Siamini nilichokishuhudia: daladala level seat, hakuna foleni, hakuna kelele, abiria hawasukumani, makonda hawatukani, unafika haraka unakoenda

Kwa Hii Hesabu Yako Ndugu---

Toa Pesa Ya Boss 100,000/=,
Toa Pesa Ya Mafuta Kwa Kesho Yake,
Toa Pesa Ya Service Ya Iyo Gari Kwa Mwezi,
Toa Pesa Ya Kula Konda Na Dereva,
Toa Sio Pesa Bali Ela Ya Wapiga Debe Kwa Vituoni,
Toa Pesa Ya Konda/Dereva Kupeleka Nyumbani....

Tupe Hesabu Yake Sasa

Pandisha nauli kama ni lazima kufidia hayo. Boss ajitune kupokea hela tofauti na hiyo, zama zinabadilika.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hebu tuongee kama watu wazima wenye akili timamu, foleni inapunguaje barabarani kwa watu kukaa level seat? Sio kwamba kuna factor nyingine imehusika?
Yaani umesoma kabisa nilichoandika ukashindwa kuelewa point ya level seat in relation to daladala na foleni?
 
Yaani umesoma kabisa nilichoandika ukashindwa kuelewa point ya level seat in relation to daladala?
Mimi nimevutiwa na kipengele cha foleni barabarani kupungua in relation to level seat, nikabaki nastaajabu, level seat kwenye daladala na kupungua kwa foleni barabarani inakuwaje? Hebu nijibu inakuwaje hadi foleni inapungua?
 
Pita njia ya mbagala , temeke, buza , keko huko utakuta watu wanatembea kwa mguu je hicho ndio unakitaka? Ivi wale abiria wa mwendokasi wa kimara wanaogombania mwendokasi unahisi now wanafanyaje shuguri zao?

Sent from my iPhone using JamiiForums
Watapata suluhisho. Adha za daladala, unakuta zimejaa, cha ajabu zinasimama popote kuendelea kupakia, zikiwa kituoni au karibu na kituo zinaziba kabisa barabara kuzuia daladala zingine kwa sababu ya kunyang'ana abiria, kelele za wapiga debe kila kona, na vurugu zingine havifai kabisa.
 
Usicheze na kifo wewe.Watu tu waoga mbayaaaaaaa

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
Mimi nimevutiwa na kipengele cha foleni barabarani kupungua in relation to level seat, nikabaki nastaajabu, level seat kwenye daladala na kupungua kwa foleni barabarani inakuwaje? Hebu nijibu inakuwaje hadi foleni inapungua?
Ngoja nikupe mfano rahisi. Sasa hivi hao abiria kama 30 -- level seat, daladala inajaza kutokea kituoni, tuseme Mbagala. Ikiondoka kituoni daladala haitasimama njiani kupakia abiria, labda kama ikishusha. Abiria wanaoshuka njiani mara nyingi ni mmoja au wawili, na mara nyingi hapohapo wanapanda abiria wengine kuwareplace na gari kuondoka.

Kwa mazoea, daladala inayotoka Mbagala kwenda Kkoo inaweza kusimama mara 30+ njiani tena popote pale ilimradi kuna abiria, kila ikisimama inasababisha magari yote yaliyo nyuma nayo kusimama. Mfano mwingine, daladala imejaza lakini inaendelea kupark kituoni, magari yanayotaka kuingia kituoni hayaweza kuingia bali yanabaki barabarani maana kituoni nafasi hakuna kutokana na msongamano unaosababishwa na daladala ambazo zimejaa muda mrefu lakini hazitaki kuondoka. Sasa jaribu kufikiria matendo kama hayo yakifanywa na daladala mia kadhaa kwenye barabara moja, mfano kutoka Mbagala mpaka Kkoo.
 
1.) Foleni husababishwa tu na daladala zinazopakia abiria kituoni kwa muda mrefu?
2.) Daladala zote hushushia na kupakia abiria barabarani na si kituoni?
 
Hata hvo mie uzoefu wangu wa kuishi Dar hapa nimegundua shule zikifungwa usafiri wa daladala huwa hausumbui kabisa hata mkisimama sio kivile sa subria shule zifunguliwe huwa kisanga... Sasa hii level aeat sijui itakuaje

