Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Siasa safi ndio msingi Wa maendeleo ya kweli kwenye nchi yoyote. Bila Siasa safi; jamii haiwezi kupiga hatua yoyote ya maana.
Hata hivyo Siasa safi ni zao la watu safi, wenye dhamira safi na matendo safi.
Ni kwa vipi tunaweza kuwa watu safi ili toka kwetu tuwe na Siasa safi na hivyo kufikia Tanzania tunayoitaka?
Usiwaze kupata vitu ambavyo huna eti ili ndio utoe mchango wako kusaidia watu na kuibadili nchi yako au hata dunia. Tumia kile ulichonacho na kile unachopata kwa kadiri kinavyojitokeza.
Mungu kamjalia kila mtu kitu Fulani, wengine wana fedha, wengine wana vyeo, wengine wana Mali, wengine wana vipaji mbalimbali ila hata kwa yule ambaye kakosa vyote hivyo, angalau ana akili. Tumia chochote ulicho nacho bila kujali ni nini na cha ukubwa gani kusaidia kujenga ustaarabu, utu na ustawi Wa mwanadamu kwenye nchi yako. Wakati ni sasa, hakuna wakati mwafaka zaidi ambao utajitokeza. Ni pale ambapo kila mtu atatia jitihada za kufanya hivyo: tutaweza kujenga nchi yenye ustawi Wa kweli.
Fikra, malengo na matendo yoyote yasiyolenga kwenye kusaidia kujenga ustaarabu na utu; hutokana na fikra za kishetani, na hakuna nchi wala jamii yoyote inayoweza kustawi kwa mawazo hayo.
Sisi watanzania ndio tutaamua hatma ya Tanzania tukianza na wewe unayesoma hapa. Anzia ulipo kwa kile ulichonacho kutoa mchango wako kuhakikisha Tanzania unayoitaka inakuwa.