Siasa na muziki hatari sana

Siasa na muziki hatari sana

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,338
Reaction score
7,183
1565012419783.png

MWANAMUZIKI wa nchini Uganda, Ziggy Wine, ambaye alikuwa chini ya usimamizi wa ‘Lebo’ ya mwanamuziki/mwanasiasa Bobi Wine, amefariki dunia usiku wa jmapili, Agosti 4, 2019.

Ziggy ambaye jina lake halisi ni Michael Kalinda, amefariki baada ya kutekwa Julai 21, mwaka huu, na kupigwa vibaya alipokuwa njiani akielekea studio za Firebase Crew. Inaelezwa kuwa baada ya watekaji kukamilisha unyama huo, walimtupa pembezoni mwa hospitali ya Mulago iliyopo jijini Kampala ambapo alikutwa akiwa amejeruhiwa vibaya huku jicho lake la kushoto likiwa limetobolewa, vidole vyake vya mkononi vikiwa vimekatwa.

Bobi Wine, Mbunge wa Kyadondo Mashariki ambaye pia alikuwa akimsimamia Ziggy kimuziki, tayari ameshazungumzia suala hilo, kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika:

“Ziggy alipatikana akiwa amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa na kuteswa, jicho lake moja la kushoto likiwa limetolewa na vidole vyake viwili vikiwa vimekatwa, na zaidi ya hapo wamemuibia kila kitu alichokuwa nacho na kisha kumtupa pembeni ya hospitali ya Mulago”.

Vyanzo vya habari nchini Uganda vimeliambia gazeti la Daily Monitor la nchini humo kuwa baada ya kutekwa na kujeruhiwa vibaya, Ziggy alilazwa katika Hospitali ya Mulago kwa zaidi ya wiki moja katika kitengo cha wagonjwa mahututi lakini hakupatiwa matibabu yoyote yanayostahili kwa makusudi, kitendo kilichofanya familia yake kulalamikia uongozi wa hospitali hiyo.

Ripoti kutoka hospitali hiyo inaeleza kuwa, Ziggy amefariki baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu ya ubongo wake, na kuwa uchunguzi wa CT Scan ulibaini kuwa kuna damu nyingi ilivujia ndani ya ubongo.
 
Sasa mbona title ya thread na content haviendani.Siasa imehusikaje hapo
 
Hakuna cha siasa na muziki wala nini,ni uchu wa madaraka wa viongozi wa Kiafrica tu
 
Lissu ni mwanamuziki? Issue ni kwamba Afrika kuna ufisi ufisi wa madaraka. Hivi ukiongoza miaka mitano au 10 siinatosha? Achia wengine wewe sio bora zaidi kuzidi wengine.
 
Mbinguni tutashangazwa sana kwa aina ya watu tutakaokutana nao kule!eti hata nduli Museven will be there
 
Yani wanaofanya haya Mungu naona anawachelewesha sn
 
Freedom came my way one day
And I started out of town, yeah!
All of a sudden I saw mr president..
Aiming to shoot me down,
So I shot - I shot - I shot him down and I say:
If I am guilty I will pay.
 
View attachment 1173024

MWANAMUZIKI wa nchini Uganda, Ziggy Wine, ambaye alikuwa chini ya usimamizi wa ‘Lebo’ ya mwanamuziki/mwanasiasa Bobi Wine, amefariki dunia usiku wa jmapili, Agosti 4, 2019.

Ziggy ambaye jina lake halisi ni Michael Kalinda, amefariki baada ya kutekwa Julai 21, mwaka huu, na kupigwa vibaya alipokuwa njiani akielekea studio za Firebase Crew. Inaelezwa kuwa baada ya watekaji kukamilisha unyama huo, walimtupa pembezoni mwa hospitali ya Mulago iliyopo jijini Kampala ambapo alikutwa akiwa amejeruhiwa vibaya huku jicho lake la kushoto likiwa limetobolewa, vidole vyake vya mkononi vikiwa vimekatwa.

Bobi Wine, Mbunge wa Kyadondo Mashariki ambaye pia alikuwa akimsimamia Ziggy kimuziki, tayari ameshazungumzia suala hilo, kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika:

“Ziggy alipatikana akiwa amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa na kuteswa, jicho lake moja la kushoto likiwa limetolewa na vidole vyake viwili vikiwa vimekatwa, na zaidi ya hapo wamemuibia kila kitu alichokuwa nacho na kisha kumtupa pembeni ya hospitali ya Mulago”.

Vyanzo vya habari nchini Uganda vimeliambia gazeti la Daily Monitor la nchini humo kuwa baada ya kutekwa na kujeruhiwa vibaya, Ziggy alilazwa katika Hospitali ya Mulago kwa zaidi ya wiki moja katika kitengo cha wagonjwa mahututi lakini hakupatiwa matibabu yoyote yanayostahili kwa makusudi, kitendo kilichofanya familia yake kulalamikia uongozi wa hospitali hiyo.

Ripoti kutoka hospitali hiyo inaeleza kuwa, Ziggy amefariki baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu ya ubongo wake, na kuwa uchunguzi wa CT Scan ulibaini kuwa kuna damu nyingi ilivujia ndani ya ubongo.
Hakuna cha siasa na muziki !! Wala siasa na uandishi, wala siasa na siasa . Ni ulafi na ubinafsi wa viongozi wa ki Africa. Kwanza kwa kujiona wao ndiyo wao. Wao ndiyo wenye akili kuliko wananchi wenyewe.

Hapa nyumbani Alphonse Mawazo hakufanya muziki. Azores hakuwa mwanamuziki. Lissu alitoka kuhutubia bunge dk 15, tena hutuba muhimu hakuwa mwanamuziki.

Tumeona UK wananchi wamepiga kura ya maoni kukataa mawazo ya David Cameron, aliachia ngazi bila makuu, Teresa May wabunge hawakupenda mapendekezo ya hakuna mbunge aliyewindwa. Africa ni sheeeda
 
Back
Top Bottom