fered mbataa
JF-Expert Member
- Feb 19, 2012
- 240
- 35
binafsi huwa nawashangaa sana viongozi wetu waliokaa kisiasa zaidi na ndomaana maendeleo yapo polepole sana. Leo nilikuwa naangalia taarifa ya habari ya star tv, nape nauye msemaji wa ccm anaelezea habari ya ushindi wao wa uchaguzi mdogo,nilimshangaa sana alipo leta kejeli za uchaguzi kwenye habari muhimu ya maendeleo ya chama. Alianza kumpondea dr slaa et babu amezeeka awapishe vijana waongoze chama yeye anapeleka chama kubaya baada ya kushindwa na ccm katika chaguzi ndogo za udiwani. kwanza kauli aliyoisema haijapita kwenye mfumo wa akili ili ipimwe. Then hakukuwa na aja ya kueleza habari za chadema kwenye maendeleo ya ccm.binafsi naona hawa viongozi wetu wanalala wanawaza kampeni, wanaamka wanawaza kampeni,waongoza serikali wanawaza kampeni, wanafungua miradi imekaa kisiasa,waongoza ofisi mbalimbali huku wanapiga kampeni. Mwisho wake ni nini?, jamani mbona viongozi wanawaza uchaguzi tu wa 2015 je wanania kweli ya kuongoza taifa au wachume tu?sion mi umuhimu wa kampeni sasa wakati mtu unajukumu la kiuongoz amepewa na wananchi, nalisema hili sababu kesho bunge linaanza noambeni msikilize kauli zao muone ni za maendeleo au kampeni, ni mda mwingine wa kampeni za siasa kwenye chombo cha kuleta maendeleo.hatuigi mazuri ya nchi zilizoendelea na badala yake mabaya tu, mda wa kazi ni kazi na siasa ni siasa.subiri usikie hasa ili la treni ya mwakiembe.