Siasa za CHADEMA kama za CCM


njaa yako sasa inakuondolea utu wako.
 
njaa yako sasa inakuondolea utu wako.
Njaa yangu kubwa ni kuona mabadilko ya kweli. kama CCM wakizomewa kwa kufanya madudu tunashangilia, nataka na CHADEMA wakifanya madudu nao pia wazomewe! Kama ni njaa ya tumbo tu mzee nakula na kusaza, kwa hilo mungu wangu wa mbinguni ahimidiwe!
 
Njaa yangu kubwa ni kuona mabadilko ya kweli. kama CCM wakizomewa kwa kufanya madudu tunashangilia, nataka na CHADEMA wakifanya madudu nao pia wazomewe! Kama ni njaa ya tumbo tu mzee nakula na kusaza, kwa hilo mungu wangu wa mbinguni ahimidiwe!

chadema haihitaji ushauri wa kipuuzi kama huu.Wewe ni Magamba na ndio maana unajaribu kupima upepo hapa jamvini.Hakuna mpigania haki mwenye mawazo mfu kama haya.Mbona huwashauri washirika wenu Cuf ambao viongozi wake robo tatu ni wapemba?
 
cdm magwanda,ccm magamba.hivyo vua gamba vaa gwanda!kuna tofauti kubwa sana kati siasa za kukumbatia mafisadi,makundi na proopaganda zinafanywa na ccm,dm harakati zidi kupinga unyonge,umaskini,ufisadfi,ukkiukwakaji wa hakiza binadamu na upuuzi mwingine unaoufahamu.ccm akili zenu na upeo wenun sawa cuf,afp,chausta,updp,na ncccr.hamna mabacho mn chokifanya ambacho kinaweza kuwafananisha na chadema na serikali yenu inao wabagua watoto wa maskini ktk elimu kama mikopo,
 

Ninachokataa ni ile falsafa ya kiyahudi kwamba "neno jema haliwezi kutoka Samaria". Kupagawa kwenu na imani ya kile mnachokiamini kwamba ndiyo sheria na Kanuni (world order) ya kimaumbile ya ulimwengu ndiko ninakokupinga. Nakumbuka zogo lililotokea wakati Zitto alipotaka kugombea uenyekiti wa taifa.

Kila mtu aliaminishwa kwamba Zitto katumwa na Rostam Aziz kugombea ili aisambaratishe CHADEMA. Hivi kila mtu mwenye mawazo tofauti na nyie ni lazima awe ni mwanachama wa CCM au katumwa na mafisadi? Ina maana demokrasia ya CDM ni kukubali kila kitu bila ya kutafakari au kuwa na mawazo mbadala?
 
chadema haihitaji ushauri wa kipuuzi kama huu.Wewe ni Magamba na ndio maana unajaribu kupima upepo hapa jamvini.Hakuna mpigania haki mwenye mawazo mfu kama haya.Mbona huwashauri washirika wenu Cuf ambao viongozi wake robo tatu ni wapemba?
Kwa hiyo "Upemba' wa CUF ni hatari bali 'undugu' wa CHADEMA ni ukamanda!!
 
Kwa hiyo "Upemba' wa CUF ni hatari bali 'undugu' wa CHADEMA ni ukamanda!!

wewe umesema upemba wa Cuf ni hatari.Mimi sijasema.Ninachoweza kukushauri mind your Magamba party business.Thats it!
 
wewe umesema upemba wa Cuf ni hatari.Mimi sijasema.Ninachoweza kukushauri mind your Magamba party business.Thats it!
Tafsiri ya maneno yako ndivyo yanavyoonyesha kwamba upemba wa CUF ni hatari. Kwa taarifa yako chama cha siasa ni Public Property hakina mwenyewe ndiyo maana hakuna kufunga milango ya kujiunga wala masharti ya kibaguzi. CHADEMA ni Public property wanachama na wasio wanachama wana haki ya kukikosoa.

Mimi si mwana CCM lakini naongozwa na CCM. Kwa hiyo CCM wakikataa kukosolewa na mimi utakuwa ni ujinga wao na CDM kwa sababu wanataka kuniongoza ni lazima niwakosoe kwa aina nipendayo. Vyama vya siasa ni watumishi wa Umma na ni umma ndiyo wenye haki ya kivikosoa vyama vya siasa na vyama vya siasa havina haki ya kuukosoa Umma.
 

