Ni kweli kuwa mimi nimefanya sana siasa za majitaka. Lakini ninatambua kuwa siasa safi hujenga nchi. Siasa za maji taka sikuzianzisha mimi, ila nimelazimika kuzifanya kwa sabau siasa za maji taka hazijibiwi kwa siasa safi.
Unakumbuka Hillary Clinton aliposema "shame on you Barack Obama" kule Ohio?
Kama vijana wa bavicha walioanzisha siasa za majitaka September 2010 watajirudi na kuendeleza siasa safi kwa maslahi ya taifa, zemarcopolo atakuwa na siasa safi kwa sababu siku zote zemarcoplo alikuwa na siasa safi mpaka alipogundua kuwa tuko kwenye dindwi la siasa za majitaka.
Kumuunga mkono Lusinde ni jambo moja, lakini kumkosoa inawezekana kama alivyofanya Filikunjombe leo.
Nauliza tu iwapo na wanaofanya siasa za majitaka upande wa pili umewakemea?
CCM walipoanza propaganda za udini tangu enzi za CUF mbona hukukemea?
Mbona hukukemea pale Salim alipochafuliwa kuwa anahusika na kumuua Karume?
Hapo ndipo napata shida kama kweli unazichukia siasa hizo za majitaka au unachukia watu ndani ya Chadema, maana umejionyesha wazi majitaka yako kwa Chadema ni kwa baadhi ya wana Chadema (Zitto humgusi)!
You need not go so low!
Nimejiunga 2012 lakini ni mfuatiliaji mzuri sana humu hata kabla sijajiunga.Kama umenifuatilia vizuri nadhani utakuwa umenotice vitu viwili 1) Sijadili mada za udini. 2) Sijadili wanaotajwa kugombea Urais ndani ya CCM.
Kila kitu kina sababu yake.
Hapo naona umejiunga mwaka 2012. Sijajua kama hapo ndio mara yako ya kwanza kuifahamu JF au ulikuwa unasoma mada za JF kabla ya hapo, lakini nikupe tu historia kwa kifupi. Around september 2010 waliibuka vijana wa bavicha in huge numbers (tuliamini vijana wengi walikuwa na multiple IDs). Vijana hawa likiandikwa jambo lolote ambalo linahoji chadema basi wanajibu ----. Thread moja unaweza kukuta posts kama 20 mfululizo zimeandikwa ---- na kejeli mbalimbali. Jambo hili lilisababisha waumiaji wengi wastaarabu wa JF kujiweka pembeni. Kuna watu kama Rev. Kishoka (Mzee wa TPP Maendeleo) alikuwa mtu fresh sana kwenye mijadala. Ila tangukipindi hicho amekuwa very passive.
Halafu mijadala ilikuwa spontaneous, mtu anatoa mchango kutokana na thread. Siku hizi ukiona mtu amechangia unaweza kuhisi alichoandika kwa kusoma jina lake tu. Michango sio spontaneous.
Chadema ina kitengo maalum cha mitandao ya jamii ambacho ndicho kinachoratibu tabia hii. Wakiambiwa waache itakuwa vizuri kwa sababu wengi tunapenda siasa safi kwa kutambua kuwa siasa safi hujenga nchi.
Nimejiunga 2012 lakini ni mfuatiliaji mzuri sana humu hata kabla sijajiunga.
Niliona kuna watu walikuwemo humu akina Rejao, Ritz, chama, Faizafox, malariasugu, zomba n.k ambao nao walikuwa wanafanya mchezo huo huo kwa upande wa CCM.
Nadhani wewe, ambaye ni kati ya wana JF ambao nawakubali hapa JF, ulikubali kujiingiza kwenye kundi ambalo halikufai. (Naheshimu uamuzi wako, na wala silazimishi ubadilike)
Wewe, kama walivyo akina Mchambuzi, Mzee Mwanakijiji, n.k. ndio great thinkers ambao tukiona majina yenu kwenye post tunajua tunajifunza kitu. Sasa kwa nini ushuke chini namna hiyo? MKJJ na mchambuzi wamekwepa kishawishi hicho.
Lakini pia siasa za majitaka hazikuanzia hapa JF. Zilianzishwa na CCM tangu wakati wa CUF, tumeambiwa CUF ugaidi, CUF udini mbona sasa wamewanyamazia hao wadini na magaidi? Walibadilika lini?
Huwezi kusafisha system chafu kwa kuamua kuwa mchafu pia.
Haya mkuu.Kama uko fair utakubali kuwa vijana wa bavicha ndio walioharibu hii JF.
Kuna njia nyingi za kutatua tatizo. Tunapokuja kwenye kujadiliana ni lazima kuwa tayari kusikia options mbalimbali na tizishindanishe kwa hoja. Mwisho hoja yenye uzito itashinda au pengine mjadala unaweza kuisha kwa kukubaliana kutokukubaliana kwenye jambo husika.
