SIASA, FURSA NA HESHIMA by Ado Shaibu

SIASA, FURSA NA HESHIMA by Ado Shaibu

halafu kingine ni kuwa kuna vyama vimeanza kuchuja kwa kasi,...kuna mtaji wa watu huko!
hamasisheni vijana kujiunga nanyi katika mapambano ya kweli.
 
Act, tangu mwanzo mlionekana kuwa na nguvu ya hoja, itunzeni zawadi hiyo mliyoipewa na Mola wenu Mlezi. Aidha, fanyeni jitihada za kuboresha michango na hoja zenu kila siku. Kumbukeni Kwa kadiri MTU anavyotumia akili ndivyo inavyoongezeka
 
Jipendeni mwenyewe, pendaneni mwenyewe Kwa wenyewe , hii itawasaidia kufanya kazi kama timu na kuepuka kuhujumiana wenyewe Kwa wenyewe aidha, mtakuwa mmenza kuusimamia ile msingi was "utu" Kwa vitendo
 
Kama mnakumbuka mlianza kutoa taarifa za mapato na matumizi kama sehemu ya transparence, sijui ilikuaje mkaacha utaratibu ile nzuri . Hata kama mnapata elfu moja Kwa mwezi msione aibu, simamieni ile misingi
 
Inawezekana msiwe na uwezo was kufanya vitu vikubwa, fanyeni vitu vidogo lakini very smart IPO Siku mtafanya vitu vikubwa.
 
Unatakiwa pia mfahamu kwamba ili muweze kuwa na mafanikio makubwa ni lazima muwe na rasilimali fedha miongoni Kwa mambo mengine. Kwa kuwa Hanna ruzuku ni vyema mkatafuta vyanzo vinginevyo vya mapato. Moja ya chanzo cha mapato rahisi ni kutoka Kwa wanachama wenu.

Lakini, hamuwezi mkapata mapato kutoka kwenye chanzo hicho kama Hamna hao wanachama wenyewe, au mnao lakini namna uratibu, au Hanna mikakati au hamna ushawishi, na hamuwezi kuwa na hivyo vyote kama hamtakuwa smart! Au sio bwana!
 
Kama nitakuwa na kumbukumbu nzuri, act mna ngome ya wazee, vijana na wanawake, viongozi ea hizi ngome hata hawajulikani. Je, wamepewa na wanajua majukumu yao? Kwa sasa wanafanya nini? Nafikiri kama mko makini mnaweza kuona matatizo yanavyoanza.
 
Kama mnakwama kwenye mambo mbalimbali, ombeni ushauri Kwa umma, ijapokuwa wapi watakaowakejeli; wapi watakaowapa ushauri mzuri.
 
Mnajibishana wenyewe kwa wenyewe tu.
ACT ni chama cha matapeli na wezi,yule Habibu Mchange,alichukuwa hela za wapiga kura kwa mgongo wa ACT,ni wizi wa mchana kweupe
 
Halafu Ado, kuwa na heshima "muheshimiwa" ni jambo moja, lakini is not a great deal! Unaweza kufanya mambo mazuri na makubwa sana na usiheshimike vile vile. Ona sasa waliofanya mambo mazuri na makubwa duniani ama walisulubiwa au kuawa! Sasa iko wapi heshima! Suala LA muhimu ni kufanya mambo ambavyo amma yatakupa furaha wewe mwenyewe na jamii ya mwanadamu Kwa ujumla au angalau matendo ambavyo yataleta unafuu was maisha Kwa jamii ya mwanadamu inayokuzunguka, hill ndilo jambo kubwa LA kupigania.
 
Wewe, Mimi na wengine, tunatakiwa tudhamirie na kisha kuanza kufanya mambo ambavyo hata Leo au kesho tukifa, tukiulizwa tulikuwa na mchango gani duniani, tuweze kujibu, kimsingi hatuwezi kusema tulikuwa na heshima duniani pamoja na Kwa heshima ni kitu kizuri na Muhimu.
 
Unatakiwa kujitahidi kuwa kwenye position ambavyo hata likitokea dubwana likakuuliza Kwa nini usife sasa hivi, uwe na sababu za msingi za kujitetea ili likuache, sio kuliambia sory sir! Nina familia inanitegemea kana kwamba wengine hawana familia
 
Au ndio wewe mwenyewe betlehem nini? mbona unampigia chapuo sana!
Katika maisha yetu duniani, sisi ni kama wanyama tu. Tofauti yetu ni busara hekima ubunifu na jitihada zetu za kuufanya ulimwengu uwe sehemu bora ya kuishi. Kama huna kati ya sifa hizi, maisha yako hayana thamani yoyote.
 