Huelewi nini? Anasikitishwa na dynasty iliyoko huko CDM ambayo haina tofauti na ile ya CCM tunayoitolea mimacho na kutoka mapovu tunapoijadili. Sasa unaomba ushahidi gani zaidi wakati umeambiwa kila kitu:

1. Dr. Slaa /Rose Kamili
2. Ndesamburo/Lucy Owenya/Grace Kiwelu
3. Tundu Lissu/Christina Lissu
4. Zito Kabwe/Muhonga Ruhwanya
5. Anna Komu/Anthony Komu (siyo mke na mume)
6. Edwin Mtei/Freeman Mbowe
 
kwenye red highlight nadhani panajieleza panyewe. Ila ninavyojua kwa chadema hamna tofauti na ccm. Na ndo maana hata juzi na wao walikuwa wakiiba kura kule igunga. kwani zilikutwa kura nyingi zimetikiwa kwa mgombea wa chadema.
chadema na ccm wote ni many'ang'au, ila kwa viwango tofauti. ila hiki kiny'ang'au kidogo kinakua kwa kasi ya ajabu, du! muda si mrefu kitakuwa linyany'ang'au likubwa kama hili la zamani. EWE MUNGU TUEPUSHIE MBALI NA MANY'ANG'AU HAYA. AMEEN!
 

ni kweli ukosoaji unaruhusiwa lakini si kwa unafiki kama ufanyavyo.Wewe unaleta ubaguzi wa kikabila kwa maslahi ya chama chako Magamba.Unataka kusema ndugu yako akiwa mwanachama na kiongozi basi huruhusiwi kushiriki harakati eti itaonekana undugu? Mnafiki ni aheri ya mchawi.Mlitumia uongo huu mwaka jana Watanzania wakawajibu kwa kuiongezea chadema wabunge kutoka 5 hadi 48.Igunga mkatumia propaganda hizohizo wanaIgunga wakawajibu kwa kuwapa kura chadema kutoka kura sifuri hadi elf 23.Hamchoki tu? Tafuteni propaganda nyingine hii imeshindwa.
 
chadema haihitaji ushauri wa kipuuzi kama huu.Wewe ni Magamba na ndio maana unajaribu kupima upepo hapa jamvini.Hakuna mpigania haki mwenye mawazo mfu kama haya.Mbona huwashauri washirika wenu ("Cuf ambao viongozi wake robo tatu ni wapemba")?
kama CDM tu viongozi wake robo tatu ni Wachagga
 
Mtoto wa kiume sio vizuri kumsifia mwanaume mwezengu! Unatupa wasiwasi kama uwa anakupa pesa sisi hatufahamu

mwambie kazi unayofanya hapa ni kubwa akupe walau buku 3 kwa siku
 
ni kweli ukosoaji unaruhusiwa lakini si kwa unafiki kama ufanyavyo.

Sielewi ni kwa nini unafikiri ukosoaji wangu ni wa kinafiki wakati kila kitu nimeweka adharani.

Wewe unaleta ubaguzi wa kikabila kwa maslahi ya chama chako Magamba.

Kama utaonyesha kwenye post yoyote nimetaja kabila lolote basi nihukumu,lakini kama utashindwa kuonyesha basi wewe ni MZUSHI

Unataka kusema ndugu yako akiwa mwanachama na kiongozi basi huruhusiwi kushiriki harakati eti itaonekana undugu?
Sijakataa kuwa ndugu yako akiwa mwanasiasa na wewe usiwe mwanasiasa. Julius alikuwa mwanasiasa na Joseph Nyerere naye alikuwa ni mwanasiasa. sioni tatizo katika hilo. Hoja yangu ni kwani nini hayo yakitokea CCM inakuwa ni nongwa kwa CDM ni baraka?

Mnafiki ni aheri ya mchawi.
Hata mimi nakusihi wewe usiwe mnafiki kwani hata dini zinakataa wanafiki.

