Siasa za majitaka CHADEMA tuziache

Siasa za majitaka CHADEMA tuziache

Status
Not open for further replies.
Ni kweli kuwa mimi nimefanya sana siasa za majitaka. Lakini ninatambua kuwa siasa safi hujenga nchi. Siasa za maji taka sikuzianzisha mimi, ila nimelazimika kuzifanya kwa sabau siasa za maji taka hazijibiwi kwa siasa safi.

Unakumbuka Hillary Clinton aliposema "shame on you Barack Obama" kule Ohio?

Kama vijana wa bavicha walioanzisha siasa za majitaka September 2010 watajirudi na kuendeleza siasa safi kwa maslahi ya taifa, zemarcopolo atakuwa na siasa safi kwa sababu siku zote zemarcoplo alikuwa na siasa safi mpaka alipogundua kuwa tuko kwenye dindwi la siasa za majitaka.

Hili ni jibu Mujarab ZeMarcopolo
 
Last edited by a moderator:
Kumuunga mkono Lusinde ni jambo moja, lakini kumkosoa inawezekana kama alivyofanya Filikunjombe leo.

Nauliza tu iwapo na wanaofanya siasa za majitaka upande wa pili umewakemea?

CCM walipoanza propaganda za udini tangu enzi za CUF mbona hukukemea?

Mbona hukukemea pale Salim alipochafuliwa kuwa anahusika na kumuua Karume?

Hapo ndipo napata shida kama kweli unazichukia siasa hizo za majitaka au unachukia watu ndani ya Chadema, maana umejionyesha wazi majitaka yako kwa Chadema ni kwa baadhi ya wana Chadema (Zitto humgusi)!

You need not go so low!

Kama umenifuatilia vizuri nadhani utakuwa umenotice vitu viwili 1) Sijadili mada za udini. 2) Sijadili wanaotajwa kugombea Urais ndani ya CCM.

Kila kitu kina sababu yake.

Hapo naona umejiunga mwaka 2012. Sijajua kama hapo ndio mara yako ya kwanza kuifahamu JF au ulikuwa unasoma mada za JF kabla ya hapo, lakini nikupe tu historia kwa kifupi. Around september 2010 waliibuka vijana wa bavicha in huge numbers (tuliamini vijana wengi walikuwa na multiple IDs). Vijana hawa likiandikwa jambo lolote ambalo linahoji chadema basi wanajibu ----. Thread moja unaweza kukuta posts kama 20 mfululizo zimeandikwa ---- na kejeli mbalimbali. Jambo hili lilisababisha waumiaji wengi wastaarabu wa JF kujiweka pembeni. Kuna watu kama Rev. Kishoka (Mzee wa TPP Maendeleo) alikuwa mtu fresh sana kwenye mijadala. Ila tangukipindi hicho amekuwa very passive.
Halafu mijadala ilikuwa spontaneous, mtu anatoa mchango kutokana na thread. Siku hizi ukiona mtu amechangia unaweza kuhisi alichoandika kwa kusoma jina lake tu. Michango sio spontaneous.

Chadema ina kitengo maalum cha mitandao ya jamii ambacho ndicho kinachoratibu tabia hii. Wakiambiwa waache itakuwa vizuri kwa sababu wengi tunapenda siasa safi kwa kutambua kuwa siasa safi hujenga nchi.
 
Nimejiunga 2012 lakini ni mfuatiliaji mzuri sana humu hata kabla sijajiunga.

Niliona propagandists wa pande zote mbili. Walikuwepo wa Chadema lakini walikuwemo humu akina Rejao, Ritz, chama, Faizafox, malariasugu, zomba n.k ambao nao walikuwa wanafanya mchezo huo huo kwa upande wa CCM.

Nadhani wewe, ambaye ni kati ya wana JF ambao nawakubali hapa JF, ulikubali kujiingiza kwenye kundi ambalo halikufai. (Naheshimu uamuzi wako, na wala silazimishi ubadilike)

Wewe, kama walivyo akina Mchambuzi, Mzee Mwanakijiji, n.k. ndio great thinkers ambao tukiona majina yenu kwenye post tunajua tunajifunza kitu. Sasa kwa nini ushuke chini namna hiyo? MKJJ na mchambuzi wamekwepa kishawishi hicho.

