- Source #1
- View Source #1
Kumekuwa na Picha Ambayo Inasambaa Kwenye Mtandao Wa Kijamii Ususani Facebook ikimuonesha Mshambuliaji Wa Psg Osmane Dembele Akiwa Pamoja Na Familia Yake Nchini Mali Baada ya Kuwa Ameshinda Tuzo ya Balloon Dor
- Tunachokijua
- Ousmane Dembélé ni mchezaji mpira wa Kifaransa ambaye kwa sasa anachezea League 1 ya nchini Ufaransa katika timu ya Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka 2025.
Madai
Kumekuwa na picha inayosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikimuonesha Dembélé akiwa amesimama na watu wawili na kuelezwa kuwa amekwenda nchini Mali na aliosimama nao kando ni baba yake na dada yake.
Uhalisia wa picha pamoja na taarifa hiyo ni upi?
JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kujiridhisha kuwa si ya kweli huku picha hiyo ikiwa imetengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde (AI).
Kupitia ufuatiliaji kwa njia ya mtandao unaonesha Kuwa Siku Osmane Dembele Akipokea Tuzo Nchini Ufaransa alikuwa Amenyoa Brush Tofauti Na Picha Inavyo onekana Hivyo kuthibitisha Kuwa Picha Hiyo Imetengenezwa kwa Kutumia Akili Mnemba
Sambamba Na Hivyo Ufuatiliaji umejiridhisha Kuwa Mchezaji Dembele hajachapisha taarifa yoyote kwenye kurasa zake za kijamii ikiwemo ya Instagram wala picha zinzzomuonesha yeye kuwa nchini Mali mwaka huu baada ya kupokea tuzo yake hiyo .
Vilevile ufuatiliaji zaidi umebaini utofauti wa rangi na muonekano wa tuzo ambayo mchezaji huyo ameishikilia mkononi katika picha Potoshi haifanani na tuzo halisi iliyotolewa kwa mchezaji huyo.