Siasa za HESLB zinawalaza njaa wanachuo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za HESLB zinawalaza njaa wanachuo!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Ashoboza Kabalim, Feb 22, 2012.

 1. A

  Ashoboza Kabalim Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ikiwa ni zaidi ya mwezi sasa zitoke tetesi kwa wanachuo kuletewa fedha za kujikimu, watendaji ndani ya bodi hiyo wamekuwa wakifanya mawasiliano yasiyo rasmi na wasomi hao kuwa fedha zimekwishatumwa vyuoni hivyo 'waukomalie' uongozi wa vyuo hivyo ili kupata fedha zao! Hii imeleta imani kuwa fedha hizo huwa zinatumwa vyuoni nakuwekwa kwenye 'fixed' account ili uongozi wa vyuo hivyo upate faida ya 'fasta fasta'.
  Hata hivyo, uongozi wa vyuo hivyo unakiri kuwapo kwa uchonganishi huo usio rasmi kati yake na wanachuo kutokana na ukweli kwamba fedha zilizotumwa ni kwa ajili ya ada (tuition fee) na si fedha ya kujikimu. Mkanganyiko huu unazidi kuwaweka katika hali mbaya ya kiuchumi wasomi hawa, wengi wao wakipiga 'dash' (kushinda njaa) kutokana na kucheleweshwa kwa fedha hizo.
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Kuna mijitu itakuja hapa kukwambia tabu hiyo yote inasababishwa na Ukristo. We subiri uone
   
 3. A

  Ashoboza Kabalim Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Teh teh teh teh! Siasa za dini hadi kwenye utumishi wa umma, kuna haja ya nchi hii kujivua gamba!
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Ndoa zitaanza kuvunjika sasa hivi..time will tell
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nyie nao njaa imewazidi duh! Kwa nini msisubili mpaka chuo kifunguliwe?
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Absolutely correct!
   
 7. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ukristo? Huko nikufikiri kimasaburi!
   
 8. A

  Ashoboza Kabalim Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vyuo vingine vimeshafunguliwa 2nd semister karibu wiki ya 3. e.g. SAUT
   
 9. M

  MYISANZU Senior Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UDSM mpaka litokee kunji [ mgomo] ndio pataeleweka!
   
 10. Mfarisayomtata

  Mfarisayomtata JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 417
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Watagoma hadi tatoto wa chekechea ila si SAUT, hapa mapimbi wamejaa. UDSM, UDOM, TUMAINI, jamani rudini vyuoni mtuokoe wenzenu hatuna pa kusemea.
   
 11. N

  NIMIMI Senior Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nyie mwalilia kucheleweshewa bumu ikiwa tulio wengi hatufahamu hilo bumu, na chakushangaza wanaUDSM pindi wanaandamana kutetea 'usawa' hasa kwa walikosa mikopo na Kuandikiwa 'NO LOAN' Wengi mlitucheka na vijembe vingi, pamoja na kauli ambazo zingestahiki kutolewa na watoto wa chekechea 'ati Wahuni' hao.

  Kuna wenzetu wapatao 98 hadi sasa hawajui hatma ya maisha kwani walifukuzwa na tunaumia sana mioyoni wanaUDSM Juu ya wenzetu kwasababu ya kutetea haki na Usawa kwa mtoto wa kitanzania wa mkulima yaani kupatiwa mikopo wote angalau hata fedha za kujikimu. Lakini mkatuona wahuni.

  Emeka aliwahi kusema katika utetezi wake kwamba Swala la mikopo kwa vyuo vya Tanzania ni 'JANGA LA KITAIFA' kwasababu mlio wengi mlikua nazo MIFUKONI na mkitembea huku mikono mmetia mifukoni mwenu mkizilinda 'leo zimekwisha' mkisubiria watumwa na kutolewa kafara wenu wanaUDSM wakusaidieni, thubutuuu

  kwataarifa yenu hata pale Udsm saivi ukisikika unahamasisha wenzako waamuke kutetea haki zao kwa usemi wetu wa mshikamano 'REVOLUTION....... For changes....., sOLIDARITY..... FOREVER....... Kwanza wasomi wote wanakuacha peke yako na huna muda mrefu jina linatoka unatakiwa Auxiliary police kuna ujumbe wako muhimu unaondoka kwenu, hivyo imefika mahali tunataka iwe zamu yenu katika Vyuo vingine muamuke na mjitetee na kuwatetea wengine kama Udsm ilivyokuwa ikiwafanyia. Kwanini Udsm tu msiwe nyie 'dont be CHICHIDODO, HATES FEACES BUT FEEDS ON MAGGOTS'

  hata sisi safari hii hakuna 'kunji' hata bumu likikosekana, hata na hivyo hatuna mikopo kabisa nyie mmekopeshwa pesa zimechelewesha mnalalama hadi makoo yanakauka subirini 'HAKI ZENU MLETEWE KWENYE VISOSI SAWA EHEE' wenzenu tumepoteza wanafunzi na kila siku tunahangaika warudishwe Vyuoni 'nyie mlinyamaza kimya na tuli kama maji mtunguni' Leo inakuja akilini eti Udsm tufungue chuo kwaajili ya kuwapigania haki zenu nyie, ingieni barabarani mpigane vyema na muondokewe na wanafunzi mpate machungu tuende sawa ndipo tuungane pamoja kuwapigania warudishwe vyuoni.

  Maisha kote ni KiZUNGUMKUTI Na Bora kidogo ulichonacho hata kikicheleweshwa kitakuja kuliko Asiyekuwa nacho na hategemei Kupata. Tembo hashindwi na Pembe zake tuamke!
   
 12. G

  Georeez Member

  #12
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kamanda wangu mi nimeheshimu mawazo yako...!ktka vingi nilivyowah kuvikuta kwenye hii forum hili nimelipenda mi co mwana Udsm bt nakussupport 110%.acha na hao wanaojifanya hawajui kugoma washinde njaa 2one mwisho wake!
   
Loading...