Lakini pia siasa za majitaka hazikuanzia hapa JF. Zilianzishwa na CCM tangu wakati wa CUF, tumeambiwa CUF ugaidi, CUF udini mbona sasa wamewanyamazia hao wadini na magaidi? Walibadilika lini?

Huwezi kusafisha system chafu kwa kuamua kuwa mchafu pia.
 
Nimejiunga 2012 lakini ni mfuatiliaji mzuri sana humu hata kabla sijajiunga.

Niliona kuna watu walikuwemo humu akina Rejao, Ritz, chama, Faizafox, malariasugu, zomba n.k ambao nao walikuwa wanafanya mchezo huo huo kwa upande wa CCM.

Nadhani wewe, ambaye ni kati ya wana JF ambao nawakubali hapa JF, ulikubali kujiingiza kwenye kundi ambalo halikufai. (Naheshimu uamuzi wako, na wala silazimishi ubadilike)

Wewe, kama walivyo akina Mchambuzi, Mzee Mwanakijiji, n.k. ndio great thinkers ambao tukiona majina yenu kwenye post tunajua tunajifunza kitu. Sasa kwa nini ushuke chini namna hiyo? MKJJ na mchambuzi wamekwepa kishawishi hicho.

Lakini pia siasa za majitaka hazikuanzia hapa JF. Zilianzishwa na CCM tangu wakati wa CUF, tumeambiwa CUF ugaidi, CUF udini mbona sasa wamewanyamazia hao wadini na magaidi? Walibadilika lini?

Huwezi kusafisha system chafu kwa kuamua kuwa mchafu pia.

Kama uko fair utakubali kuwa vijana wa bavicha ndio walioharibu hii JF.

Kuna njia nyingi za kutatua tatizo. Tunapokuja kwenye kujadiliana ni lazima kuwa tayari kusikia options mbalimbali na tizishindanishe kwa hoja. Mwisho hoja yenye uzito itashinda au pengine mjadala unaweza kuisha kwa kukubaliana kutokukubaliana kwenye jambo husika.
Tatizo ni pale vijana wa bavicha wanapotanguliza matusi badala ya hoja.

Mimi nimefanya siasa za majitaka, lakini sijawahi kumtukana mtu. Ninafanya siasa za majitaka kwa style ambayo hata Hillary Clinton alifanya, Barack Obama alifanya na ina wakati wake, mahala pake na lengo lake.
Vijana wa bavicha wao kila mada wanarusha matusi tu, kila jukwaa matusi na kejeli. Hatupaswi kwenda hivyo, tunachelewesha maendeleo...
 
Mimi nimefanya siasa za majitaka, lakini sijawahi kumtukana mtu. Ninafanya siasa za majitaka kwa style ambayo hata Hillary Clinton alifanya, Barack Obama alifanya na ina wakati wake na lengo lake.
Haya mkuu.

Jua kuwa, I was your fan, but you are losing me.

And I am sure you are losing many more, because your end does not justify the means you are using.

You are far better than that brother.
 
Kama uko fair utakubali kuwa vijana wa bavicha ndio walioharibu hii JF.

Kuna njia nyingi za kutatua tatizo. Tunapokuja kwenye kujadiliana ni lazima kuwa tayari kusikia options mbalimbali na tizishindanishe kwa hoja. Mwisho hoja yenye uzito itashinda au pengine mjadala unaweza kuisha kwa kukubaliana kutokukubaliana kwenye jambo husika.
Tatizo ni pale vijana wa bavicha wanapotanguliza matusi badala ya hoja.

Mimi nimefanya siasa za majitaka, lakini sijawahi kumtukana mtu. Ninafanya siasa za majitaka kwa style ambayo hata Hillary Clinton alifanya, Barack Obama alifanya na ina wakati wake, mahala pake na lengo lake.
Vijana wa bavicha wao kila mada wanarusha matusi tu, kila jukwaa matusi na kejeli. Hatupaswi kwenda hivyo, tunachelewesha maendeleo...