Mnajibishana wenyewe kwa wenyewe tu.
ACT ni chama cha matapeli na wezi,yule Habibu Mchange,alichukuwa hela za wapiga kura kwa mgongo wa ACT,ni wizi wa mchana kweupe
Kwenye taasisi yeyote hata iwe ya dini wahuni hawakosekani, hiyo ndio kanuni ya kimaumbile.
Hakikisheni kuwa haipiti Siku bila kufanya kitu chenye manufaa Kwa umma (so matamko, nieleweke vizuri hapa maana hakuna MTU ambaye akiambiwa atoe tamko kuhusu chochote anashindwa) fanyeni vitu ambavyo ni objective .
 
Katika maisha yetu duniani, sisi ni kama wanyama tu. Tofauti yetu ni busara hekima ubunifu na jitihada zetu za kuufanya ulimwengu uwe sehemu bora ya kuishi. Kama huna kati ya sifa hizi, maisha yako hayana thamani yoyote.

Kama ni mtihani basi umeshafeli, umeulizwa kingine unajibu kingine.
Ujinga ndani ya busara!
 
Halafu ACt inafaa muwe na data base ya wanachama na details zao. Hizi ni hatua muhimu za mwanzo kabisa na zinazowezekana. Kwa mfano Kwa sasa mna wanachama wangapi?
 
Hakuna lolote ni njaa tu zinakutuma, tusemege ukweli basi
SIASA, FURSA NA HESHIMA
"Mwenezi kuna nini unapata ACT?"
"Wanakupa nini?"
Maswali hayo na mengine mengi ya namna hiyo ninakutana nayo mara kwa mara kutoka kwa vinywa vya wenzangu, hasa vijana. Wengine huenda mbali zaidi: "Mwenezi ni mtu mkubwa Bwana! Tugawane hivyo wanavyokupa ACT" Katika dunia ya kiliberali anayotafsiri kila jambo katika sura ya fursa ya manufaa binafsi, hayo si maswali ya kuduwaza hata punje.
Jibu langu huwa ni lilelile. Maslahi ya vitu? Hapana sipati.
Kikubwa ninachokipata ACT ni heshima. Hakuna binadamu kamili asiyependa kuheshimika. Heshima inayoshinda heshima zote ni heshima ya kuheshimu utu na mawazo ya mtu. Ninafurahi kuwa nipo kwenye taasisi ambayo kwa sehemu kubwa imeyaheshimu mawazo yangu na kuyatekeleza kama ambavyo inafanya kwa wengine. Faida hii inashinda faida ya vitu.
Faida ya pili ni kuwa katika timu inayoamini sana nguvu ya vijana. Ni fahari kubwa sana kuwa katika timu inayoamini katika kuwapa vijana jukwaa kuonyesha vipaji vyao. Sio jambo dogo kuwa katika timu inayoamini kuwa kijana mdogo asiyehitimu hata chuo kikuu anaweza kuongoza mahusiano ya kimataifa** na kwamba kijana ambaye bado anapambana na masomo yake ya chuo kikuu anaweza kuongoza timu ya utafiti ya chama***. Si jambo dogo kuwa na Sekretarieti, Chombo kikuu cha utendaji wa chama kusheheni vijana wa miaka 30 na ushei ili kuwapa vijana hawa nafasi ya kuleta changamoto mpya kwenye siasa za nchi.
Kuwemo kwenye timu ya namna hiyo ni fahari na heshima kubwa kuliko heshima butu iletwayo na vitu. Ipo Siku, heshima ya chama kwa vijana itazaa matunda makubwa. Wakati utaamua.
Ndugu Ado Shaibu
Mtaa wa Kalanje, Wilaya ya Tunduru, Ruvuma.
1 Julai 2017
.......
**John Patrick Mbozu, Katibu wa Mambo ya Nje ni Mwanafunzi wa Sheria, UDSM
***Idrisa Kweweta, Katibu wa Sera na Utafiti ni Mwanafunzi wa Shahada ya Ualimu, UDSM.

becc1a56b23eabe66376327d22476c52.jpg
 
Back
Top Bottom