Shule za Ufundi (Technical Schools): The lost treasure

Shule za Ufundi (Technical Schools): The lost treasure

SAKO LA NYANI

New Member
Joined
May 17, 2013
Posts
3
Reaction score
1
Naomba kuleta mada hii ubaoni wadu japo tupate kujadili kwa mapana.

Nakumbuka kipindi nasoma sekondari miaka ya 90's ,mnapofika darasa la saba karibu na kumaliza kunafomu tulikuwa tunazijaza kama sikosei zilikuwa zinaitwa TSM9. Pale tulikuwa tunajaza shule ambazo mtu ungependa uchaguliwe kwenda kuendelea na masomo ya sekondari.

Nakumbuka tulikuwa tunachagua shule za sekondari mbili naya ufundi moja, nahata matokeo yalikuwa yakitoka unakuta kuna waliochaguliwa kwenda sekondari za kawaida na wale wanaokwenda shule za ufundi kama Mtwara Tech, Moshi Tech, Ifund Tech, Tanga Tech nk.

Na wanafunzi waliokuwa wakitoka kwenye hizi shule baada ya kumaliza form four walikuwa ni mafundi wazuri tu na hata wengine waliobahatika kwenda kusomea ualimu ndio walikuwa walimu wazuri sana wa masomo ya sayansi katika shule zetu za sekondari wakati ule kama Azania, Ilboru, Kibaha nk, lakini leo hii hizi shule hata hazipo tena kwenye nyuso za wanataaluma.

Swali langu kwa serikali ni je imeshindwa kuziendeleza hizi shule za ufundi? Na pia kwa maanguko haya ya matokeo ya kidato cha nne kwa miaka ya karibu hasa katika masomo ya sayansi serikali inajifunza nini kapo.

Pia shule hizi zilikuwa zinawafanya vijana wengi wanaotoka kwenye hizi shule waweze kujiajiri wenyewe hata kama hawakufanikiwa kuendelea na masomo ya juu zaidi.

Inaniuma sana kuendelea kuandika kwani hizi shule zilikuwa zina tija kubwa sana kwa taifa letu la Tanzania.
 
Baada ya mafisadi kuona watoto wao hawana vigezo vya kwenda ilboru, tabora boys, wakaona deal ni kuzitekeleza tu
 
Wamezitupa kama walivyokuwa wametupa reli na treni baadaye watakuja ona umuhimu wake na kusema walikosea.mzungu hakuwa mjinga kutujengea shule za secondary za ufundi na vifaa vyake.

Pia kuna shule kama ashira na zanaki za wasichana zilikuwa na mchepuo wa needlework na cookery. Ukienda haya madarasa utafurahi walivyokuwa wameweka vifaa kuanzia cherahani za mezani, za umeme, majiko ya umeme makubwa na ya gesi.

Sina hakika kama nazo zinaishi. Shule hizi zinasaidia kuwapa vijana elimu ya kujiajiri wanapomaliza kidato cha nne.
 
Raisi wa kwanza wa Tanzania alianzisha shule za ufundi (not veta), shule hizi zilijidhatiti kukidhi mahitaji mbali mbali ya nchi, shule hizi ziliandaa watu wa kada mbali mbali- mafundi makenika, umeme, ujenzi, madereva, maselemala nk.

Licha ya shule hizi kuandaa mafundi mbali mbali kwaajili ya viwanda, pia shule hizi zinaandaa wanasayansi, nasema hivi kwa sababu, masomo yanayofundishwa katika shule hizi ni ya sayansi na ufundi hivyo kuandaa watu kwaajili ya kazi za kisayansi (madaktari, mainjinia nk)

Shule hizi zilikuwa zinafanya vizuri sana katika nyanja ya elimu, kila mwaka zilikuwa zinashika nafasi za juu kwa ubora wa elimu.

Nakumbuka shule hizi kutoa division one hata 100 na zero moja au mbili au wakati mwingine bila ziro kabisa haikuwa kazi ( waliosoma shule hizi miaka ya 2007 kurudi nyuma mnalifahamu hili).

Lakini kadri miaka inavyo songa mbele hadhi ya shule hizi inapungua kiasi kwamba idadi ya division zero inakuwa kubwa kuliko division one na two kwa pamoja.

