Si mchezo, tupo bahari ya sham

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,546


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema kuna kikundi cha watu wachache ambao wanabeza maendeleo yanayofanywa na Rais John Pombe Magufuli na kumuomba Rais Magufuli asikate tamaa, aendelee kufanya kazi.

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kwa nyumba za Polisi, zoezi ambalo lilifanywa na Rais Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Simon Sirro.

"Wachache ndiyo wanaobeza jitihada za Rais hata kwenye kiganja hawajai, tena ni wafuasi wa ibirisi shetani, niwaambie Rais anaitegemea 'Isaya 41', inayosema utawapepeta na upepo wa kisulisuli, Rais usiogope wanaokubeza watapeperushwa" amesema Waziri Lugola.

Awali IGP Sirro amemuhakikishia Rais Magufuli kuwa kwenye zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajia kufanyika hivi karibuni utaenda kwa amani na usalama.

"Rais nikuhakishie uchaguzi uliopo mbele yetu utafanyika kwa amani na tumejipanga" amesema IGP Sirro.
 
Akamuulize Sadam, Gadaffi, Mgabe, na wengine nao walikuwa na kauli ngumu kuliko za kwao ila leo hii ni aibu
 
Back
Top Bottom