli. Watu wanafurahia ujumbe unaofika kwa Polisi. Ndio maana hata katika sheria za kimataifa, hata vitani, ni kosa kuwaua maadui mateka au majeruhi.

Hao unaosema wanafuhia Kibiti si kwamba wanafurahia yale mauaji. Wanafurahia ujumbe unaotolewa na mauaji yanayofanyika. Na hili ni jambo la kawaida katika mapambano ya kutafuta haki - huwa linaitwa collateral damage. Kumbuka kwamba wewe kama binadamu wa kawaida uliyeumbwa kwa mfano wa Mungu, si rahisi kufurahia kifo cha binadamu mwenzako - hata kama aliyeuwawa amekuibia wewe binafsi. Unachofurahia ni ujumbe unaofikishwa na kile kifo au justice ndani ya kifo. Kumbuka katika justice, Mungu anapenda watu wote, viumbe vyake, lakini justice itafafanya aangamize watu anaowapenda - na amefanya hivyo hata huko nyuma. Na anasema sifurahii kifo cha mtu mbaya, ni afadali abadilike. Kwa hiyo hata kama mauaji ya Kibiti ni ugaidi wa kisiasa, basi wanaofanya si kwamba wanaua kwa kuwa wanafurahia kuua - wanataka justice, mabadiliko. Justice wanayotaka ikipatikana sidhani kama wataua watu. Na ndicho hicho ninachosema siasa za Tanzania za sasa zinaweza kuleta. Hazileti watu kufurahia kuua watu, bali zinaweza kuleta watu kuua kama njia ya kufikisha ujumbe wa kutaka justice.

Najua, iko complex kidogo.
 
Ndugu, kwa hiyo kwako roho zaidi ya 40 za wananchi wasio na hatia wa Kibiti pamoja na polisi ni collateral damage, serious mtu mwenye ubinadamu unaweza sema hivi. Hivi wangekuwa ni ndugu zako hao ungeweza kusema hivi tena ?

Hivi kweli kuna chombo chochote cha usalama nchi hii wanaweza bariki watu wenye mawazo ya aina hii wachukue nchi ?
 
Kwa kusema kweli kwa upande wangu nilishapunguza ama kuacha kabisa kutoa msaada wa aina yoyote kwa MTU ambae ni mwanachama wa CCM. Na nitaendelea kufanya hivyo ata kama nitabaki pekeyangu hapa Tanzania.

Haiwezekani watu washabikie uonevu unaofanywa na serikali alafu aje kwangu ninaeonewa kuomba msaada Wangu. Mungu atanisamee kwa hayo ninayoyafanya ila sina jinsi.
 
Ni kama Tanzania tumechoka kuwa na amani tuliyofurahia kwa miaka mingi sana. Na sidhani kama Nyerere aliposhauri tuukubali mfumo wa vyama vingi, japo 20% peke yake waliunga mkono, alifikiria kwamba itafikia wakati siasa za vyama vingi nchini zitakuja kuendeshwa katika mandhari ya "uadui". Nina uhakika Nyerere alijua kwamba Watanzania ni watu wenye upendo, uvumilivu na wako tayari kukosoana, sifa ambazo alisisitiza kwa viongozi kuwa nazo siku zote wakati wa chama kimoja kushika hatamu. Nyerere alijua haitakuwa tatizo kuwa na mfumo wa vyama vingi kwa kuwa kwa miaka mingi Watanzania walishathibitisha kuwa watu wa namna hiyo.

Lakini mambo hayako hivyo tena. Ina maana kuwa na upendo, uvumilivu, na kukubali kukosolewa ni mambo yasiyokubalika chini ya mfumo wa vyama vingi? Mtu yeyote mwenye akili timamu, awe chama chochote cha siasa au asiyejihusisha na siasa, ataona kwamba kwa sasa kuna namna fulani ya "kuandamwa" kwa vyama vya upinzani, na hasa viongozi wao. Sidhani kama kuna mtu anapendezwa na hili. Kuna watu wa kila chama cha siasa na wasio na chama, Watanzania halisi, ambao hizi "harassment na hujuma" wanazofanyiwa watu wa upinzani zinawakera sana.

Jambo kubwa kuliko yote ni kwamba Tanzania tunasahau kwamba namna ya siasa zinazoendeshwa kwa sasa ndizo zilizoleta "ugaidi" katika nchi nyingi. Tunasahau kwamba "ugaidi" mara nyingi sana ni matokeo ya utawala uliopo madarakani, katika kutokuwa wenye upendo, uvumilivu na kuwa tayari kukosolewa.