Hoja ni kitu gani kimezikumba shule hizi?

Shule zinazo zungumziwa ni kama:

Ifunda tech,
Iyunga tech,
Moshi tech,
Tanga tech,
Mtwara tech,
Musoma tech,
Bwiru boys
 
Dah . . ..yaani hizi shule siku hizi sio kabisa, wizara ya elimu, wadau na hata wazazi wanaona lakini kinachoendelea ni nini ?
It's a lost treasure
 
Zipo wapi shule zetu?
Ipo wapi Moshi tech?
Ipo wapi Tanga Tech? Ifunda Tech?, Bwiru Boys, Musoma Tech n.k..
 
Tanga Tech nimepita apo nyuma kidogo nasikia hali ni mbaya sana sio practical wala theory
 
Zipo wapi shule zetu?
Ipo wapi Moshi tech?
Ipo wapi Tanga Tech?, Ifunda Tech?, Bwiru Boys, Musoma Tech n.k..
Hizo zingine umeziongeza siyooo. Shule za ufundi haswaaaa zilikuwa hizi zifuatazo:
1. Ifunda Technical Secondary School
2. Tanga Technical Secondary School
3. Mazengo Technical Secondary School
4. Mtwara Technical Secondary School
5. Moshi Technical Secondary School
 
Mh wako busy na wanufaika wa bodi ya mikopo sasa wanaandaa muswada makato iwe 15% nadhani hiyo ndo changamoto aliyoamua kuanza nayo
 
Aliyezifisha shule za ufundi ni wa kumsamehe tu. Hakuwa na maono sana.

Sote tunakumbuka namna ambavyo shule zilizokua na michepuo ya ufundi zilivyokua zikitoa wataalam kwenye kada hiyo.

Tanga technical, Arusha Technical na nyinginezo ziliongoza. Baada ya kufa kwa hizo shule sasa imekuja Veta kuchukua nafasi lakini sidhani kama wamefanikiwa kukidhi haja ya wataalam wa ufundinwa viwango vya juu kama shule hizo zilivyokua zikifanya miaka ile.

sio jambo baya kuzifufua ama kuzipa kipaumbele kurudia sifa na faida zake za zamani.
 
Wataje kabisa hao wauaji wa hizo shule. Huku wanajigamba kuwa wanamfuata Mwl. Shida tuliyo nayo si kuanzisha zile shule. Hawakuyauza majengo.

Shida ni je, tutapata wapi waalimu? Wale weshaji fwilia kabisa, hata PF yao imesha ondolewa. Sasa, tuanzishe shule au somesha wataalam tena Bulgaria na Urusi??

Tatizo ni wataalam sio shule.
 
stroke najaribu kuangalia kama naweza kuanzisha special program kwenye high school zaidi kitu kama vocational high school ktk software program za oil and gas operations ili mtoto akimaliza high school awe na soft and hard skills za kufanyia kazi i would be curious to get your views on this.
 
wewe ni waziri wa elimu?
 
Mkuu inavyoelekea hilo ni eneo lako la utaalam. Ingawa ningependa kuona ukipanua ufahamu wako kwa kuangalia namna ya kutoa ufundi wa mafunzo ya msingi ya awali ili kila mhitimu awe na uwezo wa matumizi teknolojia ya teknohama katika nyanja mbalimbali, ukitilia mkazo na hilo.
 
fafanua kidogo unamaanisha eneo gani microsoft ofice such as powerpoint, excell & word!!!
au ufundi wa aina gani?? nataka niwe nawapa basic knowledge ya mafunzo mafupi ili waende kukamata kazi kwani nimezifanya kazi hizo na haziitaji degree wala ingawa kama mtu akipenda anaweza kuendelea na mafunzo ya juu zaidi.
Taifa letu linaitaji middle class na hizi ndio kazi zake na taifa linaitaji nguvu kazi kwani work is the road to salvation and also great therapy
 
Hii nchi kila kitu kilifika sehemu kikawekwa kando na vitu vya maana kama elimu iliwekwa rehani mwa wajanja wanaojua biashara. Enzi zile shule hizi zilikuwa bora sana, mimi nilisoma kipindi cha mwisho mwisho wakati shule hizo ndio zinaelekea kudhoofika japo kulikuwa na unafuu tofauti na kipindi hiki.