Nafurahi sana kusikia kwamba hujawahi kumtukana mtu. Na kama huo ndo ukweli wako ni vyema ukawa kioo cha jamii kwa kuonesha mfano bora kwa vijana hawa wa bavicha...Kama umeshagundua siasa za maji taka zinachelewesha maendeleo, basi iwe wajibu wako kuzikemea na sikuziongezea moto. Saidia kubadilisha utamaduni wa matusi kwa kutotoa matusi hata pale unapojihisi unaulazimika, jizuie. Kwa kufanya hivyo utachangia sana maendeleo ya jamii yako na ustawi wa JF
 
Siasa za majitaka zimeanza kuchukua kasi CHADEMA baadhi ya viongozi wanaitwa masalia wakati ni viongozi wa juu wa chama this is bad either we fire or w retain naogopa kuna watu wanatumika kudisqualify baadhi ya viongozi kwa kuwaita wasaliti na wengine waonekane wanajengeka chama nyumba moja kugombania fito kwanini.

Kwahyo kwa akili yako huamini kwamba kuna mapandikizi wako cdm wanafanya kazi ya ccm?huitaji digrii kulijua hilo haiwezekani wengine wanakwenda mbere wengine wanawarudisha nyuma wavumiliwe ili iweje?sio wote waliopo chadema wanadhamila ya kweli japo zamani tuliwaamini kiivyo,leo tuna viongoz wana mahusiano mazuri na ya karibu na mwiguru,wanakunywa wanakula na kuteta pamoja, je unadhani hapo kuna nini?kama mwiguru alitumia mitambo kutuma sms za vitisho kuonyesha kuwa ni mh,Mnyika na Mh lissu ndio simu zao zimehuska na akapaza sauti mbele ya bunge kuwa ana ushahid kuwa ni wao,mtu kama huyo anakuwa na mahusiano ya karibu na mbunge na kiongoz mwandamiz wa chama unategemea nini hapo kama sio kukisaliti chama?
 
Nafurahi sana kusikia kwamba hujawahi kumtukana mtu. Na kama huo ndo ukweli wako ni vyema ukawa kioo cha jamii kwa kuonesha mfano bora kwa vijana hawa wa bavicha...Kama umeshagundua siasa za maji taka zinachelewesha maendeleo, basi iwe wajibu wako kuzikemea na sikuziongezea moto. Saidia kubadilisha utamaduni wa matusi kwa kutotoa matusi hata pale unapojihisi unaulazimika, jizuie. Kwa kufanya hivyo utachangia sana maendeleo ya jamii yako na ustawi wa JF

Sawa, asante kwa ushauti mzuri. Ninaamiini kuwa na wewe umeanza kuutumia ushauri huu mzuri ingawa wahenga walisema mganga hajigangi (you are challenged to defy wahenga).
 
Mboe na Dr.Slaa ni Maungu watu ndani ya CDM,kisiasa ni Madikteta.ukihoji chochote kuhusu WAKANDA hawa,unaonekana ni msaliti,pia unapata dhambi!!,kwasababu wafuasi wao wengi wanatoka upande mmja kwa nchi,wanaamini sehemu zingine hawana akili.Mtaendelea kuwa wapinzani na safari hii yan 2016 TUNDU LISU atachomoza na kudai usawa,hapo ndio mtajamba cheche na mtakunya mto,kudadadeki!!!
 
Ukiwa mtaani hasa maeneo ya mijini ni dadra sana kusikia mtu anaisifia CCM, wapo watu wanapenda CCM iendelee kuwa madarakani ingawa watu hao huwa hawasemi wazi. Unaweza ukawaona kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia Nick names.

Zifuatazo ni sababu zinazofanya baadhi ya Watanzania kulilia CCM ibaki madarakani pamoja na umasikini, ufisadi uliokithiri kufikia hatua ya kushika nafasi ya pili kwa ufisadi Afrika mashariki, point moja tu baada ya uganda.

1. Watu hao kwa sasa wananufaika na mfumo wa sasa, kwani ni mfumo ambao uko loose,kundi hili ni waajiriwa serikalini. Wafanyakazi wa Serikali wamefanikiwa kuvuna pesa za wizi serikalini wanaomba hali iendelee kuwa kama ilivyo, CCM iendelee kutawala .

