Si haki! 'Panya road' wametulaza saa mbili jana!

Si haki! 'Panya road' wametulaza saa mbili jana!

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
40,941
Reaction score
47,028
Huku Tabata tumelazwa mapema Sana Jana na hawa panya road, sio haki! Tunashindwa kui-enjoy nchi tuliyoijenga kwa jasho letu! Can you imagine saa mbili kila mtu ndani! Kule Mandela wamempiga mtu shoka wakamwaga utumbo! Sio haki!!!!

=======================================================================


‘Panya road' wafunga mitaa minne Dar es Salaam


kova.jpg

Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, Suleman Kova

Dar es Salaam. Ilikuwa hekaheka iliyosababisha shughuli katika mitaa minne ya Tabata, Dar es Salaam kusimama kwa saa nne baada ya kundi la vijana wenye nondo, mawe na visu kushambulia watu, kupora na kuharibu mali kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni kulipiza kisasi.

Kundi hilo la vijana zaidi ya 30 ambalo mmoja wao ameuawa linalofananishwa na lile la Panya Road ambalo hivi karibuni lilisumbua jijini Dar es Salaam, liliamua kufanya vurugu hizo Jumamosi na Jumapili baada ya ugomvi kutokea baina ya makundi mawili tofauti.

Makundi yaliyohusishwa na ugomvi huo moja ni la Tabata Kimanga, Mtaa wa Magengeni na jingine la Tabata Kisiwani, Mtaa wa Twiga.

Chanzo cha vurugu hizo zinaelezwa kuwa ni kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Alfa Mhanga, Mkazi wa Tabata Kisiwani kupigwa na kunyang'anywa simu na wenzake wa kundi jingine.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kisiwani, Herbert Haule alisema vijana hao waliingia mitaani na kujeruhi watu, kuiba na kuharibu mali walipokuwa wakilipiza kisasi baada ya mwenzao kupigwa.

Hata hivyo, Mkazi wa Kisiwani, Mwita Manofu alisema sakata zima la mkasa huo lilianza Jumamosi wakati vijana wawili waliokuwa wakiangalia mpira kuzozana hadi kupigana na mmoja wa vijana hao kwenda kutoa taarifa kwa kundi lake ambalo lilikuja kulipa kisasi.

"Unajua mmoja wa wale vijana alipopigwa alikwenda kuwaita watu wa kundi lake ambao walikuja na kuanza kuwatafuta wa kundi jingine na kuanza fujo ambazo ziliendelea hadi wakaanza kulipa kisasi kwa watu wa mtaani kwa kuwapiga," alisema.

Mama wa kijana mmoja aliyekuwa anatafutwa na vijana hao, Hadija Mhenga alisema: "Vijana zaidi ya 30 wakiwa na mapanga, visu na marungu walikuja hapa saa sita usiku na kuanza kupiga kelele huku wakitaka kuchoma nyumba moto," alisema.

Kijana mwingine, kinyozi katika saluni iliyopo Uwanja wa Twiga, Gerald Manase alisema kundi la vijana kutoka Tabata Kisiwani liliwakodi vijana kutoka Mabibo na Kigogo kuja kulipa kisasi kwa kupiga watu na kuwakata mapanga.

Askari mwandamizi wa Kituo cha Polisi Tabata Kisiwani alisema mapambano hayo yaliendelea Jumapili na ndipo kijana mmoja alipouawa.

"Kijana aliyeuawa anatokea Mabibo, si mwenyeji wa hapa Kisiwani, aliuawa baada ya wananchi kuwakimbiza vijana hao na kumshika mmoja na kumpiga hadi kufa," aliongeza kijana Manase.

Polisi Tabata Kisiwani walisema vurugu hizo zimedhibitiwa na vijana kadhaa wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa.

Shughuli zasimama

Juzi, taarifa za uvamizi mpya zilisambaa mitaani na kuwafanya wananchi kuanza kujihami kwa kufunga maduka, nyumba na biashara zote zinazofanyika katika mitaa husika.

Wakazi wa mitaa ya Mandela Juu, Tabata Twiga, Kisiwani na Makuburi, walijifungia ndani kuanzia saa mbili usiku.

Chanzo:Mwananchi
 
Huku tabata tumelazwa mapema Sana Jana na hawa panya road, sio khaki! Tunashindwa kui-enjoy nchi tuliyoijenga kwa jasho let! Can u imagine saa Mbili kila mtu ndani! Kule Mandela wamempiga mtu shoka wakamwaga utumbo! So haki!!!!

Poleni sana mkuu Francis kwa majanga ya kupewa amsha amsha ya saa mbili mkalale kama kidalipo,
ila kuna jambo naomba kuuliza, hivi hao panya #road kweli wapo au ni #myth ? kwani majibu yanayotolewaga na #kova na #IGP mangu huwa yankuwa mepesi mepesi kana kwamba hamanakitu kama hicho kwenye jamii. Noamba ufafanuzi plz.
 
Hivi hawa watoto sijui wadudu wanakuwa na silaha gani kiasi cha kufunga mtaa wa watu mia na zaidi??!!
 
Hivi hawa watoto sijui wadudu wanakuwa na silaha gani kiasi cha kufunga mtaa wa watu mia na zaidi??!!
We unasema mtaa mmoja tu! Twiga mpaka kimanga ni mitaa 20 na wote walijifungia ndani, hakuna Duka lililobaki wazi! Wamempiga mtu shoka la mgongo akafa! Usifanye masihara!
 
Poleni sana.

Wameanza tena?

Wanahitaji kupotezwa hao
 
Mi nilikuwa nishawasahau hawa panya kumbe ni uzao wao ndo umichepuka tena toba na hilo kashoka
 
Hivi hawa watoto sijui wadudu wanakuwa na silaha gani kiasi cha kufunga mtaa wa watu mia na zaidi??!!

kaka hao watu usiombe ukutane nao hao panya road yaani wanatembea km kumbikumbi na wakivamia km nyuki
silaha zao,nondo,bisibisi,misumari nk
yaani wasikie tu ni hatari na rika lao la shule kabisa mkubwa mule miaka 26 au28
vitoto vidogo
 
Huku tabata tumelazwa mapema Sana Jana na hawa panya road, sio khaki! Tunashindwa kui-enjoy nchi tuliyoijenga kwa jasho let! Can u imagine saa Mbili kila mtu ndani! Kule Mandela wamempiga mtu shoka wakamwaga utumbo! So haki!!!!

watakuwa wamekamatwa..
 
Isije ikawa ni mbinu ya kisiasa kutaka Ku divert kitu maalum. Nyie muanze kukimbizana na panya road na wao mambo zao yapite.
 
Hawa panya road badala wakavamie masaki huko
 
Tatizo majitu ya Dar es salam wana ujanja wa mdomani tu,inakuaje majitu makubwa mazima mnalazwa saa mbili na watoto hata maziwa ya pua hayajawakauka?
 
We unasema mtaa mmoja tu! Twiga mpaka kimanga ni mitaa 20 na wote walijifungia ndani, hakuna Duka lililobaki wazi! Wamempiga mtu shoka la mgongo akafa! Usifanye masihara!
Inatia hasira sana wananchi wooote nyie kufungiwa ndani na watu wasiofikia hata robo ya wingi wenu! !!!
I am mad and sad!!!
 
Back
Top Bottom