Siamini nilichokishuhudia: daladala level seat, hakuna foleni, hakuna kelele, abiria hawasukumani, makonda hawatukani, unafika haraka unakoenda

Kwa nchi na raia waliostaarabika, level seat ndo hutumika
Nchi zilizoendelea sana town buses zina viti vichache kwa ajili ya wazee na walemavu wengine ni kusimama. Basi lenye leseni ya watu 90, lina seat 30 na watu 60 wasimame.
 
Nchi zilizoendelea sana town buses zina viti vichache kwa ajili ya wazee na walemavu wengine ni kusimama. Basi lenye leseni ya watu 90, lina seat 30 na watu 60 wasimame.
Mantiki ni watu wasibanane na kubebwa kama magogo. Ni sawa na gari za airport, watu wengi husimama lakini hawabanani. Muundo wa daladala na seats zake level seat ndio mpango sahihi.
 
Hata kama corona ikiisha halafu mtu akatangaza kuwa sasa daladala zinaruhusiwa kujaza watu kama magunia kama ilivyokuwa mwanzo nitamshangaa sana. Kila mtu kukaa kwenye seat yake ni tija kwa afya ya msafiri, kiakili, kimwili na kisaikolojia. Kwa mara ya kwanza leo nimepanda daladala na kwenda ninakoenda na kurudi bila kichwa kuvurugika kwa sababu ya kelele, matusi, foleni na bughdha mbalimbali za daladala na makonda wao.

Kwa maoni yangu, huu ni utaratibu ambao waziri au mamlaka zinazohusika zilitakiwa kuchukua hatua tangu siku nyingi na kuusimamia. Ndio leo nagundua kuwa foleni na misongamano vituoni na barabarani kisababishi kikubwa kilikuwa ni daladala kujaza watu kama zitakavyo -- makonda wana msemo wao gari haijai. Ukiacha COVID-19, ndani ya daladala iliyobeba watu waliojaa kama magunia ni chanzo kingine cha kuambukizana magonjwa kwa njia ya hewa na kugusana/kubanana. Adha ya kubanana huku kukiwa na joto kama tanuru kwa daladala hasa za Dar ni chanjo cha stress na frustrations kwa watu wengi.

Daladala ikishapakia watu wakajaa kwenye seats tu haisimami popote isipokuwa kama inashusha. Daladala zilikuwa zinasimama vituoni au barabarani hata kama zimejaa kwa lengo la kuendelea kubeba abiria, hili ndilo tatizo lililokuwa linasababisha barabara zipitike kwa shida. Maoni yangu ni kuwa huu utaratibu uendelee, na watu vituoni waanze kupanda kwa foleni, yaani aliyefika wa kwanza mpaka wa mwisho.

Nimeweza kufika nilikokuwa naenda haraka sana kuliko kawaida, na kutambua kumbe nilipokuwa naenda ni pafupi mno.

Pamoja na haya "matrafiki" waache tabia zao za kuongoza magari badala ya taa, hawa ndio tatizo jingine kubwa. Hivi inakuwaje trafiki anajigeuza roboti na kuanza kuongoza magari kwa mikono? Taa za kazi gani? Nilishaambiwa mapolisi hawa wa barabarani huvuta magari ya upande fulani ili kumuwahisha mtu fulani ambaye ana uhusiano naye kwa namna moja au nyingine - kiongozi, hawara, mke/mme/rafiki/etc., ni mambo ya ajabu sana! Taa zipo na zinatosha kuongoza magari, labda kama zimezima.

Abiria kukaa level seat lisiwe tu zoezi la muda kwa sababu ya COVID-19, bali liwe ni zoezi endelevu kwa sababu ni zoezi la kistaarabu, linalojali afya na utu wa abiria.
Ila hasara kwa wamiliki wa mabasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom