Si wanaume tu hata mwanamke anaweza kuoa mwanaume

Si wanaume tu hata mwanamke anaweza kuoa mwanaume

habari ya hapa

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
12,789
Reaction score
8,755
Heri ya mwaka mpya ndg zangu

Amani iwe nanyi

Naamini mko wazima wenye nguvu na afya njema, mwenzenu Niko bukheri wa afya namshukuru Mungu kwa hili.

Moja kwa moja pasi na kupoteza muda niingie kwenye lengo LA Uzi huu ni kuhusu wanawake kusubiri kuolewa huku waoaji wakiwa safarini na haujulikani lini wanarudi, kwa ufupi wamsubiri MTU asiyekuja

Suluhisho ni kwamba imefika wakati wanawake waanze kuoa tu km kuolewa umesubiri haijawa basi unaweza kuoa, kwani wengi wanaume wa Leo wanapenda kuolewa, hii itasaidia sana,

Acheni woga chumbieni tu wanaume walio tayari kuolewa wako wengi mbona, mlipie mahari na taratibu zote zifuatwe ndoa ifungwe, maisha yaendeleee

Haya ni maoni yangu ya mwaka 2018,

Itapendeza sana kuliko kulia lia kila siku oooh naomba Mungu niolewe kumbe iko ndani ya uwezo wako

Maisha mafupi sana kwakweli

Ahsanteni sana
 
Unaonekana una shida Fulani hivi! Tafuta kwanza maana ya kuoa na kuolewa.. Kuoa si kutoa mahari Bali kutoa mahari ni process za kuoa. Maana unaweza kuoa bila kutoa mahari kama huna. Anayeolewa ni mwanamke na si mwanaume. ILA mwanamke anaweza kumpa mwanaume hela ya mahari ili aitoe kwao mwanamke. Hiyo haibadilishi maana ya kuoa na kuolewa. Kifupi kuoa ama kuolewa kuna jinsia kaka...
 
Nia mnayo.. Soko lipo.. Gharama zenu.. Why worry?
Lakini msisahau mwanamke si mwanaume
 
Unaonekana una shida Fulani hivi! Tafuta kwanza maana ya kuoa na kuolewa.. Kuoa si kutoa mahari Bali kutoa mahari ni process za kuoa. Maana unaweza kuoa bila kutoa mahari kama huna. Anayeolewa ni mwanamke na si mwanaume. ILA mwanamke anaweza kumpa mwanaume hela ya mahari ili aitoe kwao mwanamke. Hiyo haibadilishi maana ya kuoa na kuolewa. Kifupi kuoa ama kuolewa kuna jinsia kaka...
Km desturi yetu ya mwanaume kuoa na hamuoi, kwa kisingizio mambo magumu, basi wanawake wana haki ya kufanya hivyo km ana uwezo huo, shida iko wapi?

Mbona nchi zingine wanawake ndio wanaooa, kwann ishindikane kwetu?

Tuendako wanaume mtaolewa tu,
 
Hamnaga vitu kama hivyo siku zote mwanaume atasimamia kwenye uanaume wake na mwanamke vivyo hivyo.

Hapo watakaokubali kuolewa ni wale wanaopenda kulelewa tu.
Usidhani dunia nzima wana desturi ya mwanamke kuolewa,

Desturi za wenzetu mwanaume ndio huolewa
 
Back
Top Bottom