Wengi wetu tunawafahamu rafiki zetu walioko serikalini bila kujali kuwa wana nafasi za juu au za chini wamefanikiwa kutajirika ghafla, tunawafahamu lakini hakuna mahali pa kuripot kwakuwa system nzima ni Corrupt.

2. Wako wafanyabiashara wanaokwepa kodi, serikali imegubikwa na rushwa kwa hiyo hawawezi kukusanya kodi, kila kitu kinakwenda kwa dili au ten %. Hawa nao wanasema kidumu chama cha mapinduzi

3. Wako ambao wamezaliwa kwenye familia tajiri, wakiamka asubuhi wanajiuliza ama wale soseji au mayai. Friji zao Zimejaa kuku, samaki nk. Pia wanachagua watoke na aina gani ya gari. Kundi hili halifahamu vizuri umasikini uliowagubika watanzania, shida wanazisikia kwenye vyombo vya habari, maisha yao hawajichanganyi na masikini kabisa, wanasoma shule na vyuo vya kitajiri kwa hiyo umasikini hawaujui. Kwa hiyo hawaoni kosa la CCM

4. Masikini lakini wanaipenda CCM mpaka kesho. Kundi hili liko vijijini. Linaipenda CCM kwa sababu ya kukosa elimu ya uraia, au hawapati habari kabisa. Shughuli yao kubwa ni kulinda nyani wasivamie mashamba yao. Kundi hili halijui maana ya maendeleo, wanatamani hata shule zisiwepo ili watoto wachunge ng’ombe na kulima, wakivuna mazao ya kutosha wakala wakashiba hata kama hawana shilingi ya kununua ndala wao usema CCM oyeeeee

5. Kuna kundi ambalo lenyewe limedanganywa kwa uvumi au kwa mazoea tu. Kwamba bila CCM kutakuwa na vita, linasema CCM imenilea hadi hapa nilipo. Kundi ili liko tayari kuchagua hata fisadi au jiwe ilimradi tu atokee CCM. Kundi hili linafahamu kabisa kuwa serikali haifanyi vizuri lakini kwa mazoea lenyewe limeendelea kuomba CCM ibaki madarakani ili amani iendelee kuwepo.

6. Imani. Kundi hili ni mchanganyiko wa wasomi na wasiosoma. Hawa kwa sababu ya imani kali kwa dini limehamua kuweka dini mbele lakini maendeleo baadae. Kundi hili linafahamu kabisa madudu ya CCM lakini limeendelea kuwa na msimamo kwa CCM. Kundi hili udanganywa kirahisi kwa propaganda za CCM kwamba Chama fulani ni cha dini fulani. Bila kujali msitakhabali wa nchi uamua kushabikia CCM lakini baada ya miaka mitano huwa halioni mabadiliko ya kmaendeleo. Kundi hili ndilo linalochelewesha mapinduzi ya nchi, kundi hili ukesha likiomba CCM iweke mtu wa dini yake bila kujali uwezo wa kiongozi husika.

7. Mafisadi papa. Hili ni kundi ambalo ni chafu kabisa, halina hata dini. Limeiba pesa nyingi za Watanzania bila kujali kuwa kila siku kuna masikini wanakufa kwa kukosa dawa mahosipitalini. Kundi hili kwa kutumia nguvu ya pesa za wizi linatamani ligawie kila mtanzani laki moja ili wapigie kura CCM. Kundi hili linahitaji CCM idumu ili lipate security ya mali zake, liko tayari hata kuua au kung'oa mtu kucha anaehatarisha CCM kuanguka. Linahofu kuwa chama kingine kikiingia madarakani litafilisiwa na kupelekwa mahakamani. Ni kundi lenye nguvu kubwa hata sasa ndani ya CCM