Kilichoziharibu shule hizi; pamoja na ukosefu wa walimu na ubovu wa miundombinu, vilevile watoto wanaochaguliwa kupelekwa shule hizi kwa sasa hawana uwezo wanapelekwa tu kwa hisani ya headmaster na kujuana pamoja na maagizo ya baadhi ya viongozi.

Kwa sasa Waziri ametangaza kuzifufua shule hizi, tusubiri na nashauri wanafunzi wenye sifa sitahiki yaani waliofauli hisabati kwa kiwango cha juu zaidi ndio wapelekwe shule hizi tofauti na sasa mambo yanaenda visivyo.
 
Hizo zingine umeziongeza siyooo.... shule za ufundi haswaaaa zilikuwa hizi zifuatazo..
1. Ifunda Technical Secondary School
2. Tanga Technical Secondary School
3. Mazengo Technical Secondary School
4. Mtwara Technical Secondary School
5. Moshi Technical Secondary School
Mpaka mwishoni mwa miaka ya 1990s shule za umma za ufundi zilikuwa kama ifuatavyo;
Moshi technical
Tanga technical
Ifunda technical
Mazengo technical
Mtwara technical
Msoma technical
Bwiru boys
Iyunga technical
Shule zote saba hapo juu zipo isipokuwa Mazengo ambayo imebadilishwa kuwa chuo cha St. John.

Na kulikuwa na shule moja ya private iliyokuwa inaitwa Minja technical sina uhakika kama bado ipo.
 
Tajeni na zile za jumuiya wa wazazi
 
Naomba kuleta mada hii ubaoni wadu japo tupate kujadili kwa mapana.

Nakumbuka kipindi nasoma sekondari miaka ya 90's ,mnapofika darasa la saba karibu na kumaliza kunafomu tulikuwa tunazijaza kama sikosei zilikuwa zinaitwa TSM9. Pale tulikuwa tunajaza shule ambazo mtu ungependa uchaguliwe kwenda kuendelea na masomo ya sekondari.

Nakumbuka tulikuwa tunachagua shule za sekondari mbili naya ufundi moja, nahata matokeo yalikuwa yakitoka unakuta kuna waliochaguliwa kwenda sekondari za kawaida na wale wanaokwenda shule za ufundi kama Mtwara Tech, Moshi Tech, Ifund Tech, Tanga Tech nk.

Na wanafunzi waliokuwa wakitoka kwenye hizi shule baada ya kumaliza form four walikuwa ni mafundi wazuri tu na hata wengine waliobahatika kwenda kusomea ualimu ndio walikuwa walimu wazuri sana wa masomo ya sayansi katika shule zetu za sekondari wakati ule kama Azania, Ilboru, Kibaha nk, lakini leo hii hizi shule hata hazipo tena kwenye nyuso za wanataaluma.

Swali langu kwa serikali ni je imeshindwa kuziendeleza hizi shule za ufundi? Na pia kwa maanguko haya ya matokeo ya kidato cha nne kwa miaka ya karibu hasa katika masomo ya sayansi serikali inajifunza nini kapo.

Pia shule hizi zilikuwa zinawafanya vijana wengi wanaotoka kwenye hizi shule waweze kujiajiri wenyewe hata kama hawakufanikiwa kuendelea na masomo ya juu zaidi.

Inaniuma sana kuendelea kuandika kwani hizi shule zilikuwa zina tija kubwa sana kwa taifa letu la Tanzania.

Pamoja na faida zake, lakini pia shule hizi zilikuwa na hasara moja kubwa yaani ile ya kumchagulia fani mtoto mapema mno kabla hata hajatambua uwezo na matamanio yake atakapokuwa mtu mzima!

NB: Na kibaya zaidi ni kwamba zilikuwa zinachukua 'cream' ya watoto wetu na kuwafanya mafundi kana kwamba mafundi tu ndo wanatakiwa wawe na akili kuliko hata madaktari, wanasayansi na wanasheria!
 
Back
Top Bottom