Shutuma dhidi ya Kardinali Bergoglio hazina msingi wowote!

Shutuma dhidi ya Kardinali Bergoglio hazina msingi wowote!

RGforever

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
6,877
Reaction score
5,446
1_0_673906.JPG


Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba,
kampeni za kutaka kumchafua Kardinali Jorge Mario Bergoglio, ambaye kwa
sasa ni Baba Mtakatifu Francis, zimechapishwa na gazeti moja ambalo
linajipambanua kwa kampeni chafu za kutaka kuwapaka watu matope. Ni
gazeti ambalo limekuwa likiendesha kampeni dhidi ya Makleri, kiasi
kwamba, si jambo la kushangaza kusikia gazeti hili limeibuka kwa mara nyingine tena kutaka kumchafua Kardinali Bergoglio.

Shutuma zinazotolewa na gazeti hili zinapata chimbuko lake, wakati Bergoglio
alipokuwa nchini Argentina kama Mkuu wa Shirika la Wayesuit, pale ambapo Mapadre
wawili walipotekwa nyara na kwamba, hakuweza kutoa kinga dhidi ya Mapadre hao
wasitekwe nyara.

Padre Lombardi anafafanua kwamba, shutuma hizi hazina msingi wowote. Vyombo vya
sheria nchini Argentina wakati fulani vilimhoji kuhusu shutuma hizi, lakini hakuna hata
siku moja vilipomkuta na hatia wala shitaka la kujibu. Mhusika mwenyewe alikana
shutuma hizi na kuhifadhiwa.

Padre Lombardi anabainisha kwamba, kuna vielelezo na ushahidi mkubwa kutoka kwa
watu mbali mbali wanaonesha kwamba, Bergoglio aliwalinda na kuwapatia hifadhi
wakati wa madhulumu nchini Argentina, pale nchi ilipokuwa inatawaliwa kwa mtutu wa
bunduki.

Mchango wa Bergoglio unafahamika sana, pale alipoteuliwa kuwa Askofu, alipoanzisha
mchakato wa kuomba msamaha kwa ajili ya Kanisa la Argentina kwamba, wakati wa
madhulumu, Kanisa Katoliki halikujishughulisha sana kuwalinda na kuwatetea
wanyonge na wote waliokuwa wanadhulumiwa na utawala wa Kidikteta.

Mchango wa Bergoglio unafahamika sana, pale alipoteuliwa kuwa Askofu, alipoanzisha
mchakato wa kuomba msamaha kwa ajili ya Kanisa la Argentina kwamba, wakati wa
madhulumu, Kanisa Katoliki halikujishughulisha sana kuwalinda na kuwatetea
wanyonge na wote waliokuwa wanadhulumiwa na utawala wa Kidikteta.

Shutuma hizi zinafumbatwa katika upembuzi yakinifu wa masuala ya kihistoria na
kijamii wakati wa utawala wa kidikteta, zilizofanywa na makundi dhidi ya Makleri, kama
njia ya kulishambulia Kanisa. Shutuma zote hizi hazina msingi na lazima zipingwe kwa
kauli moja. Ndiyo Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican anavyohitimisha
maneno yake dhidi ya shutuma zinazolenga kumpaka matope Kardinali Bergoglio.
 
hata wakimchafua sisi wenyewe wakatoliki tumemkubali kwa hiyo kwetu ataendelea kuwa msafi........
 
Sawa tumeskia ! Tutaskia mengi sana pia alitaka kuoa akiwa na miaka 12 na sijui kale ka tunda ka Eden kama hajakang'ataaaa !

Source; Mwananchi la leo
 
Back
Top Bottom