Tatizo ni pale vijana wa bavicha wanapotanguliza matusi badala ya hoja.
Mimi nimefanya siasa za majitaka, lakini sijawahi kumtukana mtu. Ninafanya siasa za majitaka kwa style ambayo hata Hillary Clinton alifanya, Barack Obama alifanya na ina wakati wake na lengo lake.
Kama uko fair utakubali kuwa vijana wa bavicha ndio walioharibu hii JF.
Kuna njia nyingi za kutatua tatizo. Tunapokuja kwenye kujadiliana ni lazima kuwa tayari kusikia options mbalimbali na tizishindanishe kwa hoja. Mwisho hoja yenye uzito itashinda au pengine mjadala unaweza kuisha kwa kukubaliana kutokukubaliana kwenye jambo husika.
Tatizo ni pale vijana wa bavicha wanapotanguliza matusi badala ya hoja.
Mimi nimefanya siasa za majitaka, lakini sijawahi kumtukana mtu. Ninafanya siasa za majitaka kwa style ambayo hata Hillary Clinton alifanya, Barack Obama alifanya na ina wakati wake, mahala pake na lengo lake.
Vijana wa bavicha wao kila mada wanarusha matusi tu, kila jukwaa matusi na kejeli. Hatupaswi kwenda hivyo, tunachelewesha maendeleo...
Siasa za majitaka zimeanza kuchukua kasi CHADEMA baadhi ya viongozi wanaitwa masalia wakati ni viongozi wa juu wa chama this is bad either we fire or w retain naogopa kuna watu wanatumika kudisqualify baadhi ya viongozi kwa kuwaita wasaliti na wengine waonekane wanajengeka chama nyumba moja kugombania fito kwanini.
Nafurahi sana kusikia kwamba hujawahi kumtukana mtu. Na kama huo ndo ukweli wako ni vyema ukawa kioo cha jamii kwa kuonesha mfano bora kwa vijana hawa wa bavicha...Kama umeshagundua siasa za maji taka zinachelewesha maendeleo, basi iwe wajibu wako kuzikemea na sikuziongezea moto. Saidia kubadilisha utamaduni wa matusi kwa kutotoa matusi hata pale unapojihisi unaulazimika, jizuie. Kwa kufanya hivyo utachangia sana maendeleo ya jamii yako na ustawi wa JF
Wanachojaribu kumfanyia Zitto ni ujinga tu na atawashinda tuNa kuna Kirusi, Kirusi andamizi na Mamuluki!
Ukiwa mtaani hasa maeneo ya mijini ni dadra sana kusikia mtu anaisifia CCM, wapo watu wanapenda CCM iendelee kuwa madarakani ingawa watu hao huwa hawasemi wazi. Unaweza ukawaona kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia Nick names.
Zifuatazo ni sababu zinazofanya baadhi ya Watanzania kulilia CCM ibaki madarakani pamoja na umasikini, ufisadi uliokithiri kufikia hatua ya kushika nafasi ya pili kwa ufisadi Afrika mashariki, point moja tu baada ya uganda.
1. Watu hao kwa sasa wananufaika na mfumo wa sasa, kwani ni mfumo ambao uko loose,kundi hili ni waajiriwa serikalini. Wafanyakazi wa Serikali wamefanikiwa kuvuna pesa za wizi serikalini wanaomba hali iendelee kuwa kama ilivyo, CCM iendelee kutawala .
Wengi wetu tunawafahamu rafiki zetu walioko serikalini bila kujali kuwa wana nafasi za juu au za chini wamefanikiwa kutajirika ghafla, tunawafahamu lakini hakuna mahali pa kuripot kwakuwa system nzima ni Corrupt.
2. Wako wafanyabiashara wanaokwepa kodi, serikali imegubikwa na rushwa kwa hiyo hawawezi kukusanya kodi, kila kitu kinakwenda kwa dili au ten %. Hawa nao wanasema kidumu chama cha mapinduzi
3. Wako ambao wamezaliwa kwenye familia tajiri, wakiamka asubuhi wanajiuliza ama wale soseji au mayai. Friji zao Zimejaa kuku, samaki nk. Pia wanachagua watoke na aina gani ya gari. Kundi hili halifahamu vizuri umasikini uliowagubika watanzania, shida wanazisikia kwenye vyombo vya habari, maisha yao hawajichanganyi na masikini kabisa, wanasoma shule na vyuo vya kitajiri kwa hiyo umasikini hawaujui. Kwa hiyo hawaoni kosa la CCM
4. Masikini lakini wanaipenda CCM mpaka kesho. Kundi hili liko vijijini. Linaipenda CCM kwa sababu ya kukosa elimu ya uraia, au hawapati habari kabisa. Shughuli yao kubwa ni kulinda nyani wasivamie mashamba yao. Kundi hili halijui maana ya maendeleo, wanatamani hata shule zisiwepo ili watoto wachunge ngombe na kulima, wakivuna mazao ya kutosha wakala wakashiba hata kama hawana shilingi ya kununua ndala wao usema CCM oyeeeee
5. Kuna kundi ambalo lenyewe limedanganywa kwa uvumi au kwa mazoea tu. Kwamba bila CCM kutakuwa na vita, linasema CCM imenilea hadi hapa nilipo. Kundi ili liko tayari kuchagua hata fisadi au jiwe ilimradi tu atokee CCM. Kundi hili linafahamu kabisa kuwa serikali haifanyi vizuri lakini kwa mazoea lenyewe limeendelea kuomba CCM ibaki madarakani ili amani iendelee kuwepo.
