Shule zikifungwa ni muda mzuri wa kuelewa maana ya kuwa mzazi

Bado hujajua kwa nini yale majagi ya vioo yamepungua manyumbani sa hivi ni mwendo wa plastics tuuu.Bado remote, simu, havijaoshwa na Maji. All in all ni kumshukuru Mungu tuu Kwa kua kuna watu hawana watoto, kuna watu wanawatoto hawawezi kutembea mpaka wasogezwe. Ukiwa na watoto watundu mshukuru Mungu Sana. View attachment 1118302
Changudoa mpya mtaani
 
Likizo iliyopita mze akaniambia niwapeleke wajukuu zake, tena kama D wa jina lake amemmis sana, nikasema sawa......likizo hii hapa wakaenda baada ya wiki tu naambiwa wameshatengeneza hasara ya kutosha, wameua bata wa jirani, wamemvunja mkono mtoto wa mpangaji wa mzee pia wamepasua kioo cha TV yake, wamevunja kioo cha dirisha la nyumba ya jirani...... Hitimisho la mzee akaniambia niwafuate maana keshachoka nao ndani ya hiyo wiki moja tu!!!
Mwambie mzee likizo ndiyo imeanza bado wana mwezi
 
Mimi ni vyombo vya ndani, ninauliza hivi sahani itakuponyikaje ukiwa mwangalifu? Sasa wakishavunja wanasema mama samahani nilisahau kuwa mwangalifu.

Likizo ikiisha inabidi ubadilishe set ya jikoni. Unakuta mabakuli na sahani zimebaki mbili.
sahani ya kijivu,kikombe chekundu,kisosi cheupe...ni mwendo huo wa vyombo ndani na wanavyojua kuvunja kwa mpangilio,watavunja viwili kwenye set ya visos,sahan watavunja 4,vikombe watavunja mikono 6...Alafu wakat unawagombeza unaskia mlango unagongwa,ni shangazi yao kaja na dada ako Unawapakulia chakula kila mtu sahani ina rangi yake.
 
iko fursa katika eneo hili kuna wazazi hawapendi kabisa watoto wao wawepo nyumbani hivyo ukiandaa eneo lenye usalama na watoto wakaweza kushinda hapo kwa gharama nafuu kiukweli utapiga hela.
Kuna jamaa kaanzisha hapa Sinza Kwa Remy panaitwa Kuala Lumpur pako vizuri sana
 
Ila katika vitu vyote mm hua wananikera ni kuchora kuta yaan kidume umepaka rangi ya bei ndani unakuta mwanangu kajipinda anachora apple
Mkuu na wewe umepitia hayo, kama si kuchafua rangi basi ulikuwa na yako, kwa hakika ni maisha ambayo mtoto anainjoi haswaa, sote tumeyapitia, inapokuwa kuna uharibifu unafanyika basi tukae nao tuongee nao na tuwafahamishe pia ubaya na madhara ya baadhi ya michezo naamini wataelewa.
 
IMG_0596.JPG

Mwenyewe anaita crown
 
Nakumbuka miaka ile tupo primary mnyoo maarufu wa panki uliingia enzi izo sasa mimi mdingi alikuwa mkuda sana na mkoloni kweli kweli
Watoto wenzangu uswahilini wengi wamenyoa panki na ikabidi nitumie mbinu za kijajusi kumsawishi dingi aniruhusu ninyoe
Sasa wakati tupo likizo nikamfata dingi eti nikamwambia "baba mwalimu amesema likizo hii tunyoe kama madenge ili tuwe na akili sana" (madenge ni yule katuni wa kwenye jarida la sani, kwa wasiomfahamu) dingi alicheka sana akanizaba bonge la kibao "shenzi kabisa unataka kuwa muhuni"
Tokea siku iyo nikawa nataniwa sana na wenzagu na dingi ndio tani lake kubwa kwangu mpaka leo tukiwa tunakumbushana mambo ya zamani hahahaha
 
Kuchora kutani wanunulie madaftari ya kuchafua tu kwetu sisi madogo wote wana madaftari ya kuchafua.Full kuchora makatuni
Mkuu madaftari ya kuchora wanayo tena nimetenga kwa ajiri ya home tu sio tution wala shule ila ni fujo tu na utoto nadhani.
 
Nakumbuka miaka ile tupo primary mnyoo maarufu wa panki uliingia enzi izo sasa mimi mdingi alikuwa mkuda sana na mkoloni kweli kweli
Watoto wenzangu uswahilini wengi wamenyoa panki na ikabidi nitumie mbinu za kijajusi kumsawishi dingi aniruhusu ninyoe
Sasa wakati tupo likizo nikamfata dingi eti nikamwambia "baba mwalimu amesema likizo hii tunyoe kama madenge ili tuwe na akili sana" (madenge ni yule katuni wa kwenye jarida la sani, kwa wasiomfahamu) dingi alicheka sana akanizaba bonge la kibao "shenzi kabisa unataka kuwa muhuni"
Tokea siku iyo nikawa nataniwa sana na wenzagu na dingi ndio tani lake kubwa kwangu mpaka leo tukiwa tunakumbushana mambo ya zamani hahahaha
Ulisahau kuwa dingi alizaliwa kabla yako 😂
 
Back
Top Bottom