Na tusisahu kwamba jina "ugaidi" linategemea uko upande gani unapolitumia. Gaidi wako anaweza kuwa mkombozi wa mtu mwingine. Mandela alikuwa gaidi kwa Makaburu na rafiki zao, na mkombozi kwa Tanzania na marafiki zetu. Kwa hiyo tunaweza kufikia hatua ya kuitana "magaidi" Tanzania, wakati kwa upande mmoja wa Watanzania, na watu hao hao wakaonwa kuwa "wakombozi" wa sehemu nyingine ya Watanzania.

Ukweli ni kwamba, siku zote, unapoendeleza uonevu kwa kutumia nguvu unahalalisha kujitetea kwa kutumia nguvu (oppressive violence against some people will lead to their justified defensive violence against the oppressor). Hii ndio filosofia iliyotumika na kina Mandela, na iliyosababisha Nyerere kukiunga mkono kikundi cha Biafra ndani ya Nigeria dhidi ya serikali ya Nigeria. Nyerere hakuwaona Biafra na Umkhonto we Sizwe wa ANC, kuwa "magaidi" dhidi ya serikali huru zilizokuwa madarakani katika nchi zao, japo kwa serikali hizo walionekana kuwa "magaidi". Nyerere huyo huyo, aliidhabihu Tanzania kumuondoa Idd Amin madarakani, raisi wa nchi huru ya Uganda. Nyerere huyo huyo alimuunga mkono Laurent Kabila kumuondoa madarakani Mobutu Seseseko, raisi wa nchi huru ya Zaire (DRC).

Turudi nyuma, tutafakari na kujishauri, na turejee misingi ya upendo tunaosifika kuwa nao, kuvumiliana na kuwa tayari kukosolewa. Hatuwezi kusingizia tunamuenzi Nyerere bila kuwa na hizi sifa. Itakuwa ni unafiki wa kiwango cha juu sana, hata kama tumejivika kanzu ya uzalendo.
Thanks a lot Mkuu, usikatishwe tamaa na wanao toa kejeli kwa bandiko lako. kila mmoja mwenye akili timamu na mwenye kutambua thamani ya uwepo wake hapa duniani amekuelewa. Ubarikiwe....!
 
Mbegu ya chuki,hasira na visasi ndo inayopandwa huku ikimwagiliwa na makamanda wa mikoa.Sasa hivi watu hawazikani wala kujumuika kwenye sherehe steji itakayofuata siijui lakini mwishoni anayehisi anaonewa kwakuwa hanavyombo vya kumlinda atatafuta njia nyingine ya kutibua utulivu ili sasa wote wawe na hekaheka za kuokoa roho tu.Taifa linawazee lakini chaajabu nawao wamekuwa waoga kukemea au kusema chochote juu ya tuendako.
MUDA NDIO MSEMA KWELI
Hamzikani ninyi mnaoendekeza siasa uchwara lakini tusiokuwa na hizo itikadi zenu za vyama tunashirikiana shughuli za kijamii kama kawaida,nyie endeleeni na hayo masiasa yenu..!!
 
Wanaoingia misituni Congo, Uganda, Rwanda, Sudani kusini ni mazao ya madikteta uchwara.
Najua hatutafika hapo lakini naye atakiona anachokiona Mhe. JMK kama ailichokiona BWM siku za mwanzo za utawala JMK. Hata Mwl JKN. alikiona cha moto baada ya kumuachia AHM. Naye AHM alikiona cha mtema kuni kutoka kwa BWM. Tusubiri.
 
Mkuu, ni wazi haya mambo ni mazito sana kwako kuelewa. Tembea upaue wigo wako wa kufikiri, au angalau soma na kusikiliza kinachoendelea nchi nyingine. Panua kufikiri kwango nje ya mipaka ya Tanzania.
Ni wewe usiyejitambua kuwa unatumiwa na wenye uchu wa madaraka. Kama demokrasia ya mawazo imeminywa, hili jamvi unalotumia kukosoa lisingekuwepo. Hata hao wenye uchu wa madaraka wangekosa jukwaa la kuongea hayo matusi, kejeli na kebehi.
 
Hivi ndivyo mnavyokimbilia kusema siku zote. Hata kwenye masuala ya ufisadi na uhujumu uchumi huu ndio wimbo wenu. Halafu baadaye Chorus inabadilika.
 
Ni kama Tanzania tumechoka kuwa na amani tuliyofurahia kwa miaka mingi sana. Na sidhani kama Nyerere aliposhauri tuukubali mfumo wa vyama vingi, japo 20% peke yake waliunga mkono, alifikiria kwamba itafikia wakati siasa za vyama vingi nchini zitakuja kuendeshwa katika mandhari ya "uadui". Nina uhakika Nyerere alijua kwamba Watanzania ni watu wenye upendo, uvumilivu na wako tayari kukosoana, sifa ambazo alisisitiza kwa viongozi kuwa nazo siku zote wakati wa chama kimoja kushika hatamu. Nyerere alijua haitakuwa tatizo kuwa na mfumo wa vyama vingi kwa kuwa kwa miaka mingi Watanzania walishathibitisha kuwa watu wa namna hiyo.