Mlitumia uongo huu mwaka jana Watanzania wakawajibu kwa kuiongezea chadema wabunge kutoka 5 hadi 48.
idadi siyo ubora na sababu za kupatikana kwa wabunge hutofautiana kati ya Jimbo na Jimbo na na sehemu na sehemu.

Igunga mkatumia propaganda hizohizo wanaIgunga wakawajibu kwa kuwapa kura chadema kutoka kura sifuri hadi elf 23.Hamchoki tu? Tafuteni propaganda nyingine hii imeshindwa.
Wanaigunga tangu mwaka jana walishaikataa CCM na ndiyo maana walimpa Mgombea wa CUF Mahona Kura 11,000 bila ya nguvu kubwa kutumika. Kwa hiyo mwaka huu watu wengi zaidi wamefikiwa na nguvu kubwa zaidi ikatumika kwa pamoja CDM na CUF wameongeza kura 15,000 kutoka zile 11.000 za awali. Wana Igunga walishaikataa CCM hata kama CDM wasingeenda wangewachagua vyama vingine na si CCM.
 

nina swali moja kwako kwanini wanaIgunga hawakuwapa kura hao wasio na undugu katika uongozi kama chadema kwa madai yako? Kwanini kura za cuf ziporomoke ziende chadema? Kwanini wasichague vyama vingine vya upinzani kama SAU,DP,UPDP au Chausta? Kwa nini wakipe kura chadema ilihali wewe unakituhumu ni chama cha kibaguzi? Kama wewe si mnafiki nipe majibu.
 
Kwanza nashukuru ndugu yangu kwamba tumetoka kubishana hadi sasa kujadiliana, hayo ndiyo mabadiliko ya kweli na Uhuru wa Kweli ambao CHADEMA inaupigania.
nina swali moja kwako kwanini wanaIgunga hawakuwapa kura hao wasio na undugu katika uongozi kama chadema kwa madai yako?
Igunga hoja kubwa ilikuwa kama Igunga ni maskini au si maskini na kama ni maskini ni nani kausababisha huo umaskini. Kwa hoja hii CDM walishinda kwani wananchi wenyewe wa Igunga wanajua umaskini wao. Pia Igunga walikuwa hawawachagui hao niliowaorodhesha bali walikuwa wanataka kuchagua Kashindye mwana Igunga mwenzao na mwalimu maarufu anayefahamika na wengi.

CUF hawakuchaguliwa kwa sababu wenyewe waliwekeza kidogo kwenye upelekaji wa ujumbe wao kwa wananchi hadi wakashindwa kujitofautisha wao na CCM ambao wananchi wa Igunga walishaamini ndiyo wezi wa rasirimali zao na ndiyo waliosababisha wao wawe maskini.

Kwanini kura za cuf ziporomoke ziende chadema?
Hakuna anayejua kwenye suala la kura ni za nani zilikwenda CDM. Kwa nini usifikiri kwamba za CUF zilikwenda CCM na CDM wao walichota za CCM?
Kura za CUF zilipungua kwa sababu walikuwa hawana hoja mahsusis inayokubalika kwa wananchi. Halafu kumbuka ndoa ya CCM na CUF ni mzigo unaowatesa CUF huku Tanzania Bara.

Kwanini wasichague vyama vingine vya upinzani kama SAU,DP,UPDP au Chausta? Kwa nini wakipe kura chadema ilihali wewe unakituhumu ni chama cha kibaguzi? Kama wewe si mnafiki nipe majibu.

Hivi vyama vyote ulivyovitaja uwekezaje wake wa kifedha na rasirimali watu huwezi kuufananisha na CCM na CDM. CDM walikuwa na Helkopta moja wenzao wa CCM walikuwa nazo mbili. Igunga kuna kata 26 hivi vyama vingine hata magari walifanya kukodisha au walikuw nayo chakavu. kwa mantiki hiyo utaona ni kwa nini mvutano ulikuwa ni kwa CCM na CDM na CUF kwa Mbaaali.

Wabunge wa CCM na CDM walikuwa wanapishana mbugani na magari yao huku wengine wa vyama hivi hata kuzindua kampeni zao walikuwa na Horn speakers tu. heri yule wa UPDP alituburudisha kwa Mayenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…