Si ruhusa kwa askari kumpiga mtuhumiwa

Si ruhusa kwa askari kumpiga mtuhumiwa

Ulimbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2009
Posts
3,766
Reaction score
4,048
Nilimsikia naibu waziri wa mabo ya ndani akisema sheria inakataza kuwapiga watuhumiwa wakati wa kuwakamata au wakiwa kituo cha polisi, sasa hivi hawa wanaopigwa na askari wakati wakikamatwa, na wengine wakiwa vituoni, kama sheria hairuhusu, kwa nini haa askari/wahusika wasichukuliwe hatua?
 
Inasikitisha sana aisee!
Juzi kati nilikuwa Bukoba, lodge flani hivi tumelala usiku wa manane wakafika Polisi, wakaanza kukagua kila room na kuuliza baadhi ya maswali.

Sasa kuna chumba kama cha 3 kutoka kwangu, jamaa atatolewa nje akapandishwa kwenye gari lao. Alianza kupigwa fimbo hadi nilimsikitikia sana.

Jamaa naona aliponzwa na Kiswahili chake.
 
Hizi adithi zipo kila siku ila bado tunapigwa nani wakutisimamia tusipigwe?

Waziri mmoja aliwahi kusema "Nami nasema wapigwetu, mana-mana kwamba hamna namna nyingine"
 
Inasikitisha sana aisee!
Juzi kati nilikuwa Bukoba, lodge flani hivi tumelala usiku wa manane wakafika Polisi, wakaanza kukagua kila room na kuuliza baadhi ya maswali.

Sasa kuna chumba kama cha 3 kutoka kwangu, jamaa atatolewa nje akapandishwa kwenye gari lao. Alianza kupigwa fimbo hadi nilimsikitikia sana.

Jamaa naona aliponzwa na Kiswahili chake.

Kiswahili chake kilikuwa na tatizo gani? Alikuwa si wa nchi hii? au ndiyo kusema kama hujui kiswahili inakula kwako?
 
Zilongwa mbali, zitendwa mbali.

Cha msingi epuka mazingira ya kuwakasirisha, maana utagongwa na usomi wako wa sheria usijue unaanzia wapi kuchukua hatua.
 
Kiswahili chake kilikuwa na tatizo gani? Alikuwa si wa nchi hii? au ndiyo kusema kama hujui kiswahili inakula kwako?
Unajua Polisi wetu walio wengi wakiona Lugha ya Kiswahili inakutatiza; wanaichukulia kama fursa kwao. Isitoshe na hivi ni mpakani lazima wakusumbue.

Halafu polisi wanajiona wao ndiyo waTz halisi. Kiukweli niliumizwa na kitendo kile.
 
Dawa yao ni kidogo tu.
Unatumia lugha iliyoletwa na majahazi, hiyo lugha inawasumbua askari wengi
 
Sheria zetu zote zimeshindwa kuchora mstari wa neno NGUVU YA KADRI. au REASONABLE FORCE! Mana polis wana uhalali wa kutumia reasonable force. Tatzo mazingira ndo u determine hiyo force. How reasonable force is reasonable? Pia serkal iwekeze sn teknolojia na mafunzo kwa askar wawe na weled hasa katika upelelezi ili wapate ushahid kirahis. Kuna wakat nguv inatumika na kweli ushahid mzur ndo unapatkana. Mwafrica wa kupet pet akanyosha maelezo hajazaliwa. Mf camerra za uraian. Siraha na devices za kisasa hata satelite yao. DNA equipments. Magari na pikipik za ksasa. Helcopita kila mkoa. Khs weled mtaongeza
 
Inasikitisha sana aisee!
Juzi kati nilikuwa Bukoba, lodge flani hivi tumelala usiku wa manane wakafika Polisi, wakaanza kukagua kila room na kuuliza baadhi ya maswali.

Sasa kuna chumba kama cha 3 kutoka kwangu, jamaa atatolewa nje akapandishwa kwenye gari lao. Alianza kupigwa fimbo hadi nilimsikitikia sana.

Jamaa naona aliponzwa na Kiswahili chake.
ila we hukupigwa, unadhani kwanini mkuu?
 
Nilikuwa na kila kitambulisho walichohitaji. Na kila swali walilouliza niliwajibu kiufasaha.

Wakishaona weakness yako wanakomaa ili muongee kikubwa.

kwahiyo wewe hukuwa na weakness? nadhani ni watu kujichanganya wenyewe mkuu ingelikuwa hivyo wengine tungelishauwawa kwa vipigo ila tunaishi nao salama ka ndugu na watetezi wetu kwwenyeyale yatupasayo kuishi, tatizo wengui huwa tunatumia zaidi akili za kushikiwa
 
Back
Top Bottom