Shuleee naipenda, shule naipenda shuleee naipenda

torvic

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
3,805
9,294
Wakuuu!


shuleee naipenda, shule naipenda shuleee naipenda, shule naipenda shuleee naipenda... hahahah
Weweee mimi nilikuwa nachukia skuli vibaya, sana sana nilivyokuwa primary, nilikuwa muoga wa bakola hatari!
simnajua walimu wa hisabati wanavyojua kuharibu siku ya mwanafunzi, nilikuwa nikimuona mwalimu kiwango tu! mood ya shule yote inakata hata kama sijafanya kosa
kwa sekondary nilikuwa nasoma kwa interest ya baadhi ya masomo na hapo kidogo shule ilikuwa inanoga, darasa nililokuwa nasoma lilikuwa na vituko balaa kwaiyo niliipenda kwa sababu ya vituko vya wanafunzi wenzangu
na baadhi ya masomo yalinifanya niipende shule.

Sasa huyo nilikuwa mimi torvic, wewe vipi?? shule ilikuje kwako?? uliipenda au uliichukia?? kama uliipenda ni kwa mambo gani yalikufanya uipende?? na kama uliichukia ni kwa sababu gani uliichukia??

wakuuu!
 
kiuno changu chembamba cha kuvalia mkanda dereva wangu................shule naipenda shule aah
 
Shule niliipenda na ninaipenda mwanzo mwisho.....Siwezi kuchukia kitu kilichonisaidia KUSOMA,KUANDIKA NA KUHESABU (KKK)
 
Niliipenda shule kwanza nilikuwa nakuwa mwalimu wa muda kuwaandikia wenzangu notice maana nilikuwa na mwandiko wa kupendeza, pili nilikuwa mtunza stoo kwa uaminifu wangu nikapewa jukumu hilo la kuhakikisha nalinda na kutunza mali za shule, ila sikupenda Maths hadi sasa huwa sitaki kuisikia kipind mwalm anafundisha Maths nilikuwa nahangaika kuhakiki stoo kama iko salama.

Shule niliipenda sana nitarudi ngoja huu mwaka upite
 
Primary nilikuwa sio msomaji kabisa,nilikuwa naenda shule basi tu

Secondary nilikuwa napenda sana maths&physics yaani kila nilipo lazima nasoma hayo tu

Sijawahi kuichukia wala kuipenda shule asee
 
nliipenda shule hata kabla sijaianza..but nlivofika la pili viboko vikaanza...nkaanza kuichukia..
nawakumbuka umoja primary..kama sio pale ningekuwa kilaza leo
asante mwalimu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom