Siasa za kitoto

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,809
2,000


SIASA ZA KITOTO
1)Zimepitwa na wakati,syasa za kutukanana
zinapoteza bahati,siasa za kulumbana
zatuweka hati hati,siasa za kugombana
hizi syasa za kitoto,ni lini mtaziacha
2)Mitandaoni mwasema,hata yaso na maana
wengine wakata pema,kisa wameshatengana
Tanzania ndio mama,ya nini kuchukiana
hizi syasa za kitoto,ni lini mtaziacha.
3)Zimeanza kutuchosha,siyo leo tanga jana
mtu akijidondosha,ya nini kuchukiana
siasa za kujiosha,landa zitawapa jina
hizi syasa za kitoto,ni lini mtaziacha
4)Bora mseme mapema,kabla hamjaachana
siyo mlete hujuma,talaka mkipeana
mwaanza jiuma uma,vidole kuonyesha
hizi syasa za kitoto,ni lini mtaziacha
5)Eti jamaa ni mwizi,jana hamkumuona
mngemuita jambazi,ama mnafichiana
labda mnavunja nazi,nahisi mnalogana
hizi syasa za kitoto,ni lini mtaziacha
6)Mmekuwa ni majoka,kisiri mnan'gatana
walojaribu ropoka,tayari walitekana
maajabu mnacheka,kumbe mnajitekenya
hizi syasa za kitoto,ni lini mtaziacha.
SHAIRI-SIASA ZA KITOTO.
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom