Siasa iko CCM, wengine wasindikizaji

Siasa iko CCM, wengine wasindikizaji

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
Siasa ni mtazamo / dhana za wanasiasa (ama vyama vyao) na mapokeo ya wananchi katika mitazamo na falsafa hizo, ambazo kimsingi ndizo zinatoa mwelekeo na njia za maisha ya watu husika.

Wanasiasa ama labda niseme vyama vya siasa, vinajibainisha na kujitanabaisha kwa watu ama kundi la watu katika taswira fulani ya kuwavutia ili vipate kuungwa mkono na watu hao.

Upinzani ama niweke bayana zaidi, CHADEMA walipoanza siasa walijibainisha kuwa ni Chama cha Vijana, kikasema ajenda za vijana na kutenda matendo yaliyopendwa na Vijana na kikaungwa mkono na Vijana wengi wakati huo.

Vijana wanaathirika zaidi (youth are more influenced na entertainment industry) burudani ni miongoni mwa hitaji la Vijana. Wanamichezo, waigizaji, wanamuziki etc wana influence kubwa kwa jamii, na matendo yao huchukuliwa na jamii hata kufikia kuitwa kioo cha jamii..kwa maana jamii inajigezea na kufuata taswira yao.

Kuelekea Octoba 2015, tayari kundi la wasanii wameendelea kujibainisha kuwa si tu wafuasi wa CCM bali wameweka bayana nia zao za kutaka kuwa viongozi kupitia Chama hiko..hii maana yake nini..? Ni kuwa hakuna tena namna upinzani wakapata kuungwa mkono na vijana ikiwa wamepoteza mafungamano yao na wasanii.

2010, wasanii wa muziki, maigizo etc wote waliibea CHADEMA, Roma Mkatoliki, Afande Sele, Sugu etc waliweka wazi misimamo yao, vijana wakavutiwa nao wakaiunga mkono chadema, 2015 hali ni tofauti kabisa.,wasanii wamehakikisha wanafukia kaburi la upinzani nchini...

Watu wakimuangalia Diamond wanaiona CCM, wakimuangalia Wema wanaiona CCM, wakimuangalia Uwoya and the rest of the team, hawaoni isipokuwa CCM. Followers wao kwenye mitandao wana repost kuhusu CCM, matokeo yake kila unapotazama ni CCM.,upinzani tupa kule na watu wameshaanza kusahau kuwa tuna vyama vingi...masikio yako Dodoma, hawapitwi na taarifa ya habari kujua yanayojiri..

Sio kwa bahati mbaya, SIASA ni CCM, wengine wasindikizaji.
 
Umeshatumika kama muwa na sasa umebakia kuwa makapi tu
 
Juliana Shonza

Umeshindwa hata kuambulia ukatibu kata?pole sana kwa usaliti
 
Last edited by a moderator:
Juliana Shonza pole.Nend kasome political science japo articles tu zilizoandikwa na wanazuoni.Siasa si kama uitafsirivyo.Pole mdogo wangu rudi shule japo kidogo tu,utajua maana ya siasa.Mnavyoitafsiri siasa inawafanya watu wengine waichukie siasa na waione kama ni uongo fulani hivi.Siasa si hivyo uisemavyo.Na wala huko kwenye CCM wengi wao wala hawaelewi maana ya siasa.

Kwangu ninamuona Diomond kama diomond na si kama CCM the same to Uwoya na Wema.Kuna vijana wanaofanya vizuri kuliko hawa na wala hawajajitanabaisha kama wanachama wa vyama vya siasa,maana hata kesho wanawez kjtoka huko wakaingia vyama vya upinzani sasa sijui utawaitaje.

Hawa ni watanzania wakawaida ambao wanasababu zao za msingi kabisa kujiunga na Chama Tawala, na kuna vijana wanaofanya vizuri zaidi ya hawa.nao kwa sababu ya sababu zao binafsi wako upinzani,na wako tofauti na vyama vyao.hawaonekani kama chama wanaonekana kama watanzania wa kawaida vijana walioamua kujiunga na.vyama vya siasa kwa upinzani au CCM.

Kwa hao uliowataja sioni CCM ndani yao bali na waona ni vijana wakitanzania au wasanii wa kizazi kipya.Usiwaharibie soko la kazi zao kwa kuwafananisha na Uccm.
 
huyu dada elimu yake ni ya kiwango gani maana mambo anayoandika humu hata watoto wa shule ya msingi hawawezi kuandika upuuzi kama huu kweli njaa ni mwanaharamu
 
njaa haina baunsa mjomba .
 
laana ya usaliti usiombe mkuu , ni noma ! huyu keshaviponza hadi vitukuu vyake ( kama siyo mgumba )

Sharti la kutumika ni kutopata mtoto,hivyo huyo mtoto hawezi kuwa naye hata wa kisingiziwa
 
Juliana Shonza pole.Nend kasome political science japo articles tu zilizoandikwa na wanazuoni.Siasa si kama uitafsirivyo.Pole mdogo wangu rudi shule japo kidogo tu,utajua maana ya siasa.Mnavyoitafsiri siasa inawafanya watu wengine waichukie siasa na waione kama ni uongo fulani hivi.Siasa si hivyo uisemavyo.Na wala huko kwenye CCM wengi wao wala hawaelewi maana ya siasa.

Kwangu ninamuona Diomond kama diomond na si kama CCM the same to Uwoya na Wema.Kuna vijana wanaofanya vizuri kuliko hawa na wala hawajajitanabaisha kama wanachama wa vyama vya siasa,maana hata kesho wanawez kjtoka huko wakaingia vyama vya upinzani sasa sijui utawaitaje.

Hawa ni watanzania wakawaida ambao wanasababu zao za msingi kabisa kujiunga na Chama Tawala, na kuna vijana wanaofanya vizuri zaidi ya hawa.nao kwa sababu ya sababu zao binafsi wako upinzani,na wako tofauti na vyama vyao.hawaonekani kama chama wanaonekana kama watanzania wa kawaida vijana walioamua kujiunga na.vyama vya siasa kwa upinzani au CCM.

Kwa hao uliowataja sioni CCM ndani yao bali na waona ni vijana wakitanzania au wasanii wa kizazi kipya.Usiwaharibie soko la kazi zao kwa kuwafananisha na Uccm.
Inawezekana usiitafsir hivyo nilivyoitafsir mimi, lakini utakosea kusema kuwa wanazuoni hawatafsir hivyo, naomba mwanazuoni mmmoja ambae anakataa kuwa siasa sio perception, mmoja tu ambae sio wewe.

Pili, umesema kuwa kuna wasanii wanaofanya vizuri kuliko Diamind na akina wema na hawajawa affiliated na chama cha Mapinduzi...naomba kumjua mmoja tu.
 
Another opportumistic wasio kujua ndio wanaweza kuhangaika na hoja mgando hizo.
 
Back
Top Bottom