Suala la foleni kupungua ni wazi kuna watu hawaendi kazini mana hata jumapili hakuna foleni na daladala huwa zinapaki kituoni kama kawa
1.) Foleni husababishwa tu na daladala zinazopakia abiria kituoni kwa muda mrefu?
2.) Daladala zote hushushia na kupakia abiria barabarani na si kituoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimevutiwa na kipengele cha foleni barabarani kupungua in relation to level seat, nikabaki nastaajabu, level seat kwenye daladala na kupungua kwa foleni barabarani inakuwaje? Hebu nijibu inakuwaje hadi foleni inapungua?
Nadhani anamaanisha kuwa
1. Vituo vyetu vya daladala havina uwezo wa kupaki gari nyingi kwa hiyo daladala huwa zinapaki mostly barabarani huku zikipiga debe wakati abiri waliomo wanatosha aondoke, kitendo hicho kinasabisha jam kwa magari mengine na kuleta msongamano.
2. Kwa kuwa walikuwa hawatosheki hadi wenye nyomi daladala iliyo mbele humzuia mwenzake asipite ili kituo kinachofuata pia apige gap hii ndio issue ya kuchomekeana inaanzia hapo nayo inaimpact ya kukwaruzana na kupoteza muda kusuluhisha ugomvi hapo jam lazima.
My take.
Kwa kuwa abiri ni wale wale isipokuwa utawasomba kwa route nyingi basi pesa inayopatikana ni ile ile. Kitachoongezeka ni route huenda zikaongeza kuweka mafuta.
Lakini jam hutumia mafuta zaidi maana gari inakuwa iko ON inaenda mwendo mdogo at lower gear inatumia mafuta zaidi kwahiyo unaweza ukute unatumia mafuta mengi kuliko kurudia abiria. HILI LINAHITAJI UTAFITI
Leo niliona mambo mawili
1. Abiria wakitembea Mbagala to town
Barabara nyeupe unajikunjua dk 5 uko town hakuna jam
Hapo sijaua issue ni nini?
Kama kufunga shule zimefungwa muda, kama maofisi mengi yamefungwa sijui kama yamefungwa jana tu.
Labda tusubiri

Nadhani ameelewa. Swali la watu kutembea kwa miguu maana yake magari machache. Wajasiriamali wataliona hilo na kununua au kuongeza magari. Kutokana na hilo pia nimeona bajaji nyingi zikibeba abiria.
 
Duh hamna alietumia Kilwa road leo! Kuna foleni hio balaa
Kama kuna foleni basi itakuwa sababu zingine lakini sio kwa matatizo ya daladala tunayozungumzia hapa. Kama hayo matatizo hakuna na foleni ipo, maana yake hiyo foleni ni nafuu na ingekuwa mbaya zaidi kama ingechanganyikan na tabia za kidaladala.
 
Wanachuo wanazurura mjini bila msingi , maana tangu wao walizuia kurudi utofauti ukaanza kuonekana kuanzia maeneo yetu ya kunywa bia.

Sema swala la level seat ni zuri kwa upande wa abiria ila ni chungu kwa tajiri maana hesabu inavurugika. Ili ku cover cost ya level seat napendekeza isiwapo nauli ya 400 na badala iwe 500 kidogo kuongeza pato lao.

It is never to late to begin. Start now
 
1.) Foleni husababishwa tu na daladala zinazopakia abiria kituoni kwa muda mrefu?
2.) Daladala zote hushushia na kupakia abiria barabarani na si kituoni?

1. Wewe huelewi nini? Vituo vingi (tena karibu vyote) vina capacity ya daladala moja au mbili, zikija daladala kumi kila moja inataka kusimama na kuchukua abiria zingine zitalazimika kupark au kusimama barabarani (kumbuka wakati huo tayari zina abiria na wengine wamesimama). Tena tabia za madereva wa daladala ni kumblock wa nyuma yake ili asichukue abiria. Matatizo hayo hayatakwepo kwa sababu daladala ikiondoka kituo cha kwanza itakuwa ina abiria waliojaa gari na hivyo hakuna sababu ya kusimama ovyo njiani. Swali lako linafanana na hili "Hivi tunahangaika n corona, kwani corona tu ndio ugonjwa hatari au tatizo?". Kuwepo kwa sababu zingine zinazosababisha foleni kama vile barabara finyu, mbovu, nk., sio sababu ya kuzuia kuchukua hatua fulani inayoonyesha kupunguza foleni.

2. Hapana

Uzi wangu hauongelei foleni tu. Unaongelea afya, utu, ustaarabu, iwapo mikakati sahihi ya kubebwa abiria itazingatiwa. Jambo jingine, leseni zote za daladala zinataka abiria wote wawe wamekaa kwenye siti -- ni sheria. Sasa kwa nini isifuatwe?
 
Kumbuka shule zimefungwa.. na baadhi ya ofisi..

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimeelezea jambo linalopunguza foleni (sio kumaliza foleni, kuna matatizo mengine pia yanayochangia), na kuleta ustawi katika usafiri wa daladala:

1. Nidhamu - hakuna matusi, kelele, ugomvi, fujo vinavyotokana na makonda, wapiga debe na madereva kunyang'anyana abiria.
2. Afya ya mwili, akili na kiroho -- abiria wanakuwa na amani kwa sababu ya kutokuwepo misukosuko na bughdha ndani ya daladala iliyobeba watu na kujaa kama magogo.
3. Kuepuka maambukizi ya magonjwa mbalimbali, adha na harufu mbaya za jasho kwa sababu ya kubanana, kujali utu wa mtu/abiria kwa kumpa huduma sahihi.
 
Back
Top Bottom