Mkuu uchambuzi wako kiasi kikubwa una ukweli,ingawa napenda kukuomba unapofanya uchambuzi usijumuishe watu wote.Mf kundi na moja,wapo watumishi wengi wa umma wasioridhishwa na mwenendo wa serikali iliyopo.Na jambo la kustaajabisha ni kwamba chuki waliyonayo kwa serikali ni kutokana na baadhi tu viongozi wao wanaowanyima haki zao pasipo sababu zozote za msingi!Unakuta serikali imetoa pesa za malipo mbalimbali,alafu kiongozi mmoja anahujumu pesa hizo kwa kushirikiana na baadhi ya wahasibu na madiwani,hata udai hadi utambikie,hutasikilizwa na mtu na unaweza kupewa jina baya ili wakushughulikie vizuri!Sasa ukiona hata mtu kama Waziri mkuu anawatetea hao wababe ni lazima itakuuma na hutakipenda chama chao.Bahati mbaya tena,ukikutana na baadhi ya watu waliolishwa sumu ya m4c na waliona hisia kama zako,wanakuona wewe si mwenzao ingawa ukweli ni kwamba Wengi wa watumishi wa umma wamechoka kwa kugawanywa katika matabaka!Nawaomba wana CDM msiwakatishe tamaa hawa kundi na 1 kwa kuhisi tuu kuwa wote wanafaidika na mfumo uliopo!Wengi wamekandamizwa sana kwa ubabe wa viongozi wanaoweza kuwajibishwa na serikali lakini serikali haifanyi hivyo!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Sawa, asante kwa ushauti mzuri. Ninaamiini kuwa na wewe umeanza kuutumia ushauri huu mzuri ingawa wahenga walisema mganga hajigangi (you are challenged to defy wahenga).

Ni imani yangu unajua ndani ya moyo wako kwamba nia ya kuingia hapa JF ilikuwa ni kusaidia kuzuia siasa hizi za matusi maana hazisaidii ustawi wa jamii yetu bali kubomoa. Leo hii mimi na wewe tungetumia muda kushauliana namna ya kwenda mbele si kupingana tu kwa sababu tunaimani tofauti. Kwa msukumo huu ndo maana natumia jina langu halisi...ningekuwa na nia tofauti na yangu basi hata nami ningejiita ZeMarcopolo-2 au Im-Hamza n.k. Au ningetumia muda wangu kujadili elimu yako, chuo ulipoipatia, kazi yako, unapoishi, ndugu zako, nikatundika picha zako za utoto nk, lakini sijafanya hivyo kwani si jambo jema...Mimi nilishadefy wahenga zamani sana...nafurahi you have accepted to take on the challenge.
 
Na kuna Kirusi, Kirusi andamizi na Mamuluki!

Kumekuwepo na shinikizo kubwa mitaani na zaidi kwenye mitandao ya kijamiii hasa facebook,Twitter,Blogs na hata huku JamiiForums kama mlivyoshuhudia la wafuasi wa Chadema na wapenda mageuzi wasio na vyama la kutaka Naibu katibu mkuu wa Chadema bara Zitto Zuberi Kabwe kujiuzulu nafasi yake.
Naungana na wote wanaomtaka ajiuzulu nafasi yake kama alivyopendekeza kwa lwakatare.Kitendo cha juzi kuja kulalamika humu kuhusiana na namba yake aliyokiri kwamba aliaacha kuitumia tangu mwaka jana mwezi july lakini bado ipo kwenye business card yake na kutaka pia kuaminisha umma kuwa taarifa ya Mabere Marando ina lengo la kumgeuza Dennis Msacky aliyemuita victim kuwa mtuhumiwa ni makosa makubwa yanayoweza kuvumilika
Inachosha kuona kiongozi kama huyu anashirikiana na wabaya wa chadema na kuwakingia kifua kwa gharama yoyote hata kuja huku kuwatetea na kurusha tuhuma kwa viongozi wa chama chake.
Kitendo alichofanya juzi kinathibitisha kuhusika kwake katika njama hizi na pia barua yake iliyodaiwa kuvuja aliyotuma kwa Katibu Mkuu wa Chama hicho na kurusha tuhuma ya moja kwa moja kwa ofisi ya katibu mkuu bila kufuata utaratibu wa vikao ni kuokosa umakini maana ni lazima watu wajiulize je Dr.Slaa angeibuka huku na kumjibu kama alivyofanya Ben Saanane alipojibizana nae kuhusu sakata la masalia ingekuaje?
Mwanzoni niliwashangaa sana vijana wa chadema walipokua wakimsema live kwewnye mitandao kuwa wamekosa imani naye na ni vyema angechukua uamuzi wa kujiuzulu na chama kifanye uchunguzi juu ya uhusika wake kwenye sakata hili.
Kwa kufanya hivyo atakua ame-Walk the talk kama ilivyotakiwa na mwanzisha mada mmoja huku siku chache zilizopita na pia zitto atakua amejipambambanua kwa kile alichokua akitaka kifanyike kwa Lwakatare kama kulikua hakuna ajenda ya siri na unafiki uliomsukuma kuandika barua kama ile