Lakini mambo hayako hivyo tena. Ina maana kuwa na upendo, uvumilivu, na kukubali kukosolewa ni mambo yasiyokubalika chini ya mfumo wa vyama vingi? Mtu yeyote mwenye akili timamu, awe chama chochote cha siasa au asiyejihusisha na siasa, ataona kwamba kwa sasa kuna namna fulani ya "kuandamwa" kwa vyama vya upinzani, na hasa viongozi wao. Sidhani kama kuna mtu anapendezwa na hili. Kuna watu wa kila chama cha siasa na wasio na chama, Watanzania halisi, ambao hizi "harassment na hujuma" wanazofanyiwa watu wa upinzani zinawakera sana.

Jambo kubwa kuliko yote ni kwamba Tanzania tunasahau kwamba namna ya siasa zinazoendeshwa kwa sasa ndizo zilizoleta "ugaidi" katika nchi nyingi. Tunasahau kwamba "ugaidi" mara nyingi sana ni matokeo ya utawala uliopo madarakani, katika kutokuwa wenye upendo, uvumilivu na kuwa tayari kukosolewa.

Na tusisahu kwamba jina "ugaidi" linategemea uko upande gani unapolitumia. Gaidi wako anaweza kuwa mkombozi wa mtu mwingine. Mandela alikuwa gaidi kwa Makaburu na rafiki zao, na mkombozi kwa Tanzania na marafiki zetu. Kwa hiyo tunaweza kufikia hatua ya kuitana "magaidi" Tanzania, wakati kwa upande mmoja wa Watanzania, na watu hao hao wakaonwa kuwa "wakombozi" wa sehemu nyingine ya Watanzania.

Ukweli ni kwamba, siku zote, unapoendeleza uonevu kwa kutumia nguvu unahalalisha kujitetea kwa kutumia nguvu (oppressive violence against some people will lead to their justified defensive violence against the oppressor). Hii ndio filosofia iliyotumika na kina Mandela, na iliyosababisha Nyerere kukiunga mkono kikundi cha Biafra ndani ya Nigeria dhidi ya serikali ya Nigeria. Nyerere hakuwaona Biafra na Umkhonto we Sizwe wa ANC, kuwa "magaidi" dhidi ya serikali huru zilizokuwa madarakani katika nchi zao, japo kwa serikali hizo walionekana kuwa "magaidi". Nyerere huyo huyo, aliidhabihu Tanzania kumuondoa Idd Amin madarakani, raisi wa nchi huru ya Uganda. Nyerere huyo huyo alimuunga mkono Laurent Kabila kumuondoa madarakani Mobutu Seseseko, raisi wa nchi huru ya Zaire (DRC).

Turudi nyuma, tutafakari na kujishauri, na turejee misingi ya upendo tunaosifika kuwa nao, kuvumiliana na kuwa tayari kukosolewa. Hatuwezi kusingizia tunamuenzi Nyerere bila kuwa na hizi sifa. Itakuwa ni unafiki wa kiwango cha juu sana, hata kama tumejivika kanzu ya uzalendo.
Bila hata kusoma kilichomo,kichwa tu cha habari kimfanya nikuunge mkono

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa wanapanda mbegu ya chuki, huweki kumweka ndani kiongozi wa chama chenye wabunge zaidi ya 30 wa kuchaguliwa, chama chenye kura mil 6 dhidi ya mil 8 yaani tofauti ya kura mil 2 tu za yule aliyeko madarakani. Unamweka ndani tena bila sababu za msingi. hapa unapandikiza chuki kubwa kwenye taifa lako, watu mil 6 si wa kubeza.

Ni kweli lazima watu waheshimu sheria zilizopo lakini makosa mengi yanakuwa hayana maana. Watanzania ni watulivu na wavumilivu lakini kuna siku uvumilivu wao utafikia kikomo.
 
Sishangai kwa akili yako hata kufurahia mauaji ya Kibiti, huna utu wala ubinadamu. Tanzania lazima isimame na ilindwe vilivyo dhidi ya wajinga wa aina yako. Ingieni msituni na mtafundishwa somo zuri sana la maana ya uhaini na jinsi mhaini anashughulikiwa.
Na wakithubutu kuingia msituni utafanya nini, watu wanatoa mawazo constructive wewe unajifanya ubabe ambao hauna lolote, kama ungekuwa na lolote lingeonekana kibiti sasa huo ni mfano tuu ambao unapewa live unajitia kichwa ngumu. Hapo tuu kaeneo kadogo kamepasua kichwa. What if kila mahali pakilipuka una nini wewe cha kufanya. Leo kwa kiburi unawaambia watu ingieni msituni. Wee nani Nchi hii bwana. Aliyedai uhuru mwenyewe hayupo.
 
Back
Top Bottom