Dr A. Paurine
Sasa unajidhihirisha wazi ni jinsi gani ulivyogubikwa na wingu la uchadema; upo tayari kupotosha ukweli; watanzania tupo kwenye amani; pamoja na matatizo yetu ya kiuchumi bado watanzania wengi wana nafasi ya kujiajiri kwenye kilimo na kujipatia vipato halali na kupata amani ya moyo. Serikali ya CCM imeweka kipau mbele kuhahakikisha watanzania wanajiajiri kwenye kilimo; serikali haiwezi kuwalimisha wale ambao kwa makusudi wamekimbia vijijini na kuacha shughuli za kilimo kwa kudhani mjini ndio kwenye neema zote; homeless wa Tanzania ni wa kujitakia; nadhani ulichokiandika umeandika bila kufanya utafiti au umeamua kuwa mpotoshaji badala ya kuwa muelimishaji; kama unataka tukupe darasa la matatizo ya kiuchumi tuliyokuwa nayo na nini kifanyike kupunguza athari sema tukufundishe bahati nzuri ni moja ya moja ya eneo ninalolimudu na nimetembea sehemu nyingi na nina uwezo wa kulinganisha matatizo ya nchi za Afrika; narudia tena usipotoshe watu Tanzania tuna amani kubwa sana na watanzania wana nafasi kubwa sana kujikwamua kimaisha
Turudi kwenye ziara yetu Morogoro
Kuna tofauti kubwa sana ya speech ikitolewa na politician na activist; viongozi wa CCM ni wanasiasa wanamwaga sera na kusikiliza kero na kujadiliana na wananchi kwenye mada husika na ndio sababu mikutano yao inatawaliwa na amani hiyo ndiyo siri kubwa; kwa Chadema ni tofauti viongozi wao wamegeuka activists wanachojua ni kuhubiri na kuwajaza watu hisia kali kwa kutumia uwongo wa kila aina na hicho ndio kimekuwa ndio kiini cha uvunjaji wa amani; mikutano mingi ya Chadema baada ya kumalizika kinachofuatia ni uvunjaji wa amani wa makusudi. Mkuu usiidhalilishe taaluma yako kwa kuongea vitu ambavyo huna uhakika navyo.
Chama
Gongo la mboto DSM