Paragraph yako ni fupi lakini ina maneno mazito sana. Amani ipi? nakumbuka kabla sijatoka nje niliamini kwamba nchi yangu ni nchi ya amani sana. Nilivyo ishi nje ndo sasa naelewa maana ya amani ni nini. Tanzania kama nchi inahesabika kama nchi yenye utulivu lakini watu wake hawana amani hata kidogo nikimaanisha walionacho na wasio nacho. Mtu anayelala njaa hana amani, mtoto anayelala mtaani hana amani, ombaomba hana amani, mkulima hana amani, mfugaji and so on. Matajiri wenye nacho ndo kabisa wakiwa kwenye magari vioo mpaka juu, ma-gates nyumbani, walinzi na bunduki mchana kutwa majumbani, ubakaji uvunjifu wa haki za binadamu kila kona. Wanyama nao hawana amani, misitu inachomwa, wanauliwa hovyo kinyume cha sheria nk. Makazini ndo shida kabisa wengi hawana uhakika na kesho, sumu utalishwa ukipiga kelele, siasa ndo basi nisiseme maana ni kazi kweli kweli.
Zaidi Ukisingiziwa kibaka raia ni kama ruksa kukuua, ukikimbilia polisi ni afadhali ya uraiani. Ukienda jela nasikia ni jela kweli kweli. Ukienda mahospitalini ndo amani imetoweka...daktari akiua ni kazi ya mungu....ndugu yangu hatuna amani kabisa ni maneno tu ya kutufurahisha. Kwa wenzetu ukisikia amani ni amani kweli kweli kiasi kwamba mtu akikuvyonza polisi watasaidia kama wakihitajika, mbwa panya nk nao wanapatiwa huduma ya ambulance. nyumba unasahau mlango na kurudi kesho yako unakutakila kitu kiko vile vile. Ofcoz kuna vi-pockets vidogovidogo vya uvunjifu wa amani lakini vinakuwa addressed effectively.
Kuhusu viongozi wenu Morogoro, ni kweli hakuna vurugu wala uvunjifu wa amani kwa sababu wanalindwa na vyombo vya dola...Kuhusu sera kweli wana sera lakini wamekuwa na sera hizo kwa muda wote wa utawala na maisha ya mtanzania yanarudi nyuma ktk kila sekta, elimu, afya, utamaduni, uchumi(time bomb), mahusiano ya ndani nk. Kuna sababu za msingi za kuibadili system iliyopo na hili litawezekana nje ya utawala wa sasa. "Tatizo haliwezi kutatuliwa na uwezo wa kuwaza ule ule uliolitengezeza" na matatizo ya Tanzania kwa imani yangu yametengenezwa na chama tawala...