Siasa za kizamani,Bunge na gharama za Uendeshaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za kizamani,Bunge na gharama za Uendeshaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbunge, Jun 28, 2011.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LAITI mikoa ingekuwa na mabunge ya mikoa basi bunge la JMT lingehitaji tu kukutana mara nne kwa mwaka katika vipindi vya juma moja kila kikao.Kikao cha kwanza kingelihusu kupitia maamuzi ya mabunge ya mikoa na kuyabariki; kikao cha pili kingelihusu kupitisha miswaada mbalimbali; kikao cha tatu kingelikuwa juu ya mahiraji ya msingi ya wananchi, ulinzi na usalama; na kile cha nne kingelikuwa cha mapitio ya bajeti za mikoa na bajeti ya kitaifa.Mabunge ya mikoa yangelikutana nayo kwa vipindi vifupi vya siku 3-4 mara nne kwa mwaka kwa utaratibu wa kuzungumzia maazimio na taarifa za maeneo-bungekimkoa; kupitisha miswaada mbalim bali; kikao cha tatu tathmini ya mafanikio katika kuundoa mkoa toka kwenye umaskini na hatimaye kuzungumzia, kurekebisha na kupitisha bajeti ya mkoa na maeneo husika. Hivi leo kuwa na bunge linalokaa miezi 3 kujadili bajeti ya maeneo ambayo watu hawayajui, hayawahusu wala hawana habari nayo kunaonesha jinsi ambavyo hatuendani na teknolojia wala wakati.Bajeti nzima sasa hivi inatakiwa iwe ni zana iliyomo katika laputopu ya kila mbunge. Atakabonyeza kitufe chochote kwenye bajeti hiyo maelezo yote yanatiririka kiouto na akitaka maelezo zaidi anwani zote pepe zinakuwepo hapo ikiwezekana kwa kutumia teknolojia ya mesenja 'messenger' .Badala ya Waziri wa Fedha kukaa ofisini kwake na watu wake na kuandika bajeti dakika za mwisho kabla ya kikao cha bajeti kwa kuwa bajeti hiyo iko kwenye laputopu ya mbunge ni rahisi kuunganishwa naye akachangia lolote alilokuwa nalo huko huko aliko bila kupoteza bure fedha za walipa kodi baada ya hapo.Tatizo hili linakuzwa na kuwa na lundo la mawizara ambayo hayana maana wala hayahitajiki ila tu kwa sababu kuna mtu aanamini hawezi kufanya kazi bila mawaziri hao. Lakini ukweli ni kuwa kama huwezi basi huwezi tu na wala siyo idadi ya wasaidizi itakayokuwezesha kuweza usichokiweza.Nina hakika serikali huru za mikoa zikiwepo basi serikali kuu haitahitaji zaidi ya mawaziri 14 tu. Na siku 14 zitatosha kabisa kuzungumzia bajeti ya serikali na hivyo kuokoa gharama za miezi miwili na nusu.KWA kuwa serikali na wabunge wetu wameshindwa kutupunguzia umasikini wakati umefika wa kuwaambia jamani mlichokuwa mnakula na kazi mmeshindwa ni kikubwa mno. Tunakipunguza kwa kiasi tutakachokubaliana katika kikao cha pamoja. Watanzania mnawabebesha zigo wasiloweza kulibeba, la sivyo tutawalemaza kabisa!
   
 2. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hilo nalo nenoooo.
   
Loading...