6. Imani. Kundi hili ni mchanganyiko wa wasomi na wasiosoma. Hawa kwa sababu ya imani kali kwa dini limehamua kuweka dini mbele lakini maendeleo baadae. Kundi hili linafahamu kabisa madudu ya CCM lakini limeendelea kuwa na msimamo kwa CCM. Kundi hili udanganywa kirahisi kwa propaganda za CCM kwamba Chama fulani ni cha dini fulani. Bila kujali msitakhabali wa nchi uamua kushabikia CCM lakini baada ya miaka mitano huwa halioni mabadiliko ya kmaendeleo. Kundi hili ndilo linalochelewesha mapinduzi ya nchi, kundi hili ukesha likiomba CCM iweke mtu wa dini yake bila kujali uwezo wa kiongozi husika.
7. Mafisadi papa. Hili ni kundi ambalo ni chafu kabisa, halina hata dini. Limeiba pesa nyingi za Watanzania bila kujali kuwa kila siku kuna masikini wanakufa kwa kukosa dawa mahosipitalini. Kundi hili kwa kutumia nguvu ya pesa za wizi linatamani ligawie kila mtanzani laki moja ili wapigie kura CCM. Kundi hili linahitaji CCM idumu ili lipate security ya mali zake, liko tayari hata kuua au kung'oa mtu kucha anaehatarisha CCM kuanguka. Linahofu kuwa chama kingine kikiingia madarakani litafilisiwa na kupelekwa mahakamani. Ni kundi lenye nguvu kubwa hata sasa ndani ya CCM
Sawa, asante kwa ushauti mzuri. Ninaamiini kuwa na wewe umeanza kuutumia ushauri huu mzuri ingawa wahenga walisema mganga hajigangi (you are challenged to defy wahenga).
Na kuna Kirusi, Kirusi andamizi na Mamuluki!
Ni imani yangu unajua ndani ya moyo wako kwamba nia ya kuingia hapa JF ilikuwa ni kusaidia kuzuia siasa hizi za matusi maana hazisaidii ustawi wa jamii yetu bali kubomoa. Leo hii mimi na wewe tungetumia muda kushauliana namna ya kwenda mbele si kupingana tu kwa sababu tunaimani tofauti. Kwa msukumo huu ndo maana natumia jina langu halisi...ningekuwa na nia tofauti na yangu basi hata nami ningejiita ZeMarcopolo-2 au Im-Hamza n.k. Au ningetumia muda wangu kujadili elimu yako, chuo ulipoipatia, kazi yako, unapoishi, ndugu zako, nikatundika picha zako za utoto nk, lakini sijafanya hivyo kwani si jambo jema...Mimi nilishadefy wahenga zamani sana...nafurahi you have accepted to take on the challenge.
Ungetaja siasa za majitaka zimechukua kasi CCM na Chadema.
Ungewaonya wote wa chadema na CCM. Siasa za maji taka hazipendezi. Hao wa Chadema wenye majitaka wajirekebishe, lakini Mwigulu Nchemba, Juliana Shonza, Nape Nnauye, Mtela Mwampamba nao pia wana midomo michafu, na mikakati ya majitaka wajirekebishe pia.
kama wewe mbeba mabox ...
k..wewe
Siasa safi hujenga nchi...
Thread yako ya kwanza kuianzisha hapa uliianzisha kwa lengo la kumtukana mwana JF mzalendo kuwa ni mgonjwa wa akili. Hilo halikuwa jambo sahihi na ndio maana ukakutana na counter force ambayo ilikushinda kwa nguvu.
Kwavile umegundua kuwa siasa za kuitana wagonjwa wa akili na matusi hazifai kiasi kwamba umekuwa mshauri mzuri kwa wengine, ninakubaliana na wewe asilimia 100 kuwa tulenge kupeana ushauri wenye manufaa kwa taifa.
Jitahidi pia kuwashauri vijana wa bavicha ambao ni vinara wa matusi, matusi yanachelewesha harakati za maendeleo...