Hizi ni tuhuma ambazo hazijathibitishwa, na anaetuhumiwa hajathibitisha utetezi wake, kama ni wa kweli au anafanya kile wanachofanya wakosaji wote, kukana mashitaka hata kama wamekosa hata kama ameiba. Nadra sana mkosaji kukiri kosa mbele ya umma au vyombo vya dola.
Mtoa tuhuma alipaswa kuweka support ya tuhuma zake, kama video picha za mnato au mmoja watu wawili wengine waliyokuwa katika ndege hiyo kutolea maelezo ya kuunga mkono tuhuma hizi. Kwani hawakuwa hao wawili tu, pia hao watu aliyokuwa anazozana nao japo mmoja angekuja humu ndani athibitishe tuhuma hizi.
Nae mtuhumiwa katika ndege hiyo na huko kwote anakodaiwa kufanya fujo hakukuwa na hao Wabunge Watanzania wenzake, au hata Mkenya au Mganda anaeelewana nae aliekuwepo ndanda ya ndege hiyo ambaye hakuona hata chembe ya tuhuma hizi anazotuhumiwa mdada huyu akazikanusha yeye badala ya kusimama mwenyewe peke yake kukanusha?
Kwa nini Wabunge Watanzania na rafiki zake wamekaa kimya kwa siku zote hizi wakati mwenzao mpambanaji anachafuliwa hivi?
Kama ni kweli mama huyu katengenezewa zenge hili na hakuna ukweli wa hata asilimia 2 na kutupwa hadharani kiasi hiki, je ina maana wabunge wote wa Tanzania katika Bunge hilo hawaingii katika mitandoa ya jamii au wote wanafurahia kuchafuliwa kwa huyu mwenzao kwa tuhuma ambazo hazina ukweli hata asimilia 10 kama anavyotueleza mwenyewe mtuhumiwa?
Utetezi wa kwamba, angefikishwa polisi au angechukuliwa hatua au hata kukosekana kwa picha unaweza usiwe na msingi, kwa sababu, Huyu mama hakuwa mtu wa kawaida ni Mbunge tena wa Bunge kubwa la AFRIKA MASHARIKI lazima ana hadhi yake na ana sheria zinazomlinda tofauti na mtu wa kawaida kama ilivyo kwa mabalozi wa nje.
Hivyo hivyo, inawezekana kabisa katika ndege hiyo pamoja na yote hayo wabunge wenzake wakamhifadhi kwa heshima na taratibu za shirika hilo la ndege juu ya upigaji picha na kanuni zingine uwapo katika safari zao.