Mwanakijiji,
Sina hakika kama ni Mbeya tu; lakini kwa ujumla wake, huyu jamaa alipewa U-RC Mbeya kwa kazi maalum, hasa baada ya kujeruhiwa vibaya sana na Mwakyembe kwenye kura za maoni, ndipo mtandao ukampa U-RC ili amshungurikie Mwakyembe kwa upande mmoja na Mwandosya kwa upande mwingine. Na jamaa anawajibika kweli kweli katika katika kumdhibiti Mwakyembe, kwani alishapewa green light na wazee wenyewe. Rejea kamati ya Kinana na matokeo yake pale Mwakyembe alipolalamika kwa JK kwamba Mwakipesile anahujumu juhudi zake.
Mafuchila,
Hii case ya Mwakyembe na Mwakipesile kwa mawazo yangu wote wawili wana makosa makubwa sana kwa wana Kyela. Wameruhusu migogoro yao binafsi idumaze shughuli za maendeleo za Kyela.
Mimi nawajua wote wawili kwa karibu na kila mmoja wao ana kosa kwenye hili.
Nafikiri unajua kwamba Mwakyembe alifanya foul kubwa sana kwenye uchaguzi
wa kuteua mgombea wa CCM. Walimzidi speed Mwakipesile kwa kutorosha wajumbe na kwenda kuwalaza Rungwe kabla ya siku ya uchaguzi. Kundi la Mwanyembe waliandaa magari ambayo yaliwafuata wajumbe na kuwaambia wametumwa na Mwakipesile kwenda kuwachukua na kwamba watakaa hotelini mpaka kesho yake ambapo uchaguzi ulikuwa ufanyike. Walivyopakiwa, kituo cha kwanza kikawa kwenye hizo Guest houses huku Rungwe. Mwakipesile alivyogundua akachanganyikiwa. Haijulikani nini kilitokea huko, lakini Mwakyembe akashinda huo uchaguzi.
Pamoja na kwamba mimi nilikuwa nimechoshwa na Mwakipesile na nilikuwa namuunga mkono Mwakyembe, lakini sikufurahia hiyo njia waliyotumia. Ilikuwa ni rushwa na uvunjaji wa sheria wa hali ya juu.
Baada ya uchaguzi Mwakyembe na kundi lake walikuwa wanarusha vijembe vingi mno dhidi ya Mwakipesile kiasi cha yule mzee kukosa raha pale Kyela. Mimi niliwahi kumshauri Mwakyembe akutane na Mwakipesile waongee na kuyamaliza maana ule ulikuwa uchaguzi. Hofu yangu ilikuwa ni Kyela kugeuka kama Zanzibar ya Hamad na Komandoo. Kundi la Mwakyembe walipuuza na kusema amekwisha huyo.
Baada ya muda baraza la mawaziri likatangazwa na Mwakyembe hakuwemo. Kulikuwa na uvumi mkubwa Kyela kuonyesha kwamba Mwakyembe alienda kugombea ubunge kwa kuamini kwamba atapata uwaziri. Watu wa Mwakipesile wakafanya sherehe kushangilia Mwakyembe kutokuwa waziri.
Haikupita muda Mwakipesile akateuliwa kuwa mkuu wa mkoa. Mwakipesile baada ya kuapishwa tu safari ya kwanza Kyela kwenda kutamba na gari lake la ukuu wa mkoa. Pia akaanza kupinga mipango mbalimbali ya maendeleo ambayo Mwakyembe alikuwa anataka kufanya.
Kama hiyo haitoshi Mwakyembe akaanza kuandika barua kwa PM Lowassa kulalamikia kitendo cha Mwakipesile kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na kwamba hiyo ni dharau kwa wana Kyela. PM akawa anamwonyesha hizo barua Mwakipesile. Kwahiyo ugomvi badala ya kupungua ukawa unaongezeka.
Ukiaangalia maelezo hapo juu utaona wote wawili wana matatizo yao ambayo yanatokana na ubinafsi na hakuna faida kwa Kyela. Mwakipesile inabidi akubali kwamba Mwakyembe kachaguliwa kihalali na wananchi wa Kyela na amsaidie kutimiza majukumu yake. Mwakyembe naye hakuna haja ya kulalamikia mwenzake kupewa cheo. Alitaka sasa mpaka Mwakipesile afe njaa? Kwa wote wawili lazima waweke maslahi ya Kyela mbele kuliko masters wao Dar au chama chao. Vinginevyo wote wawili wataishia kujiangusha machoni mwa wana Kyela.
Kwa uwezo Mwakyembe ana uwezo mkubwa sana na huwezi kumlinganisha na Mwakipesile ila ni too ambitious na hajua kabisa grassroot politics. Wakati huku kitaifa kazi yake inaonekana, kule Kyela hapatikaniki kabisa, sio rahisi kwa wananchi kuonana na mbunge wao. Pia ni msanii, Mwakyembe akikuambia njoo kesho, wewe endelea na safari zako maana hiyo kesho huwezi kumwona.
Kama sasa wanapanga Mwakyembe afike Kyela weekend kwasababu wanajua Mwakipesile weekends zote anakuwa Kyela. Wanataka kumlima vijembe, jambo ambalo sio zuri kabisa. Ilitakiwa Mwakyembe aseme hapana, huo mpango sio mzuri.
Labda sasa ni kumwomba mheshimiwa rais ili amhamishe Mwakipesile kwenda mkoa mwingine. Mimi kama mwana Mbeya ni heshima kuwa na wana Kyela wawili wenye nafasi. Hata siku moja siwezi kuomba Mwakipesile aondolewe kuwa mkuu wa mkoa. Ila kwasababu imeshindikana hao mafahari wawili kukaa pamoja, basi Mwakipesile ahamishiwe mkoa mwingine.
Mwakipesile anaungwa mkono na afisa usalama wa taifa aliyemaliza muda wake, bwana Apson. Pia ana makada wa CCM ambao wanamwunga mkono sana kwasababu yeye kila alichokuwa anapata, alikuwa anagwana nao. Kwa habari ambazo naziamini kwa asilimia kama 90, ni kwamba Mwakipesile hana mpango wa kugombea ubunge tena Kyela. Labda amegundua kwamba hata akigombea atashindwa. Nasema ni tisini kwasababu kwenye siasa lolote linaweza kubadilika. Yeye anasema maadui zake walimtafutia mtu ili amshinde na labda na yeye anamtafuta mtu wa kupambana na Mwakyembe sasa.
Hizo ni za jikoni kabisa kuhusu hawa waheshimiwa wawili.