Shule zikifungwa ni muda mzuri wa kuelewa maana ya kuwa mzazi

Likizo iliyopita mze akaniambia niwapeleke wajukuu zake, tena kama D wa jina lake amemmis sana, nikasema sawa......likizo hii hapa wakaenda baada ya wiki tu naambiwa wameshatengeneza hasara ya kutosha, wameua bata wa jirani, wamemvunja mkono mtoto wa mpangaji wa mzee pia wamepasua kioo cha TV yake, wamevunja kioo cha dirisha la nyumba ya jirani...... Hitimisho la mzee akaniambia niwafuate maana keshachoka nao ndani ya hiyo wiki moja tu!!!

sidhani kama atarudia kuwa miss tena
 
Hivi hawa watoto wanafanana wote, tena ukikuta wanaangalia hizo cartoons zao wapo kimya kama vile baadae wataulizwa maswali.
Kuna mmoja leo asubuhi asubuhi anakuja kuniuliza "baba niwashe TV".

Nilijua cartoon za Sophia the first, ben ten na zingine. Ilibidi niwe naungana nae kuziangalia ili nijue maudhui yaliyomo kwenye hizo cartoon. Nyimbo za vidudu ndo usiseme Esta arodia I say come here shake body . John John yes papaa, eat sugar no papaa
 
Mimi nimeshagombana sana na mama yangu na dada zangu sababu ya watoto,there is limit to everything. Wa kwanza wa kike miaka 8,wa pili wa kike miaka 6 wa mwisho wa kiume miaka 3 ila wameshakula kipigo cha mikanda,fimbo,makofi,waya,kandambili yaani ujinga nakamata nachapa makalio kidogo wakifanya ujinga ukiwatazama tu wanaacha,imesaidia kupunguza kwakweli ila sio kumaliza maana Tv imekua yao,meza zimevunjwa mpaka sasa nawatazama tu,radio tena huyu wa kiume ameshaziua mbili kwa kumtafuta anaeongea humo ndani,Tv wameshaua moja,ukuta siongei,chooni kwao sink wameshavunja yaan basi tu sema ndio furaha ya kua nao na nikiwa mbali nao namiss vurugu zao.
Nimegundua watoto wa kiume ndio wakorofi sana wa kike wa pole kidogo,ila mimi nisingepigwa vyema nisingenyooka na wao inabidi tu nijikaze niwanyooshe mapema ila kwa kipimo
 
Back
Top Bottom