Inasikitisha kuona Chadema kilisimama nae kama timu alipotuhumiwa kuhongwa bungeni hata kamati yake ya ukaguzi wa hesabu za serikali kwenye mashirika ya umma ilipovunjwa CHADEMA kiliungana na kusimama nae bega kwa bega lakini anataka chama kimtose mkurugenzi wake aliyebambikiziwa kesi na maadui wa Chadema huku akijaribu kuwatetea baadhi ya wahusika wanaotumika na usalama wa taifa kukiangamiza chadema.

Mawasliano yake na dennis msaki kama yalivyoripotiwa na mwanahalisi yanatosha kuibua haja ya kufanyika uchunguzi wa kina juu ya uhusika wa zitto katika sakata hili pamoja na uvujishahji wa barua iliyowekwa huku nay eye kudai alifanya uchunguzi na kugundua aliyeweka humu ni yule aliyeweka video ya Lwakatare na pia kuna kirusi Chadema.
Zitto kama ni muumini wa kweli wa alichosema kama hakuna ajenda ya siri nyuma yake aaachie ngazi ili uchunguzi ufanyiuke juu yake na mienendo inayokatisha tama vijana na kujaribu kuleta mgawanyiko ndani ya chama na mtizamo wa jamii dhidi ya chama chake.Ajipime aone kama bado wanachadema wanayo imani kwake.Yeye mwenyewe ni shuhuda wa mijadala inayomtaka ajiuzulu iliyotawala sasa kwenye mitandao
 
Ni imani yangu unajua ndani ya moyo wako kwamba nia ya kuingia hapa JF ilikuwa ni kusaidia kuzuia siasa hizi za matusi maana hazisaidii ustawi wa jamii yetu bali kubomoa. Leo hii mimi na wewe tungetumia muda kushauliana namna ya kwenda mbele si kupingana tu kwa sababu tunaimani tofauti. Kwa msukumo huu ndo maana natumia jina langu halisi...ningekuwa na nia tofauti na yangu basi hata nami ningejiita ZeMarcopolo-2 au Im-Hamza n.k. Au ningetumia muda wangu kujadili elimu yako, chuo ulipoipatia, kazi yako, unapoishi, ndugu zako, nikatundika picha zako za utoto nk, lakini sijafanya hivyo kwani si jambo jema...Mimi nilishadefy wahenga zamani sana...nafurahi you have accepted to take on the challenge.

Thread yako ya kwanza kuianzisha hapa uliianzisha kwa lengo la kumtukana mwana JF mzalendo kuwa ni mgonjwa wa akili. Hilo halikuwa jambo sahihi na ndio maana ukakutana na counter force ambayo ilikushinda kwa nguvu.

Kwavile umegundua kuwa siasa za kuitana wagonjwa wa akili na matusi hazifai kiasi kwamba umekuwa mshauri mzuri kwa wengine, ninakubaliana na wewe asilimia 100 kuwa tulenge kupeana ushauri wenye manufaa kwa taifa.

Jitahidi pia kuwashauri vijana wa bavicha ambao ni vinara wa matusi, matusi yanachelewesha harakati za maendeleo...
 
Ungetaja siasa za majitaka zimechukua kasi CCM na Chadema.

Ungewaonya wote wa chadema na CCM. Siasa za maji taka hazipendezi. Hao wa Chadema wenye majitaka wajirekebishe, lakini Mwigulu Nchemba, Juliana Shonza, Nape Nnauye, Mtela Mwampamba nao pia wana midomo michafu, na mikakati ya majitaka wajirekebishe pia.

