Hansen Nasli
JF-Expert Member
- Mar 18, 2012
- 883
- 340
SIASA, FURSA NA HESHIMA
"Mwenezi kuna nini unapata ACT?"
"Wanakupa nini?"
Maswali hayo na mengine mengi ya namna hiyo ninakutana nayo mara kwa mara kutoka kwa vinywa vya wenzangu, hasa vijana. Wengine huenda mbali zaidi: "Mwenezi ni mtu mkubwa Bwana! Tugawane hivyo wanavyokupa ACT" Katika dunia ya kiliberali anayotafsiri kila jambo katika sura ya fursa ya manufaa binafsi, hayo si maswali ya kuduwaza hata punje.
Jibu langu huwa ni lilelile. Maslahi ya vitu? Hapana sipati.
Kikubwa ninachokipata ACT ni heshima. Hakuna binadamu kamili asiyependa kuheshimika. Heshima inayoshinda heshima zote ni heshima ya kuheshimu utu na mawazo ya mtu. Ninafurahi kuwa nipo kwenye taasisi ambayo kwa sehemu kubwa imeyaheshimu mawazo yangu na kuyatekeleza kama ambavyo inafanya kwa wengine. Faida hii inashinda faida ya vitu.
Faida ya pili ni kuwa katika timu inayoamini sana nguvu ya vijana. Ni fahari kubwa sana kuwa katika timu inayoamini katika kuwapa vijana jukwaa kuonyesha vipaji vyao. Sio jambo dogo kuwa katika timu inayoamini kuwa kijana mdogo asiyehitimu hata chuo kikuu anaweza kuongoza mahusiano ya kimataifa** na kwamba kijana ambaye bado anapambana na masomo yake ya chuo kikuu anaweza kuongoza timu ya utafiti ya chama***. Si jambo dogo kuwa na Sekretarieti, Chombo kikuu cha utendaji wa chama kusheheni vijana wa miaka 30 na ushei ili kuwapa vijana hawa nafasi ya kuleta changamoto mpya kwenye siasa za nchi.
Kuwemo kwenye timu ya namna hiyo ni fahari na heshima kubwa kuliko heshima butu iletwayo na vitu. Ipo Siku, heshima ya chama kwa vijana itazaa matunda makubwa. Wakati utaamua.
Ndugu Ado Shaibu
Mtaa wa Kalanje, Wilaya ya Tunduru, Ruvuma.
1 Julai 2017
.......
**John Patrick Mbozu, Katibu wa Mambo ya Nje ni Mwanafunzi wa Sheria, UDSM
***Idrisa Kweweta, Katibu wa Sera na Utafiti ni Mwanafunzi wa Shahada ya Ualimu, UDSM.