Lakini hata wewe nikikusoma between line, unajaribu ku-discredit watu wa CCM na kuacha watu wa CHADEMA.

Kama kweli unataka watu waache siasa za majitaka, kwa nini unataja hao watu wa CCM kwa majina na huku wengine wa CHADEMA bila hata kuwataja kwa majina wakati uzi huu uko mahususi kwa ajiri ya CHADEMA kama Title yake inavyobainisha.

Wataje na hao wa CHADEMA ili uonekane kweli mawazo na ujumbe wako uko balanced. Bila kufanya hivyo, tunaamini huu ni mwendelezo wa spinning za kisiasa against CCM
 
Last edited by a moderator:
Taja hao wanaoandamwa zaidi ya zitto
 
kama wewe mbeba mabox ...
k..wewe

Usitudharau wabeba mizigo dada,"kazi ni kazi mbaya kuiba!!!"tunajua nyinyi Wachaga munauwezouwezo,musidharau kazi za wengine,Chama chenu kifwata falsafa ya UBEPARI lkn tunaieshimu.
 
Thread yako ya kwanza kuianzisha hapa uliianzisha kwa lengo la kumtukana mwana JF mzalendo kuwa ni mgonjwa wa akili. Hilo halikuwa jambo sahihi na ndio maana ukakutana na counter force ambayo ilikushinda kwa nguvu.

Kwavile umegundua kuwa siasa za kuitana wagonjwa wa akili na matusi hazifai kiasi kwamba umekuwa mshauri mzuri kwa wengine, ninakubaliana na wewe asilimia 100 kuwa tulenge kupeana ushauri wenye manufaa kwa taifa.

Jitahidi pia kuwashauri vijana wa bavicha ambao ni vinara wa matusi, matusi yanachelewesha harakati za maendeleo...

Tutofautishe kutukana na kusema kesema ukweli unaouma, sikuja kumtukana mtu na si hulka yangu kutukana watu japo naweza. Nadhani kuguswa kwako na thread ile ni kwa sababu wana JF kwa njia moja au nyingine kwa muda sasa wamekuwa wanakuassociate na kukulinganisha na mlengwa wa ile thread. Ninyi ni watu tofauti sana kwa kila kitu, japo wewe hujatambua hilo kwa sababu haumfahamu na matokeo yake unabebana nae hata pale unapojua hayuko sahihi. Hukutaka hata kujiuliza ni kwa nini sikwenda pale kwake in person au nikampigia simu ama nikamu-email na badala yake nikaja hapa. To cut the story short sikuja hapa kushindana na yeyote na hivyo sikushindwa na mwanaJF yeyote. Nia yangu ilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa mlengwa in person and with confidence bila kujificha nyuma ya jina la kufikirika. na nilifanikiwa sana katika hilo na wewe unaweza kukubaliana nami kama ukiwa muungwana.

Nimekufuatilia sana hapa JF na nikaona wewe ni mchangiaji wa mada nyingi sana zenye kujenga na kubomoa na nimejiridhisha kwamba wewe ni muelimishaji na mpotoshaji at the same time. Kwa sababu sasa umenilazimu kukuzoom na kukufahamu fika wewe ni nani, ninakuja kwako na ombi langu binafsi.

"Naomba uchukue upande wako wa busara (si akili) na na ndo u-portray kwa jamii. Kutukana na kukashfu viongozi na wazee wetu for political gain (ambitions) si swala jema. Nchi yetu inatuhitaji wote as one" Tuijenge jamii iliyobora kwa kuonesha mfano, leo hii watu wanakimbia JF kisa kuna mtu anaitwa ZeMarcopolo anatukana sana.

Binafsi nitashukuru sana kama utaliona hili na kulipa uzito unaostahili, ukichagua kukosa heshima na kuipuuza heshima niliyokupa wewe na si ZeMarcopolo basi labda nifanye utaratibu wa watawala wetu, nije hapo ofisini kwako au nyumbani tunywe kahawa halafu nikuuliza vizuri kulikoni. Uwe na siku njema.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom